Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  27 Dhu al-Hijjah 1440 Na: 1440 H / 043
M.  Jumatano, 28 Agosti 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sera za India ndani ya Kashmir Zinalenga Kuwateka Nyara Watoto Waislamu

Mnamo 15 Agosti 2019, gazeti la UK, The Telegraph liliripoti kuhusu utekaji nyara unaotamausha wa watoto wa Kashmir kufuatia jaribio la India kuliteka eneo ililolivamia la Kashmir. Timu ya Wanachama wa Mashirika ya Kijamii ikijumuisha Jean Dreze na Maimoona Mollah, yameweka orodha ya watoto ambao wanasema kuwa walitiwa korokoroni na kupigwa na Vyombo vya Usalama vya India wakati wa uvamizi wa kigaidi unaoendelea wa Kashmir juu ya Waislamu katika eneo hilo. Jumla ya vyombo vya habari vimenyamazia kimya ili kuruhusu uendelezaji wa uhalifu huo pasina kuripotiwa, lakini kundi la wanaharakati wa haki za binadamu waliweza kuzuru sehemu za Kashmir na kurekodi baadhi ya unyanyasaji walioushuhudia. Hawakuruhusiwa kutumia Vyombo vya Habari vya India ili kufichua maangamivu yaliyotendwa lakini wameweza kupeperusha filamu yao kwa YouTube kwa kichwa cha "Kashmir Caged." ("Wafungwa wa Kashmir") Katika tukio moja maalum,kijana wa kiume wa miaka 11 kutoka Pampore alishikiliwa kituo cha polisi pamoja na mamia ya vijana wenye umri mkubwa na mdogo kuliko yeye. Hapo alipigwa kinyama. Watoto hawa aghalabu huchukuliwa kwa nguvu kutoka vitandani mwao katikati mwa usiku katika uvamizi unaolenga kuwatia hofu wao na familia zao, wakati ambapo wanawake na wasichana nyumbani humo hunajisiwa. Filamu hiyo inaonyesha tukio la kijana mwengine mdogo wakiume ambaye alitekwa nyara baada ya Swala akiwa Msikitini mnamo 5 Agosti. Aliripoti kuwa kulikuwepo na vijana wengine wadogo wakiume 10 au 12 pamoja na yeye. Yote haya ni pamoja na majeruhi mabaya ambayo dola dhalimu ya India imeweza kuwatekelezea watoto Waislamu na vijana wa Kashmir, ikijumuisha kuwatia upofu kwa kutumia risasi za vyuma katika maandamano dhidi ya uvamizi huu wa mauaji.

Dola ya India imepewa ruhusa kuteka nyara na kuwanyanyasa watoto wa Ummah huu kutokana na kukosekana kwa dola ambayo ina uwezo wa kisiasa wa kuyaunganisha majeshi yake ili kuwanusuru na kutia hofu katika moyo wa utawala wa Modi. Watawala wote Waislamu waliopo ni washirika katika kuwatesa na kukiuka haki za watoto wa Kashmir kutokana na kunyamaza kwao, kutochangamka na kufeli kwao kutuma majeshi yao kwenda kuwalinda Waislamu wanaokandamizwa wa Kashmir. Majibu ya aibu na yasiyokuwa na maana ya Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan kwa mfano, amebakia kutamka maneno matupu ya kulaani na kwenda kuomba msaada kwa UN isiyokuwa na uwezo wowote ili kuilazimisha India kurudi nyuma katika hatua zake za hivi majuzi za kivita. Ni UN hii hii ambayo maamuzi yake kuhusiana na ukiukwaji wa haki za Kashmiri ambayo hayakutiliwa maanani na dola ya India na imeyakiuka kwa miongo 7 iliyopita.

Mtume (saw) alisema, «الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ لَا يَظْلِمُهُ وَلَا يُسْلِمُهُ»“Muislamu ni ndugu ya Muislamu: hamkandamizi, wala hamkati.” Lakini chini ya tawala hizi ndani ya ulimwengu wa Waislamu, wamefanya kuwakata Waislamu wanaokandamizwa kuwa ni sera ya dola zao, kuwafunga wanajeshi wao katika kambi ilhali ndugu zao na dada zao wanatoka damu, mama zao na binti zao wanavuniiwa heshima na watoto wao wanatekwa nyara na kuteswa. Tunawauliza, watoto mukhlisina walio na Imani ndani ya majeshi ya Waislamu, mpaka lini mutatoa ahadi ya utiifu kwa watawala waoga, ambao ni chimbuko la ukhaini na wasiowajali Waislamu kwa lolote, na ambao wameipa nguvu mikono ya maadui wa Dini hii na wamewafunga musiweze kutekeleza jukumu lenu kwa Ummah wenu? Mpaka lini mutaendelea kushuhudia ukandamizaji na mauaji ya ndudu zenu na dada zenu ndani ya Kashmir, Palestina, Syria na kwengineko huku mukiwapa migongo licha ya kujua kiwango cha hasira ya Mwenyezi Mungu (swt) juu ya ukosefu wenu wa kuchukua hatua? Mpaka lini mutafunga masikio yenu ili msisikie mayowe ya watoto wa Ummah huu waliotiwa hofu na kufunga macho yenu ili msione machozi ya aibu ya dada zenu waliovunjiwa heshima…ilhali mwajua kwamba munao uwezo wa kuyasitisha yote haya?

Tunawalingana muweze kunyanyuka na kutekeleza jukumu lenu la Kiislamu la kuwalinda Waislamu, kutia hofu katika mioyo ya maadui wa Dini yenu, kukomboa ardhi za Waislamu zilizovamiwa na kutoa Nusrah (nguvu za kijeshi) kwa Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itakuwa ndio mlinzi wa kila Muislamu mwanamume, mwanamke na mtoto. Ni dola ambayo haitokubali kattu kwa wasioamini kuwa juu ya Waumini au kuruhusiwa kutia hofu au kutesa hata mtoto mmoja Muislamu.

Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُواْ فِي سَبِيلِ اللّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الآخِرَةِ إِلاَّ قَلِيلٌ]
“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.” [At-Taubah: 38]

Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir


Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu