Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 6 Dhu al-Hijjah 1444 | Na: 1444 / 42 |
M. Jumamosi, 24 Juni 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mpango wa Kufufua Uchumi Hauwezi Kumaliza Mgogoro wa Kiuchumi Unaokua. Mpango huo tiifu kwa Mfumo wa Kimataifa wa Kibepari.
Inafungua Njia kwa Ukoloni Zaidi wa Kiuchumi wa China kwa Pakistan
(Imetafsiriwa)
Taarifa moja kwa vyombo vya habari iliyotolewa na serikali ya Pakistan mnamo Juni 20, 2023 ilitangaza mpango mpya wa kufufua uchumi. Kimsingi unaungwa mkono na uongozi wa jeshi, na kupewa lakabu ya "Kanuni ya Asim Munir." Katika mpango huu, imedaiwa kuwa Baraza la Uwezeshaji Uwekezaji Maalum litaundwa ili kukuza uwekezaji kutoka nchi nyingine katika sekta za ulinzi, kilimo, mifugo, madini, nishati na teknolojia ya habari. Ni kutoa mfumo toshelezi ili kuwawezesha wawekezaji kwa kutatua vikwazo vya urasimu.
Hata hivyo, kinyume na madai yake, Mpango wa Kufufua Uchumi hautaweza kutatua mgogoro wa kiuchumi. Hautaleta ustawi wowote kwa nchi pia. Hata kama ahadi za miaka mingi za uwekezaji wa dolari bilioni chache zitatimizwa, hazitatosheleza kwa miaka mitatu ijayo, kufidia wastani wa kila mwaka wa dolari bilioni 35 za deni na malipo ya maduhuli.
Pakistan bado inayumbayumba kutokana na "mabadiliko ya mchezo" uliopita, Ukanda wa Kiuchumi wa Pakistan na China (CPEC). CPEC iliinasa sekta ya nishati ya Pakistan katika mtego unaoongezeka wa madeni. Ilimomonyoa uwezo wa serikali kununua umeme katika joto kali la kiangazi, licha ya kuwa na uwezo wa kuzalisha. Pakistan sasa inazama katika deni la China, ambalo China inapata riba kwa jina la upanuzi wa deni. China yenyewe inapanga kutupilia mbali sekta yenye thamani duni ya chini nchini Pakistan, ili kuruhusu umakini zaidi wa uchumi wake kwenye teknolojia ya kisasa na bidhaa zenye thamani ya juu. Aidha, kazi za kiwango cha juu katika sekta hii ya bidhaa zenye thamani ya chini hukabidhiwa kwa raia wa China. Hili linadhihirika katika miradi mbalimbali ya uwekezaji ya China nchini Pakistan. Jeshi la Pakistan lililazimika kuunda kikosi kipya cha usalama kulinda vitega uchumi vya China nchini Pakistan.
Kwa hiyo, baada ya kusalimisha uchumi wa Pakistan kwa ukoloni wa China kwa jina la CPEC, Mpango wa Kufufua Uchumi wa uwekezaji zaidi wa China, utatudhoofisha zaidi kabla ya ukoloni wa China.
Mpango wa Kufufua Uchumi ni jina jipya la ubinafsishaji. Mali muhimu ya Pakistan itakabidhiwa kwa wawekezaji wachache ili kupata dolari. Bandari, viwanja vya ndege, au ardhi za kilimo kwa jina la kilimo cha ushirika zitapotea. Pia kuna madini ya thamani ya kupotezwa kwa makampuni ya Magharibi au ya Kichina, pamoja na mradi wa Reko Diq wa kampuni ya Barrick Gold Corporation. Dolari zitakazopatikana kwa kuuza mali hizi zitalipwa China au nchi za Magharibi, kwa njia ya mikopo na riba.
Kujenga uchumi wa nchi kupitia Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI) ni muundo wa kiuchumi uliofeli. Baada ya uwekezaji wa awali, nchi na makampuni haya huregesha faida katika nchi zao kwa dolari kila mwaka. Kwa kweli, baada ya miaka michache, uhamishaji wa kinyume kinyume wa mtaji huanza. Hata leo, Benki ya Kuu ya Pakistan imezuia kwa muda faida ya makampuni ya kigeni, yenye thamani ya takriban dolari bilioni moja, kuondoka nchini, kutokana na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni.
Wawekezaji wa kigeni wanatumia rasilimali, wafanyikazi, mazingira na sheria za nchi zetu. Wanatengeneza bidhaa kwa ajili ya masoko yao wenyewe, badala ya kutengeneza bidhaa ambazo Pakistan inahitaji. Nchi na kampuni za kigeni hazihamishi teknolojia yoyote muhimu, kama ilivyo kwa viwanda vya kuunganisha simu na magari nchini Pakistan. Kwa jina la hati na haki miliki, makampuni haya yanasisitiza kuwekeza, badala ya kuhamisha teknolojia. Kwa hivyo yanaongeza utajiri wao kwa kufaidika na masoko ya nchi zengine.
Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Tunakuulizeni, mtaendelea kuvumilia hadi lini mfumo huu mbovu na uliofeli? Mfumo huu wa kikoloni uliundwa na wakoloni wa Magharibi ili kuwafanya Waislamu kuwa watumwa, baada ya kuvunjwa Khilafah. Hautaleta kheri yoyote. Sasa mfumo huu umeporomoka, je hamtauzika sasa, kwa kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume? Je, sio wakati wenu sasa muunusuru mradi wa kweli wa mabadiliko?
Mradi wa kuunganisha Ulimwengu wa Kiislamu kupitia kuasimamishwa kwa Khilafah utaleta ustawi mkubwa kwa Umma wa Kiislamu. Umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu na ruwaza ya kimapinduzi ya Uislamu, itatusimamisha kwa miguu yetu wenyewe ndani ya wiki na miezi michache. Jitokekezi na mutoe Nusrah yenu kwa ajili ya kusimamisha Khilafah. Ondoa nusra yenu kutoka kwa mfumo huu, na mupate mafanikio hapa duniani na kesho akhera kwenu na Ummah wenu kupitia kusimamisha tena Khilafah.
Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |