Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  3 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 010
M.  Alhamisi, 29 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Lau Tungekuwa na Ngao ya Ulinzi na Imam, Mayahudi Wasingesubutu Kunyakua Ardhi Yetu na Kuifisidi
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 9/23/2022, Al Jazeera Kiingereza ilichapisha ripoti kuhusu mateso ya watu wa Masafer Yatta [Palestina] kutokana na mashambulizi ya walowezi. Ripoti hiyo ilinukuu ushahidi wa wanawake wa eneo hilo, waliozungumzia mateso yao na familia zao kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na wanajeshi wavamizi na makundi ya walowezi, ambapo wanapigwa, kupigwa risasi za moto, kushambuliwa kwa gesi na kukamatwa. Ardhi na mali zao huchukuliwa na kuharibiwa, bila kusahau wasiwasi, hofu na ukosefu wa usalama wanaoishi ndani yake.

Eneo la Masafer Yatta liko katika mji wa Yatta, kilomita 12 kusini mashariki mwa Hebron, kwenye eneo la takriban kilomita mraba 32. Wakaazi wake wamekuwa katika hatari ya uhamaji wa kudumu wa makaazi yao kwa kulazimishwa kwa miongo mingi kutokana na kuanzishwa kwa makaazi 10, na "Maeneo ya ufyatuaji risasi (918)" kwa mafunzo ya kijeshi. Jamii zinazotishiwa kuhamishwa kwa lazima ziko kusini mashariki mwa Al-Masafer kwenye eneo la kilomita mraba 32. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), "Hivi sasa huko Masafer Yatta, familia 215 za Wapalestina zinaishi katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na watu wapatao 1,150, ambapo 569 ni watoto."

Wakaazi wa vijiji hivi hutandikwa kwa fimbo na kurushiwa mawe na walowezi, na mifugo yao inatishiwa na kutawanywa na farasi wanaoendeshwa na walowezi au magari ya milimani ambayo hutumiwa kutisha mifugo hiyo, na kuwaachilia mbwa wanaoshambulia wachungaji na kondoo wao. Wakazi hao hukabiliwa na kuchomwa moto mashamba yao na kukatwa miti yao.

Wananchi wa maeneo hayo hasa wanawake na watoto wanaishi katika hali ngumu ya maisha kwani wanaishi kwenye mapango ya chini kwa chini kwa sababu ya kutopata vibali vya ujenzi kiasi kwamba hawawezi kufanya ukarabati wa nyumba zao wala kuzipanua. Tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, wamekuwa wakijenga vijumba vya mabamba na vyumba vidogo juu ya ardhi. Hata hivyo, vyengi yavyo viligeuka kuwa mabaki baada ya vikosi vya uvamizi kuingilia kati na tingatinga kuvibomoa. Aidha, huduma zao za afya, elimu, maji, usafi wa mazingira na umeme ni finyo. Taratibu za kidhulma na sheria za Uvamizi huzuia uanzishwaji wa huduma hata ndogo za afya kwa watoto, wanawake, wazee na wale wanaougua magonjwa sugu, kwani barabara imefungwa na harakati za watu, pamoja na wafanyikazi wa matibabu, ni marufuku. Pia wanazuia uwekaji wa lami na ujenzi wa barabara hiyo, hivyo kuwalazimu kutumia matrekta yao ya kilimo katika kujaribu kusafirisha wagonjwa na kesi za dharura hadi maeneo ya karibu kutokana na ukosefu wa zahanati na vituo vya afya vyenye ujuzi katika eneo hilo.

Umbile la Mayahudi na mkusanyiko wa walowezi wake wana shauku kubwa ya kufanya jinai dhidi ya watu wa Ardhi Iliyobarikiwa na Masraa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Wanawashambulia na kuwahangaisha wanawake katika viwanja vyake na huko Masafer Yatta, na hapo awali, katika kijiji cha Douma, ambapo waliiteketeza familia ya Dawabsheh na jijini Jerusalem ambapo walimteka nyara na kumchoma moto mtoto Muhammad Abu Khdeir; na haya yanaendelea na kuendelea. Sababu ya haya yote ni kuwa umbile hili katili lina kinga kutokana na adhabu, na linategemea ulinzi wa tawala za vibaraka katika nchi za Kiislamu. Na juu yao kwenye orodha ni Mamlaka ya Palestina, ambayo rais wake alikwenda siku chache zilizopita kuomba suluhu kutoka kwa Umoja wa Mataifa, ambayo ndiyo sababu ya maafa ya Ardhi Iliyobarikiwa na watu wake.

Je, uhalifu wote huu hautoshi kuweka udugu na hamasa ndani ya nyoyo za watoto wanyofu wa majeshi katika nchi za Kiislamu kuhamasika, kuikomboa katika njia ya Mtume wao (saw) na kuukomboa Ummah wake kutokana na dhulma inayoukumba?! Je! Bado hawajasikia maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu?

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipo kuwa juu ya watu ambao yapo mapatano baina yenu na wao. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.” [Al-Anfal:72]?! Je wakati haujawadia kwao kujinasua kutokana na minyororo yao na kumtii Muumba badala ya viumbe?!

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu