Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  10 Jumada II 1442 Na: 1442 / 43
M.  Jumamosi, 23 Januari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Amerika Haikuikalia Afghanistan Pekee ili Kujiondoa kwa Kuitaka tu Ifanye Hivyo!

(Imetafsiriwa)

Katika mahojiano na Al-Jazeera yaliyochapishwa mnamo 21 Januari 2021, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Shah Mahmood Qureshi, alisema kuwa nchi yake inatarajia kushirikiana zaidi na serikali mpya ya Amerika, huku utawala wa Joe Biden ukitoa wito wa kuhakikiwa kwa mchakato wa amani unaoendelea wa Afghanistan, pamoja na uondoaji unaokuja wa majeshi ya Amerika kutoka Afghanistan. Qureshi aliiambia Al-Jazeera, "Nadhani wao [uongozi wa Biden] wanapaswa kutambua kuna fursa nchini Afghanistan na wanapaswa kuvumilia kile kilichoanzishwa na sio kubadili mambo." "Wasukume mbele, kwa sababu, baada ya muda mrefu, tumeanza kusonga mbele katika mwelekeo unaofaa," alihimiza. "Pakistan imefanya mengi, tumepinda nyuma sana ili kuunda mazingira ya kuwezesha mchakato wa amani," alisihi.

Amerika, ambayo ilivamia na kuikalia Afghanistan baada ya matukio ya 9-11, ambayo yalikuwa matukio ambayo ima iliyapanga yenyewe au kuyapatiliza, haikuja kama mvamizi na mkaaji, ili tu ijiondoa au la, kwa ombi tu la Qureshi au mtu mwingine yeyote. Amerika ilikuja kukaa ima kupitia wanajeshi wake au vibaraka wake, ambao iliwaweka dhidi ya watu wa Afghanistan, baada ya kuua, kujeruhi na kuhamisha watu wengi, ambao idadi yao halisi haijulikani hadi leo, kutokana na idadi yao kubwa. Yeyote anayefikiria kuwa Amerika itaondoka Afghanistan kabla ya kupata maslahi yake katika nchi hiyo na eneo hilo, ni limbukeni na hajui chochote juu ya uhalifu, ulafi na uchu wa dola za wakoloni, zikiongozwa na Amerika yenyewe. Kwa hivyo, ukweli ni kwamba Qureshi anatumai tu kushirikiana zaidi na Amerika, kana kwamba Qureshi anajitolea kushirikiana na kutumia uwezo mkubwa wa kijeshi na kijasusi wa Pakistan kwa nia ya kuimarisha ushawishi wa Amerika nchini Afghanistan, huku akilinda maslahi makubwa ya Amerika katika eneo hilo.

Fauka ya hayo, yeyote anayefikiria kuwa mabadiliko ya rais wa Amerika yatakuwa kwa maslahi ya Waislamu kwa njia moja au nyingine, pia ni limbukeni, asiye tafakari juu ya Maneno ya Mwenyezi Mungu (swt),

 [وَالَّذِينَ كَفَرُوا بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ]

“Those who disbelieved each other are only loyal to one another.” [Surah al-Anfaal 8:73]. Haiwezekani kwa mtu mwenye akili timamu kufikiria kwamba rais mpya wa Amerika Biden ni mzuri kwa vyovyote vile. Kwa kweli, kama Makamu wa Rais wa Rais wa zamani wa Amerika Barack Obama, Biden alisisitiza kwa wanajeshi wa Amerika waliobaki Afghanistan na mara kadhaa alikataa kukaa na Taliban kwa mazungumzo, wakati akiwashutumu kama "magaidi." Kwa hivyo, haishangazi kuona kwamba Ikulu ya White House ilitoa taarifa ikithibitisha kwamba Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Joe Biden, Jake Sullivan, amemjulisha mwenzake wa Afghanistan kwamba Amerika itahakiki makubaliano ambayo yalikamilishwa na harakati ya Taliban mnamo Februari2020. Ilikuwa kulingana na makubaliano haya kwamba vikosi vyote vya Amerika vitaondoka Afghanistan ifikapo Aprili 2021. Lakini, Pentagon hivi karibuni ilidokeza kwamba inaweza kuchelewesha uondoaji huu, ikiwa vurugu halitapungua.

Kinachoitwa "amani" ambayo Qureshi anazungumzia na utawala wa Trump ulizungumzia, ilikuwa ni Amerika kutambaa kwa uoga kwa magoti yake hadi kwa washauri wa harakati ya Taliban. Ukweli wa hii "amani" inayodaiwa ni kuiwezesha serikali ya vibaraka katika Ukanda wa Kijani jijini Kabul, ambayo pia itahifadhi maslahi na ushawishi wa Amerika nchini Afghanistan na eneo zima. Kukubaliwa kwa wale ambao wamependezwa na kugawanya madaraka na serikali ya vibaraka ni khiyana na usaliti wa damu ya wale waliouawa mashahidi na mashine ya vita ya Amerika kwa zaidi ya miongo miwili. Ni kukubali kwa vibaraka wa Amerika kutawala nchi tohara kwa ukafiri na utiifu kwa Amerika. Kile walicho fanya watawala wa Pakistan katika kufungua njia ya mchakato wa "amani" ni kutumikia tu maslahi ya mkakati wa Amerika, kwa gharama ya damu hiyo safi, na pia kwa gharama ya watu wa Afghanistan na Pakistan.

Amerika iliyoshindwa na kudhalilishwa kamwe haitaondoka Afghanistan isipokuwa kwa nguvu, kwani ilikuja kwa nguvu na haitaondoka isipokuwa kwa kama iyo hiyo. Hairuhusiwi hata kukubali maridhiano ambayo uondoaji wa vikosi vya Amerika unaambatana na kuikubali serikali ya mamluki ya Afghanistan, kwa msaada wa watawala wa Pakistan. Ni wajibu juu ya shingo za Jeshi la Pakistan kumng'oa Qureshi pamoja na serikali yote ambayo ni kibaraka wa Amerika, na kukabidhi mamlaka kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Wakati huo pekee ndipo Khaleefah Rashid anaweza kuliongoza Jeshi la Pakistan katika kutokomeza uwepo wa Amerika, kwa aina zake zote, kutoka Afghanistan na Pakistan. Ni kwa hili ndilo tunawalingania, Enyi maafisa wenye ikhlasi katika Jeshi la Pakistan.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu