Hali Ngumu ya Kiuchumi: Matunda ya Mti Mouvu wa Mfumo wa Kiuchumi wa Kibepari Uliong’olewa Ardhini
- Imepeperushwa katika Kenya
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mwaka mmoja baada ya serikali ya Kenya Kwanza kuchukua hatamu za uongozi, hali ya kiuchumi na maisha ya raia wa kawaida imezidi kuwa mbaya. Ni dhahiri shahiri kwamba matarajio makubwa ya wananchi kurahisishiwa gharama za maisha na utawala ulioko mamlakani sambamba na kuondokewa na malimbikizi ya deni la taifa, yamegeuka kuwa mangati/mazigazi.