Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  16 Ramadan 1441 Na: 1441/09
M.  Jumamosi, 09 Mei 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari kwa Ajili ya Rai Jumla Nchini Lebanon

Kuhusu Kukiri kwa Ehud Barak, juu ya suala la Uhamishaji wa Wapalestina kutoka Lebanon kama moja ya malengo ya Oparesheni ya 1982 ya Kuvamia Lebanon
(Imetafsiriwa)

Mkuu wa serikali ya Kiyahudi, na waziri wake wa zamani wa jeshi, mhalifu Ehud Barak amekiri kwamba moja ya malengo ya Oparesheni ya 1982 ya kuivamia Lebanon na kubakia kusini mwake hadi mwaka wa 2000, yaani, hata baada ya Yasser Arafat kuondoka Lebanon, ilikuwa ni uwepo wa wakimbizi Palestina nchini Lebanon. Akiongea kwenye redio juu ya ile inayoitwa "Tel Aviv", Barak alisema kuwa serikali yake ilukuwa "inapanga kuwahamisha wakimbizi wa Palestina kutoka Lebanon hadi Jordan, lakini mpango wake ulishindwa kutokana na ugumu wa utekelezaji wake ardhini”.

Pia alitangaza, na yeye ni mmoja wa wahusika wakubwa wa uhalifu na mauaji dhidi ya Wapalestina, kuwa mpango wa Mayahudi ni pamoja na kucheza kwenye safu ya madhehebu, na kuwaandaa Wakristo upande wa kulia ili kumaliza uwepo wa Wapalestina nchini Lebanon.

Tunasema: Kutokana na wa ile taarifa iliyotolewa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon, tarehe tisa ya Ramadhan, sawia na 2/5/2020, kwa anwani "Wapalestina Nchini Lebanon baina ya Kuishi na Shinikizo na Hasara ya Kisiasa," ambayo kwayo walielezea maoni yao juu ya ukweli wa tatizo la Wapalestina nchini Lebanon, taarifa za mhalifu Barak zinakuja kudhibitisha kuoana kwa lengo la Mayahudi, na vitendo vya kibaguzi ambavyo ndugu na dada wa Palestina wanaathirika navyo nchini Lebanon hadi leo, sio ya kwanza ambayo ni kukataa kuwahamisha kutoka katika maeneo ya uwepo wao Lebanon kwa ndege ile ile iliyo warudisha Walebanon hadi Lebanon kutokana na janga la virusi vya Korona.

Hivyo basi, hatusisitizi tu umuhimu wa kuwatendea haki ndugu na dada wa Palestina nchini Lebanon kama watu wengine wa Lebanon, wote kwa usawa, haswa katika haki ya kazi na umilikaji, lakini badala yake zaidi ya familia, haswa wale wanaoendesha gurudumu la utawala nchini Lebanon, mbele ya pazia na nyuma yake, na wale wanao payuka usiku na mchana kuhusu Palestina na upinzani, wanatunga mashairi kuihusu na wala hawayabadilishi kuwa vitendo, bila ya kutaja ukiukaji wa ubaguzi wa rangi dhidi yao wakati wote.

Ndugu na dada wa Palestina nchini Lebanon leo, baada ya miaka sabiini na mbili ya kuwepo nchini Lebanon, ni sehemu ya kitambaa cha kijamii na wachangiaji katika uchumi wa nchi kupitia uingizaji wao wa rasilimali za kigeni na misaada ya Kimataifa.

Fauka ya hayo, uchumi nchini Lebanon unaweza kupona tena ikiwa utaweza kufaidika na taaluma za hali ya juu za Wapalestina nchini Lebanon na kuvutia uwekezaji wa Wapalestina kutoka ng'ambo. Na hili linaweza kufanywa pekee kupitia uondoaji wa vizuizi vyote vya ubaguzi wa rangi, ambavyo vinaambatana na mpango wa kuwaondoa tena Wapalestina nchini Lebanon, ambao umekuwa ukifanywa dhidi yao tangu uvamizi wa 1982 hadi leo ili kuwaweka mbali na Jerusalem na pambizoni mwake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu