Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  21 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 H / 040
M.  Jumatano, 29 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Inatosha Inatosha, Hali Haivumiliki Tena

Baada ya Mauaji ya Mahema, Ni Kipi chengine Kitausukuma Ummah na Majeshi yake?!
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 27/5/2024, Wizara ya Afya huko Gaza ilitangaza kwamba idadi ya waliouawa kutokana na mauaji yaliyofanywa na vikosi vya uvamizi dhidi ya waliokimbia makaazi yao katika kambi ya mji wa Rafah imeongezeka hadi 45, wakiwemo wanawake 23, watoto na wazee, na waliojeruhiwa kufikia 249. Video zilizosambazwa zilionyesha miili iliyoungua, vichwa vilivyokatwa kutoka kwa miili, majeraha ya moto, na kunyofolewa viungo. Mauaji hayo, ambayo yaliitwa kama “moto wa hema,” yalitokea katika eneo ambalo jeshi la uvamizi lilikuwa limeainisha kama “eneo salama”. Ndege za uvamizi zilishambulia kwa mabomu watu waliokimbia makaazi yao katika kambi mpya iliyoanzishwa karibu na maghala ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kaskazini mwa Rafah Magharibi.

Mauaji mapya ya kutisha yaliyofanywa na umbile la Kiyahudi katika vita vyake vya maangamizi huko Gaza kwa muda wa miezi minane, mbele ya macho ya ulimwengu kwa video na sauti, bila mtu yeyote kuinua kidole! Mauaji mapya ya kikatili, ambayo wengi wa wahasiriwa walikuwa wanawake na watoto, ambao walikuwa “walengwa wa kimkakati” wa mashambulizi ya Mayahudi katika kipindi cha miezi minane iliyopita. Mauaji mapya ya kikatili katika eneo ambalo umbile la Kiyahudi lilitangaza kuwa salama, lakini hakuna mahali salama na hakuna mistari mekundu kwa umbile hili la kihalifu.

Enyi Umma wa Uislamu: Damu na mabaki yaliyoungua ya watoto, wanawake na wazee yatapambana na nyinyi mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) ikiwa hamtasonga kuokoa mabaki ya Rafah na Gaza. Je, Mtume wetu Mtukufu (saw) hakutueleza kuwa: «الْجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالى حالسَّهَرِ وَالْحِمَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحِمَى إِذَا أَشْتَكَا “Kiungo kimojawapo kinapoumia, mwili wote huitikia kwa kukesha na homa”.

Hivi kwa nini munawaacha ndugu zenu watengwe na adui huyu mhalifu?! Je, mutakaa kimya hadi lini kuhusiana na tawala halifu za vibaraka zinazolinda umbile la Kiyahudi na kuzuia harakati zozote dhidi yake?!

Enyi Wenye Ikhlasi katika Majeshi ya Waislamu, hasa tunatoa wito kwa askari wa Misri (Al-Kinanah), ambao mauaji haya yalitokea karibu nao, kwa kusikiwa na kuonekana askari wao wanaolinda mipaka bandia iliyotengenezwa na wakoloni. Mipaka hiyo na migawanyiko inayowazuia kunusuru ndugu zao wanaposikia wito na maombi ya wanawake na watoto ya kuomba msaada asubuhi na jioni. Enyi askari na maafisa: inatosha inatosha, hali haiwezi kuvumilika tena. Ikiwa matukio haya ya kutisha hayakusukumini, basi mutasukumwa lini?! Tunakuonyeni, ikiwa hamuchukui hatua ya kuwanusuru ndugu zenu wa Gaza, basi tahadharini na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake na kukutelekezeni kwake mahali ambapo mutakuwa mukingojea nusra yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «مَا مِنْ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِماً فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتِهُفْمَتِهُ ِفْمَتِهُ فِيهِ فِيهِ حُرْمَتِهُ ِهُ ِنَّعْرِفُوِي ِ، إِلَّا خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ، وَمَا مِنْ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِمْ فَمَا مِنْ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلُمْصِبُّ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ ، إِلَّا نَصَرَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ» “Hakuna (Muislamu) atakayemtelekeza Muislamu mwengine mahali ambapo utukufu wake inakiukwa na heshima yake inavunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza mahali ambapo angetamani nusra yak; na hakuna mtu (Muislamu) ambaye atamnusuru Muislamu mahali ambapo heshima yake inavunjwa na utukufu wake unakiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamnusuru mahali ambapo angetamani nusra wake”.

Basi jiandaeni kwa ajili ya siku ambayo mtasimama mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), na adui yenu ni mtoto kutoka Gaza au mmoja wa wanawake wake huru, wakisema: Ewe Mola Mlezi, watu hawa waliniangusha na ilhali waliweza kuninusuru!

Matukio ya Gaza yameonyesha udhaifu na uoga wa umbile hili, na kwamba lau si kamba (uungaji mkono) wa watu waliopanuliwa kwake kutoka kwa wakuu wa uhalifu, Marekani, Ulaya, na vibaraka wao miongoni mwa watawala, halingeweza kusimama baada ya kukatwa kamba ya Mwenyezi Mungu kutoka kwao. Kwa hiyo, irudieni njia ya washindi wa kwanza na simameni kunusuru kaka na dada zenu wanaokandamizwa huko Gaza na Palestina yote.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu