Jumapili, 24 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  3 Rabi' I 1445 Na: H.T.L 1445 / 03
M.  Jumatatu, 18 Septemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon Inaendelea na Amali zake za Ziara huko Sidon Kuhusiana na Kambi ya Ain al-Hilweh na Athari za Matukio yake
(Imetafsiriwa)

Tangu kuzuka kwa matukio katika kambi ya Ain al-Hilweh mnamo 29/7/2023, haswa wakati na baada ya raundi ya pili, ya vurugu zaidi, lililozuka usiku wa Alhamisi, 6/9/2023, ambapo ilisababisha uharibifu mkubwa, hasa nje ya kambi ya Ain al-Hilweh, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Lebanon imefanya kila juhudi kuendelea na kazi yake kujaribu kuzima ugomvi na kuzuia mapigano kwa kuwasiliana na wanasiasa na watendaji katika mji wa Sidon na Kambi ya Ain Al-Hilweh.

Katika muktadha huu, ujumbe kutoka kwa hizb ulitembelea mji wa Sidon, na kufanya ziara Mstahiki Mufti wa Sidon na makadhi wake, Sheikh Salim Soussan, Naibu Mkuu wa Afisi ya Kisiasa ya Chama cha Kiislamu nchini Lebanon, Dkt. Bassam Hammoud, na Mheshimiwa Katibu Mkuu wa shirika Maarufu la Nasserite, mbunge Dkt. Osama Saad. Ujumbe huo ulijumuisha Mhandisi Ndugu Bilal Zidane, mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya hizb katika Wilayah ya Lebanon, na Ndugu Haj Hassan Nahas, mjumbe wa Afisi ya Habari ya hizb Wilayah hiyo. Waliandamana kutoka kambi ya Ain al-Hilweh na mwanachama wa Hizb ut Tahrir, Mhandisi Wajdi Shehadeh.

Majadiliano hayo yalilenga kuwasilisha maoni ya kisiasa ya hizb juu ya kile kilichotokea kambini na athari zake kwa watu wa kambi hiyo na kitongoji chake, na kwamba kilichotokea ilikuwa sehemu ya mpango wa Marekani maalum kwa eneo hilo na kupanuka kwake hadi kusini mwa Lebanon, ikihusiana na kuwekwa kwa mipaka ya ardhi, na kabla yake mipaka ya bahari, ambayo itasababisha kupunguza hali ya mzozo na umbile la Kiyahudi hadi kuwa ya chini kulingana na maslahi ya Marekani yake yenyewe nchini Lebanon na viunga vyake. Kuna viashiria vingi vya hili, kama vile harakati za Marekani katika kanda hii kwa miaka, na taarifa ya kushangaza ya msemaji wa Wizara ya Kigeni ya Marekani mnamo 1/8/2023 kuhusu matukio yaliyokuwa kambini wakati wa raundi ya kwanza ya vita, ukimya wa kutiliwa shaka wa Mamlaka ya Lebanon, na ziara ya wakati ya wakati mmoja ya Hochstein na Hossein Amir Abdollahian mnamo 30/7/2023, ambayo ilitilia shaka juu ya muitiko wa polepole wa vyama vyenye ufanisi vya Lebanon.

Ujumbe huo ulithibitisha upingaji wa Hizb wa mauaji, mauaji ya kisiasa, na kulegea kwa vyama vyote, ambayo hairuhusiwi na Sharia, akili, au mafungamano ya damu na udugu. Kisha ujumbe huo ulisema kwamba ulitaka kuunda hali ya jumla ya harakati miongoni mwa watu wa Sidon na amali zake dhidi ya mapigano yaliyotokea, na kuunda shinikizo maarufu kutoka kwa watu wa mji na viunga vyake kujaribu kumaliza ugomvi huo ambao ilikuwa umeathiri kila mtu. Ujumbe huo ulitumaini kwamba harakati hiyo itakuwa nzuri zaidi kuliko wanasiasa wa mji huo na shughuli zake ikiwa matukio kama haya yangetokea tena - Mwenyezi Mungu aepushe mbali - na kwamba kazi ya wanasiasa na shughuli katika mji haipaswi kuonekana kuwa na upendeleo isipokuwa kwa manufaa ya watu, uhai wao, maslahi yao, na uhifadhi wa uhai na usalama wao. Hili linahitaji mawasiliano ya haraka ili kuzuia athari.

Ujumbe huo ulipata majibu ya jumla kutoka kwa pande zote kwa yale uliyowasilisha. Waliwaarifu juu ya baadhi ya harakati walizochukua, na kusisitiza majaribio yao ya kuendelea ili kudhibiti athari zozote, na kuwasiliana na pande zote kufuatilia kila yanayojiri, kuhifadhi usalama wa watu wa Ain al-Hilweh, mji wa Sidon, na eneo viunga vyake. Ujumbe huo ulikabidhi maoni ya kisiasa yaliyotolewa na Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon katika suala hili kwa kila mtu uliyemtembelea.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu