Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 10 Shawwal 1443 | Na: 1443 / 62 |
M. Jumanne, 10 Mei 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mfumko wa Bei Uliovunja Rekodi! Chini ya Demokrasia, Nyuso Zinabadilika lakini Mateso ya Watu Yanabakia. Sera ya Mapinduzi ya Sarafu ya Kiislamu ya Khilafah Itakomesha Mfumko wa Bei Unaovunja Mgongo
(Imetafsiriwa)
Je, ni tofauti gani hasa iliyofanya kwa mateso ya watu kwamba serikali ya Bajwa-Imran imeondoka na serikali ya Bajwa-Sharif imewasili? Kando na mfumko wa bei wa juu zaidi katika miaka miwili na nusu, ni nini kingine ambacho watu wamepata ndani ya mwezi mmoja wa mabadiliko ya hivi karibuni katika nyuso za waporaji, wasaliti na wale wanaougeuza uchumi wa Pakistan kuwa kitega uchumi kwa mafia wa riba? Mara baada ya jina la Waziri wa Fedha kuondolewa kwenye Orodha ya Udhibiti wa Kutoka, alikimbilia mlango wa nani? Je, IMF sio taasisi ile ile ya kikoloni ambayo maagizo yake ya sumu yameangamiza uchumi wa Pakistan mara 21 nyuma? Iwe ni serikali ya Bajwa-Imran au serikali ya Bajwa-Sharif, sera chini ya Demokrasia zinasalia kuwa zile zile. Sumu ya polepole iliyopeanwa kwa jina la matibabu ni ile ile. Maagizo ya mfumo wa kirasilimali na IMF ni yale yale. Kwa hivyo mtu yeyote mwenye akili timamu anawezaje kutarajia matokeo tofauti chini ya Demokrasia? Hata kama Imran Khan ataruhusiwa kufikia kutawala tena, hakutakuwa na mabadiliko.
Mfumko wa bei ni sifa ya kudumu ya mfumo huu wa kirasilimali kwa sababu Benki ya Kuu ya Pakistan kila mara hupanua sarafu ya isiyo na thamani ya kidhati katika mzunguko, kusababisha mikopo kupitia vyombo vya madeni, ikilinganishwa na bidhaa na mali, kupitia shughuli za uchapishaji pesa, hifadhi ya benki ya sehemu pesa na kufadhili matumizi ya ziada kupitia bondi za hazina zenye kuzalisha riba. Ni mifumo hii ya kudumu ya kibepari ndioyo ambayo huchanganyika na kuwa mafuriko makubwa ambayo huzamisha watu katika mfumko wa bei.
Ni sera ya mapinduzi ya Kiislamu ya sarafu, kama inavyotabikishwa katika Khilafah, ndiyo ambayo itaweza kukomesha mfumko wa bei unaovunja migongo. Khilafah itatoa tu sarafu inayoegemezwa na dhahabu na fedha pekee, hivyo basi kuondoa mfumko wa bei unaosababishwa na uchapishaji wa sarafu isiyo na thamani ya dhati inayozidi mali na bidhaa. Kuondolewa kwa mikopo yenye riba kutaondoa mfumo wa benki wa hifadhi ya sehemu ya pesa, na kulazimisha nidhamu ya fedha katika ukusanyaji wa mapato na matumizi. Kukomeshwa kwa riba pia kutaikomboa Pakistan kutokana na malipo ya riba ambayo sasa ni zaidi ya nusu ya jumla ya kodi inayokusanywa. Na Khilafah itamaliza uhodhi na ulanguzi wa bidhaa kutoka nje. Haya ndiyo mabadiliko pekee ambayo yatakomesha mfumko wa bei unaovunja migongo. Hizb ut Tahrir tayari imetayarisha sera za kina katika suala hili kwa ajili ya utabikishaji. Inawataka watu wa Pakistan waache kuuvumilia mfumo wa kikafiri wa Demokrasia kimya kimya, wasonge mbele kuunga mkono mradi wa Khilafah kwa ajili ya mabadiliko ya kweli.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |