Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
H. 9 Shawwal 1444 | Na: H.T.L 1444 / 10 |
M. Jumamosi, 29 Aprili 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Sote tuko dhidi ya Kampeni ya Kibaguzi na ya Kidhulma dhidi ya Ndugu zetu Watu wa Ash-Sham”
Kisimamo cha Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon kuwatetea Ndugu Zao
(Imetafsiriwa)
Baada ya kuongezeka kwa mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya watu waliokimbia makaazi ya Syria nchini Lebanon, na baada ya Gatuzi la Kaskazini kuchukua maamuzi kadhaa yasiyo ya haki dhidi yao, na uvamizi wa vyombo vya usalama vilivyo nje ya mamlaka yao kwenye kambi za wakimbizi hao, kukamatwa kwa mamia, na kuwakabidhi makumi kadhaa kwa utawala wa Bashar, Hizb ut Tahrir/Wilayah Lebanon iliwaalika watu wa Tripoli Kaskazini mwa Lebanon katika kisimamo wingi mbele ya Saray Tripoli ili kuwanusuru ndugu zao waliokimbia makaazi miongoni mwa watu wa Syria, na kupinga maamuzi ya gatuzi hilo, uvamizi, na kukabidhiwa wakimbizi hao kwa utawala wa Assad.
Kisimamo hiki kilifanyika baada ya swala ya Ijumaa 4/28/2023, ambapo mamia walipoitikia wito huo. Mwanzoni mwa kisimamo hicho, alizungumza mfungwa ambaye ni mwanachama wa Hizb ut Tahrir, aliyeachiliwa huru kutoka katika magereza ya utawala wa Bashar, Ndugu Ahmed Al-Abdullah, na kutokana na yale yaliyosemwa katika kalima yake, "ni kwamba wakimbizi hao ni watu wetu, na wana haki ya kuishi kwa heshima miongoni mwetu, na kukataliwa kwa maamuzi ya kuwadhikisha na kuwawekea mipaka uhuru wao, na kwamba hatutaruhusu kudhoofishwa kwao." Hii ilifuatiwa na kalima ya Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Lebanon, Sheikh Dkt. Muhammad Ibrahim, ambapo aliwaonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kuburuzwa nyuma ya tawala zinazoharakisha kuhalalisha mahusiano na Bashar katika utekelezaji wa amri za Marekani, na kuonya dhidi ya kuendelea kuwanyanyasa watu wa Ash-Sham, na akatangaza kupambamoto dhidi ya maamuzi ya dhulma na ya kibaguzi dhidi ya wakimbizi hao. Na kutowalaumu kwa uhalifu wa baadhi ya wapambe wafisadi wa utawala wa kihalifu, wanaoingiza wao miongoni mwa watu wetu waheshimiwa waliohamishwa. Pia aliwakumbusha wanahabari kuacha kampeni yao ya tashwishi ya kupotosha taswira ya wakimbizi hao, na kuacha kutangaza kuwa wao ndio chanzo cha migogoro nchini Lebanon, huku wakijua fika kuwa chanzo cha mgogoro kinajulikana na kila mtu, kikiwakilishwa na mamlaka fisadi ambayo imepora mamia ya mabilioni ya pesa za umma. Akamalizia kwa kukumbusha kuwa Magharibi na vibaraka wake wanafifia, na kwamba nuru ya Uislamu itang’aa tena, na kwamba siku ni zina zunguka, na ni lazima Mwenyezi Mungu asimamishe haki na kubatilisha batili.
Kisimamo hicho kilihudhuriwa na wafuasi wa Hizb ut Tahrir miongoni mwa watu wa Tripoli, mbali na kundi la vyombo vya habari na wale wanaosimamia mitandao ya mawasiliano ya kielektroniki.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: |