Jumamosi, 23 Sha'aban 1446 | 2025/02/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  19 Sha'aban 1446 Na: H 1446 / 090
M.  Jumanne, 18 Februari 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Miaka Miwili Iliyopita Baada ya Tetemeko la Ardhi la Februari 6 Bado Mateso Hayana Mwisho

(Imetafsiriwa)

Mnamo Februari 6, 2023, matetemeko makubwa mawili ya ardhi yenye kipimo cha 7.8 na 7.5, yaliyopiga kusini na katikati mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria, yaliathiri mikoa 11 na kusababisha uharibifu mkubwa na kupoteza maisha. Takriban watu 54,000 nchini Uturuki na 8,500 nchini Syria walipoteza maisha katika matetemeko haya ya ardhi huku kitovu cha matetemeko hayo kikiwa Kahramanmaraş. Jumla ya waliopoteza maisha ilizidi 62,000, na mamilioni ya watu wakabaki bila makao. Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wa huru na rasilimali za ndani zinaonyesha kuwa idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi.

Baada ya matetemeko hayo makubwa ya ardhi, watu walilazimika kuishi katika mahema na nyumba za muda zilizotengenezwa kwa makontena ya chuma yaliyobadilishwa kuwa nyumba za makaazi. Katika kipindi cha miaka miwili iliyofuata, idadi ya watu wanaoishi katika miji ya makontena ilipungua kwa asilimia 7.78 pekee. Kulingana na takwimu za hivi punde zilizochapishwa na Idara ya Mawasiliano ya Afisi ya Rais mnamo Januari 2025, zaidi ya watu 650,000 bado wanaishi katika miji ya makontena.

Wakati huo huo, zaidi ya watu 300 waliripotiwa kutoweka baada ya tetemeko hilo la ardhi. Huku Waziri Ali Yerlikaya akizungumzia watu 75 waliopotea kufikia Novemba 2024, Naibu wa CHP wa Hatay, Nermin Yildirim Kara, anasema wana orodha ya watu 140 waliopotea, wakiwemo watoto 38. Wakati huo huo, familia zinalalamika kuhusu kutojali kwa serikali na wangali wanawasaka watoto wao.

Licha ya kuwa iko kwenye mojawapo ya njia zenye makosa makubwa zaidi duniani, uzembe na kutojali kwa serikali kulidhihirika wazi wakati wa tetemeko hilo, kwani ilishindwa kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya matetemeko ya ardhi, haswa katika miji mikubwa yenye msongamano mkubwa wa watu na ukuaji wa miji usio na mpango. Fauka ya hayo, ukosefu wa mpango madhubuti, mzuri na wa haraka wa utafutaji na uokoaji, pamoja na maandalizi duni ya timu na vifaa, ulifichua kiwango cha kutowajibika huku.

Tetemeko la ardhi la Marmara la 1999 lilifichua jinsi maamuzi ya serikali yalivyopuuzwa na mamlaka, huku taasisi zikifumbia macho na hongo kukithiri katika mashirika rasmi na ukaguzi wa majengo. Kushindwa huku kunatokana na Serikali kutokuwa na uwezo wa kuanzisha mifumo ya udhibiti. Kwa kweli, moto wa hoteli huko Bolu mnamo 21 Januari 2025 pia unachukuliwa kuwa matokeo ya moja kwa moja ya kushindwa huku. Moto wa 21 Januari 2025 katika hoteli ya Bolu ni matokeo ya moja kwa moja ya haya: uzembe, ukosefu wa ukaguzi, na ulafi wa kirasilimali - kuanzia mmiliki wa hoteli, idara ya zima moto iliyotoa ripoti ya moto, manispaa iliyotoa cheti cha usalama wa moto, jimbo na Wizara ya Utalii ambao wote waliidhinisha bila udhibiti - na kugharimu maisha ya watu 78. Walakini, kila mmoja anamtupie mwengine lawama, na hakuna anayechukua jukumu. Hatimaye, uhalifu na sababu zake ni dhahiri. Ni ulafi wa mabepari na watawala wanaowatumikia, wakiamini maisha haya kamwe hayatakwisha na lengo lake pekee ni kujilimbikizia mali.

Uongozi wa Kiislamu, unaotafuta tu radhi za Mwenyezi Mungu na Pepo ya Milele kama lengo pekee la maisha, huhakikisha bila kuchoka usalama wa maisha, mali, na heshima ya watu wake. Hakuna uwekezaji uliomkubwa sana; daima unajitahidi kupata uboreshaji, ukilenga kusimamisha mfumo wa Mwenyezi Mungu wa uadilifu, usalama, na ustawi katika nyanja zote za maisha – daima kwa njia bora zaidi inavyoweza, kwani lengo lake kuu ni radhi za Mwenyezi Mungu (swt). [وَاَحْسِنُواۚ اِنَّ اللّٰهَ يُحِبُّ الْمُحْسِن۪ينَ]  “Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.” [Al-Baqarah 195]

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu