Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  23 Sha'aban 1443 Na: 1443 / 49
M.  Jumamosi, 26 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu ni Faradhi Kubwa, Ambayo Inahitaji Kusimamishwa kwa Khilafah na Kutabikishwa Kikamilifu kwa Shariah.

 (Imetafsiriwa)

Imran Khan alitangaza mkutano mkubwa jijini Islamabad mnamo tarehe 27 Machi, siku moja kabla ya kupiga kura juu ya hoja ya kutokuwa na imani. Mada ya mkutano huo ni "Kuamrisha mema." Imran Khan alisema katika ujumbe wa video kwenye mtandao wa kijamii, "Tunapinga uhalifu unaofanywa dhidi ya demokrasia na taifa, ambapo dhamiri za wawakilishi wa umma zinanunuliwa kwa pesa zilizoporwa" na "Nataka taifa zima lijiunge nami mnamo Machi 27 kutuma ujumbe mmoja - kwamba hatuko pamoja na uovu, tunaupinga." Bila shaka amri ya kuamrisha mema na kukataza maovu ni faradhi kwa kila Muislamu kwa mujibu wa Uislamu. Hata hivyo, haikuamuliwa na mtu yeyote ila na Shariah ya Mwenyezi Mungu (swt). Hizb ut Tahrir/ Wilayah Pakistan inawataka Waislamu wa Pakistan kwamba ni lazima waamrishe mema yote ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameyaamrisha na kukataza maovu yote ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameyakataza, kuwakamata watawala hawa mafisadi.

1. Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha kwamba utawala na hukmu lazima ziwe kwa mujibu wa Qur’an Tukufu na Sunnah za Mtume, ambazo mafaqihi wa kale wanazikadiria kuwa ni faradhi kubwa katika Dini yetu. Katika Qur'an Tukufu, Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

 [وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]

“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Maida 5:45]. Nchini Pakistan, sheria iliyoachwa na mkoloni Raj Muingereza inatekelezwa, ambapo maamuzi, sera na sheria hufanywa, ambayo ni uovu mkuu uliowekwa juu yetu sote na ndio kitovu cha maovu mengine yote. Sote tunawajibika kusimamisha hukmu kwa mujibu wa Wahyi wa Mwenyezi Mungu (swt), kwa kukataa katakata Taghut.

2. Mwenyezi Mungu (swt) imeifanya Jihad kuwa ni faradhi katika Aya nyingi za Qur'an Tukufu na Hadithi katika Sunnah za Mtume. Mwenyezi Mungu amesema, 

 [وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّى لاَ تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلّهِ]

“Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu.” [Surah Al-Baqarah 2: 193]. Waislamu wa Kashmir na Palestina wanasubiri takbira za simba wa jeshi la Pakistan, mingurumo ya vifaru vya Pakistan na mingurumo ya ndege za kivita za Jeshi la Anga la Pakistan. Ni faradhi kwa majeshi ya Pakistan kutumia uwezo wao kwa ajili ya jukumu kubwa la kuwakomboa Waislamu kutokana na vikosi vya uvamizi vya makafiri.

3. Dola ya Pakistan hivi sasa inalipa riba ya bilioni 3,000, ambayo Uislamu umeitangaza kuwa ni kualika vita na Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Huu ni ukafiri uliyo wazi ambao mtawala yeyote Muislamu lazima aiache mara moja. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

 [ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ ٱلرِّبَوٰاْ لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ ٱلَّذِي يَتَخَبَّطُهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ مِنَ ٱلۡمَسِّۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡبَيۡعُ مِثۡلُ ٱلرِّبَوٰاْۗ وَأَحَلَّ ٱللَّهُ ٱلۡبَيۡعَ وَحَرَّمَ ٱلرِّبَوٰاْۚ فَمَن جَآءَهُ مَوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّهِ فَٱنتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمۡرُهُ إِلَى ٱللَّهِ وَمَنۡ عَادَ فَأُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ]

“Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.” [Surah Al-Baqarah 2:275].

4. Mwenyezi Mungu (swt) amewatangaza Waislamu kuwa ni Umma mmoja, ambao ardhi na dola yake ni moja. Ni haramu kuwagawanya Waislamu. Hairuhusiwi kwa Waislamu kuwa na Makhalifa wawili kwa wakati mmoja, iwe kwa ridhaa au kwa kutokubaliana. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إِذَا بُويِعَ لِخَلِيفَتَيْنِ فَاقْتُلُوا الْآخَرَ مِنْهُمَا»

“Pindi ahadi ya utiifu (Bay’ah) inapopewa makhalifa wawili, muuweni wa pili.” [Muslim]. Mipaka yote baina ya Waislamu imeharamishwa waziwazi. Ni wajibu kwa mtawala wa Waislamu kuibomoa mipaka hii na kuwaunganisha ndani ya dola moja. Ni lazima ianze kwa kuziunganisha Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati chini ya Khilafah moja.

5. Uislamu unawaharamisha Waislamu kukubali mamlaka ya makafiri juu yao, huku Uislamu ukiasisi mfumo wake wenyewe wa kimataifa. Hiyo basi, ni wajibu kwa mtawala wa Waislamu kukataa ubwana wa Umoja wa Mataifa, IMF, Mahakama ya Kimataifa ya Haki, FATF na taasisi nyingine za makafiri, huku akiwaunganisha Waislamu wa Eurasia chini ya mamlaka ya dola moja, ambayo ndio mwanzo wa mfumo mpya wa kimataifa. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

 [وَلَن يَجْعَلَ ٱللَّهُ لِلْكَٰفِرِينَ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا]

“Wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surah Al-Nisa 4: 141].

Haya ni baadhi tu ya maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) yanayomfunga mtawala halali wa Waislamu katika suala la kuamrisha mema na kukataza maovu. Utawala katika Uislamu ni mas'uliya na msingi wa malipo makubwa, iwapo mtawala atafanya kwa mujibu wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), vyenginevyo kuna dhambi kubwa kwa mwenye kutawala kinyume na yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hiyo hili ndilo jambo tunalopaswa kulisisitiza na kuwaepuka watawala wa sasa ambao hubadilishana zamu ya kututawala kwa ukafiri, badala yake tujitahidi na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu