Jumanne, 07 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  2 Dhu al-Hijjah 1444 Na: 1444 / 23
M.  Jumanne, 20 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hali ya Elimu nchini Jordan ni Msiba na Inahitaji Mabadiliko Msingi ya Uokoaji
(Imetafsiriwa)

Waziri wa Elimu na Waziri wa Elimu ya Juu, Azmi Mahafza, alisema mnamo Jumapili, Juni 18, 2023, "Wataalamu wanakadiria kuwa itachukua zaidi ya miaka 10 kushughulikia na kufidia upungufu wa elimu." Alijadili kuwepo kwa "umaskini wa kielimu" nchini Jordan kabla ya 2019, ambayo inahusu kutokuwa na uwezo wa wanafunzi wa darasa la nne kusoma na kuelewa aya ndogo. Asilimia ya umaskini wa elimu ilikuwa takriban 52.5%. Zaidi ya hayo, zaidi ya nusu ya wanafunzi walikuwa na upungufu mkubwa wa elimu kwa kuzingatia viwango vya kimataifa na tathmini za kimataifa. Uchunguzi umethibitisha kuwepo kwa upungufu mkubwa wa elimu.

Miaka kumi kabla, Waziri wa Elimu wakati huo, Dkt. Mohammad Thneibat, alitoa taarifa mnamo Disemba 22, 2013, kwamba wanafunzi wa madarasa matatu ya kwanza ya shule hawakuweza kusoma herufi za Kiarabu au Kiingereza, ambayo ni karibu 22% ya jumla ya idadi ya wanafunzi, takriban wanafunzi 100,000. Ni waziri huyo huyo ndiye aliyehisi dhiki kubwa kutokana na matokeo ya mitihani ya Tawjihi mwaka 2014, ambapo shule 342 kote katika ufalme hazikuwa na wanafunzi waliofaulu.

Kati ya kauli za waziri huyu na kwamba, muongo mmoja umepita na hali ya elimu imezidi kuzorota, na kufikia hatua ya kuporomoka. Uhalisia wa elimu duni unashuhudiwa na kila familia nchini Jordan, na haihitaji ufafanuzi wowote au uwasilishaji wa ushahidi na nukuu kutoka kwa mawaziri au wale wanaojiita wataalamu wa tawala mtawalia za serikali. Inahusu hali mbaya ya elimu ambayo imeathiri viwango vyote, kuanzia elimu ya msingi hadi ya juu, na imeenea hadi mitaala yake ya kitamaduni na kisayansi, pamoja na mfumo wake wa kiidara unaozidi kuzorota na kubadilika kila mara kwa kila waziri wa elimu, ambao ni wengi na hubadilika kila mwaka wa masomo.

Mifano ya mgogoro wa elimu nchini Jordan na katika nchi zote za Kiislamu inakubaliwa na duara husika, kwani imefikia hali mbaya kwa sasa ambayo haiwezi kuelezewa kikamilifu. Hata hivyo, tunaweza kutaja kile mawaziri wa elimu wamesema kuhusu umaskini na upungufu wa elimu unaohitaji zaidi ya miaka kumi kufidia, na mabadiliko ya mara kwa mara ya mitaala ili kuendana na maagizo ya nchi koloni za Magharibi, huku kukiwa na kuhodhi misaada ya kifedha na mashirika yasiyo ya kiserikali. Hili linalenga kuingiza maadili potovu ya Kimagharibi katika fikra za wanafunzi wetu, kama vile uhuru, haki za watoto, usekula, na demokrasia, kwa maana ya utawala wa watu, ili kuondoa utawala wa Mwenyezi Mungu na Shariah yake. Zaidi ya hayo, juhudi zinafanywa ili kuingiza maadili haya katika mitaala ya juu ya elimy chini ya pazia la falsafa na demokrasia.

Na juu ya sera hii fisidifu na ovu ya elimu, serikali ya Jordan inawalazimishia watu kwa gharama kubwa mno. Imekuwa chanzo cha mfadhaiko na ubora duni. Wanaotafuta elimu na nidhamu, hata katika mazingira ya ufisadi, hukimbilia shule binafsi za gharama kubwa, ambapo waziri wa sasa alidokeza kukosekana kwa ushahidi wa upungufu mkubwa wa elimu katika shule za kibinafsi. Hii ni dalili tosha ya usimamizi mbovu wa serikali wa maslahi ya watu. Ingawa elimu inatakiwa kuwa bure, inawahadaa wanafunzi wake wakati wa likizo za shule, kwani idadi ya siku za shule katika mwaka wa masomo haizidi siku 200, na kusababisha watoto wetu kupoteza sehemu iliyobaki ya mwaka kutoka kwa maisha yao. Badala ya kutekeleza mitaala ya ufundishaji endelevu inayokidhi viwango vya umahiri wa wanafunzi na kutoa fursa ya kumaliza masomo yao katika miaka michache, ingepunguza mzigo wa mapumziko haya kwa wazazi.

Kutokana na uzembe huu katika huduma ya elimu inayotolewa na serikali, elimu imekuwa moja ya njia pana kwa uwekezaji wa serikali na wa kibinafsi, katika ngazi za shule na elimu ya juu. Hii imewezeshwa, haswa kwa shule zenye mwelekeo wa kigeni au vyuo vikuu vya kibinafsi. Kwa hakika, vyuo vikuu vya serikali vimegeuka kuwa taasisi za kibiashara kupitia kile kinachojulikana kama programu sambamba. Kwa mfano, huku wanafunzi 100 wakikubaliwa kusomea udaktari katika chuo kikuu kimoja, zaidi ya wanafunzi 1,500 walikubaliwa katika programu sambamba. Mapato yaliyotokana na programu sambamba yalichangia 40% ya bajeti zilizotarajiwa za vyuo vikuu vya serikali, ambazo zilipaswa kufadhiliwa na serikali kupitia ushuru wa juu unaotozwa kwa watu. Hii ilipelekea baadhi ya dola za Ghuba kugoma kuwapeleka watoto wao kusoma katika vyuo vikuu vya Jordan kutokana na msongamano wa wanafunzi na kushuka kwa ubora wa elimu.

Hali hii duni ya elimu haihimili mabadiliko na kuwaokoa watoto wetu kutokana na kukengeuka  katika mitaala ya elimu na pengo la muda wanalolikubali. Tuna hatari ya kupoteza kizazi kizima ambacho kiwango chao cha elimu, thaqafa, na maarifa kinalingana na nafasi yao katika Umma huu mtukufu wa Kiislamu. Thaqafa ya taifa ndio uti wake wa mgongo, ambapo hadhara yake imejengwa, dhamira na malengo yake yanafafanuliwa, na mfumo wake wa maisha unasifiwa. Thaqafa hii inawakilisha imani yake, ambayo kwayo hukmu, masuluhisho na mifumo huchipuza, na juu yake elimu na sayansi hujengwa.

Mojawapo ya sababu kuu za kutofaulu kwa sera ya elimu ni ukinzani kati ya thaqafa na malengo yanayotarajiwa katika hali ya sasa ya dola ya kitaifa na thaqafa ambayo sera ya kikoloni iliondoa kutoka kwa mtaala wa elimu, ambayo inahusika na shakhsiya ya kweli ya kanuni iliyokumbatiwa na taifa, sio serikali, ambayo ni thaqafa ya Kiislamu. Sera ya elimu katika Dola ya Kiislamu imeegemezwa kwenye Aqida, ambapo nyenzo za masomo na mbinu za kufundishia zinaundwa kwa njia ambayo haikengeuki kutoka kwa msingi huu. Madhumuni ya elimu ni kukuza shakhsiya ya Kiislamu na kuwapa watu elimu na ufahamu kuhusiana na mambo ya maisha. Kwa hiyo, thaqafa ya Kiislamu lazima ifundishwe katika hatua zote za elimu.

Hapo awali tumeangazia katika hafla na taarifa mbalimbali kanuni, malengo, mbinu za kufundishia na muundo wa mtaala wa sera ya elimu katika dola hili. Yote yamepitishwa kwa kuzingatia dalili wazi ya Sharia, na njia sahihi ya kufundisha ni kupitia mazungumzo ya kifikra kutoka kwa mwalimu na mapokezi ya kifikra kutoka kwa mwanafunzi. Fikra au akili ndicho chombo cha elimu na kujifunza, sio mbinu ya kuchosha ya kufunza itikadi au sera inayochochea uigaji na ufuasi. Badala yake, ni sera inayofuata kanuni za uongozi na ubunifu.

Katika historia yake yote, Dola ya Al-Khilafah imetoa umuhimu mkubwa na usaidizi mkubwa katika upatikanaji na usambazaji wa elimu kwa mujibu wa kanuni za Uislamu. Imekuwa kitovu cha elimu duniani, ikivutia ubora wa kitaaluma wa taasisi za elimu na wasomi na wanafikra bora kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Imetoa elimu ya hali ya juu kwa maelfu ya wanafunzi, imeunda enzi inayojulikana kwa uvumbuzi na ugunduzi, na kuasisi hadhara tukufu iliyokuwa nguvu kuu ulimwenguni. Kwa hiyo, ni wajibu wetu kufanya kazi kwa bidii ili kuiregesha Khilafah Rashida, Khilafah yenye msingi wa haki na uadilifu, ili ardhi za Uislamu kwa mara nyingine tena zigeuke kuwa mwenge unaong’aa wa kheri ya elimu, sio kwa ulimwengu wa Kiislamu pekee bali kwa ulimwengu mzima.

[وَاللهُ أَخْرَجَكُم مِّن بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْئاً وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ]

Na Mwenyezi Mungu amekutoeni matumboni mwa mama zenu, hali ya kuwa hamjui kitu, na amekujaalieni masikio na macho na nyoyo ili mpate kushukuru.” [An-Nahl: 78]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu