Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  21 Dhu al-Hijjah 1441 Na: H.T.L 1441 / 13
M.  Jumanne, 11 Agosti 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Vilipuzi katika Bandari ya Beirut!
Ni nani Aliyejua kuvihusu Mbali na Utawala Fisidifu?!
(Imetafsiriwa)

Katika habari zilizo chapishwa na gazeti la New York Times katika tovuti yake mnamo 10/08/2020, liliashiria telegram ya kidiplomasia iliyo na alama isiyojulikana, lakini yenye na hisia nzito, iliyotolewa na Ubalozi wa Amerika nchini lebanon siku ya Ijumaa, yaani baada ya mlipuko wa Jumanne, 04/08/2020.

Telegram hii iliyovuja, inazungumzia kwamba mshauri wa kiusalama wa Kiamerika aliyeajiriwa na jeshi la Kiamerika amegundua vifaa vya kemikali wakati wa upekuzi wa usalama, na alionya kwa uchache miaka saba kabla, kuwepo kwa "kiwango kikubwa cha kemikali zenye uwezo wa kulipuka zilizo hifadhiwa katika bandari ya Beirut katika dhurufu zisizo salama. Na kwa mujibu wa telegram hiyo, ("mshauri huyo, chini ya mkataba na jeshi la Amerika, alilishauri jeshi la wanamaji la Lebanon kuanzia 2013 hadi 2016…) na waya huyo ukasema: (Mshauri huyo alinakili kwamba amefanya upekuzi wa taratibu za usalama katika huduma za bandari hiyo, na kuwafikishia maafisa wa bandari wakati wa upekuzi huo kuhusu hifadhi isiyo salama ya ammonium nitrate.)

Bali zaidi ya hayo, telegramu hiyo ya kidiplomasia yenye hisia nzito iliyovuja, inaorodhesha majina ya maafisa wa Lebanon ambao walijua kuhusu ammonium nitrate hiyo.

Telegramu hiyo pia ilieleza kuhusu "Shaka katika maelezo ya awali ya serikali ya Lebanon kuhusu sababu iliyo washa ammonium nitrate hiyo: kwamba moto ulizuka katika bohari lililokuwa karibu lililojaa fataki kisha ukaenea, na kusababisha mlipuko mkubwa sana wa ammonium nitrate ulioharibu sehemu kubwa ya Beirut); badala ya hivyo, "telegramu hiyo inaibua uwezekano kwamba silaha zilizo kuwa zimehifadhiwa huenda zikawa ndizo ziliyo sababisha nguvu ya mlipuko huo wa ammonium nitrate". Na wakati huo huo telegramu hiyo inataja kuwa "sababu ya moto wa kwanza bado ingali haijulikani – kama ilivyo hali kuwa fataki, silaha au kitu chochote chengine kilicho kuwa kimehifadhiwa karibu na ammonium nitrate kilihusika". Maafisa wa sasa na wa zamani wa Amerika wanaofanya kazi Mashariki ya Kati wanasema: inatarajiwa kwa mwanakandarasi kuwasilisha ripoti ya matokeo ya uchunguzi kwa Ubalozi wa Amerika au Pentagon.    

Na pindi gazeti la New York Times lilipowajulisha baadhi ya wanadiplomasia kuhusu yaliyomo ndani ya telegramu hiyo, baadhi ya wanadiplomasia hao walionyesha kushangazwa kwao na hasira zao kwamba ikiwa Amerika ilikuwa na habari, basi haikuzishirikisha kwa mwengine yeyote! Na akasema mwanadiplomasia mmoja wa Kimagharibi – ambaye nyumba yake ilivunjika wakati wa mlipuko huo – aliyezungumza kwa sharti la kutotambulishwa kwake kwa mujibu wa itifaki ya kidiplomasia: "Pindi itakapothibitika hilo, kusema kwa ucheche: itakuwa ni jambo la kushtua mno"

Hivyo basi, sio tu serikali tawala fisidifu inayojua, na wala sio wenye kunufaika tu na vifaa hivi vya kemikali pekee, bali kadhalika pia mabwana zao katika ubalozi wa nchi ya ubalozi huo wanajua, kuwepo kwa makombora yaliyowekwa katika mji huu mkuu, na pamoja na hivyo utawala ukanyamaza kimya, na wakanyamaza kimya wenye kunufaika na vifaa hizi, kwa sababu wao ni duni, wafisadi, walioporomoka, wanawauza bali wanawauwa watu wao wenyewe ili nchi hii ibakie ni shamba la miradi yao michafu; na wamenyamaza pamoja nao mabwana zao, ambao hawakuwajulisha hata jamaa zao wenyewe, kwa sababu huu ni mchezo wa kuidhibiti nchi na watu wake, hata ikiwa thamani ya hilo ni mlipuko wenye kulemaza sehemu kubwa ya mji mkuu huu, na kuwauwa wale waliouwawa, wakiwemo wanadiplomasia wa Kimagharibi wanaoishi katika maeneo yanayotazama mlipuko huo, huku maafisa wa ubalozi na wafanyikazi wake wakiishi katika uwanja wa Awkar, mbali na mlipuko huu.

Habari kama hizi, zilizovuja katika wakati kama huu, ni kwa malengo ya kisiasa yenye tashwishi. Na wala hatuoni kuvujishwa kwake hivi sasa isipokuwa ni kwa ajili ya kuhafifisha shinikizo kutoka kwa serikali za Amerika nchini Lebanon, kana kwamba ulimi wa telegramu hii unasema: Sio utawala na serikali zilizojua pekee, bali sisi pia tulijua, na sisi ni Amerika na huu ni utawala wetu na serikali zetu! Basi nyinyi mnafanya nini enyi wachezaji baada ya mlipuko huu?!

Enyi Watu wa Lebanon: Haya, mnawaona wale wanaodai kuwa walinzi wenu sasa, miongoni mwao Amerika na wengineo, walijua kuhusu jambo la kuweko na vifaa vyenye uwezo mkubwa wa kulipuka, kama ulivyojua utawala fisidifu, wala hakuna yeyote aliye taharaki kitini mwake, hivyo basi nyinyi hamko katika kupaumbele cha usalama, maadamu nchi hii iko mikononi mwao wanaitawala kwa kuikamata juu yake na wanawekeza ndani yake miradi yao. 

Enyi Watu wetu wa Lebanon: Hakika Trump na Macron, na kila anayezunguka mzungunguko wao, miongoni mwa wanasiasa wa Kimagharibi au wa ndani ya nchi wanataka mabadiliko ya kihakika, ya kimsingi nchini Lebanon. Licha ya hotuba zao za ummah kuzungumzia mabadiliko ya kisiasa, hakika wao wanatoa maneno yao katika matokeo ya makongamano yao, Mfaransa anasema: uundaji wa serikali moja ya kizalendo!! Na Mwamerika anasema: uundaji wa serikali isiyo egemea upande wowote!! Hivyo, ni nani atakaye kuwemo ndani ya uundaji huu? Je, ni nyinyi?! Bila shaka hapana, bali yeye ni miongoni mwa tabaka la kisiasa ambalo dhati yake ni fisidifu na wakuu wake ni wafisadi, ambao licha ya kuwajibika kwao kukubwa kwa yale yaliyotokea, Macron alikutana nao wote kwa jumla, na juu ya meza moja, akiwasihi juu ya kufanya kazi pamoja!! Je, hiki sio kidokezi bali tangazo la kubakia kwao na kuhalalisha uwepo wao?!  

Enyi Watu wetu wa Lebanon: Je, wakati haujawadia kwenu wa kukinai na kutambua kwamba tabaka hili fisidifu na angamivu la kisiasa, halina nafasi miongoni mwenu, na kwamba nafasi yake sasa iko mahakamani na magerezani, baada ya kuwang'oa kwa mizizi yao kwa mikoni yenu na mikono ya wenye ikhlasi, na kuwatupa katika bonde lenye kina kirefu?!

Enyi Watu wetu wa Lebanon: Shida na migogoro zimeongezeka, hivyo basi simameni na mufanye kazi ya wale walioyazingatia majanga haya yanayo fuatana, maambukizi, mfumko wa bei kisha mlipuko katika ukubwa wa nchi… La sivyo, basi hamjui litakalokuja baada ya hili kama matokeo ya wanayoyafanya wajinga miongoni mwetu.

 (أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ)

“Je! Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki?” [At-Tawba: 126]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu