Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  27 Rajab 1444 Na: 1444 / 13
M.  Jumamosi, 18 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tatizo la Kiuchumi nchini Jordan Kimsingi ni Tatizo la Kisiasa, na halitatatuliwa isipokuwa kupitia Mfumo wa Kiuchumi wa Kiislamu kwa kuregea Dola ya Khilafah
(Imetafsiriwa)

Haikutarajiwa kamwe kwamba Baraza la Wawakilishi, lenye kiwango cha 75% ya waliohudhuria, lingeidhinisha sheria jumla ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023, licha ya ukosoaji mkali wa mswada huo wakati wa vikao vya mijadala ya siku 3 kutokana na nakisi ya kifedha, riba kubwa (riba) ya deni la umma, na kukosekana mipango, miradi na mikakati inayokuza ukuaji wa uchumi. Kwa hiyo, methali hii inawahusu: “Tumewatosheleza kwa matusi, na wakajishindia ngamia!”. Inapingana kabisa na uwakilishi wa kirongo wa wawakilishi wa matarajio ya umma, ambayo ilionyesha kuwa 85% ya watu wa Jordan wanaamini kuwa sera na hatua za kiuchumi za serikali zimeshindwa kupunguza mizigo ya kiuchumi, kudhibiti ongezeko la bei, au kupunguza viwango vya umaskini na ukosefu wa ajira.

Ni jambo la kuvunja moyo, upotofu, na kisingizio kibaya zaidi kuliko dhambi wakati kudorora kwa uchumi wa Jordan kunalinganishwa na sababu za migogoro ya uchumi wa dunia na hali zake za msukosuko, na kisha kudai kwamba Jordan imezishinda dhurufu ngumu, licha ya ukweli kwamba nchi hiyo imezishinda dhurufu ngumu, licha ya hotuba ya jumuiya ya kisiasa ambayo imekuwa katika chumba cha dharura kwa zaidi ya miongo miwili na kuielezea kama "mgogoro usioweza kuepukika." Uhusiano huu ni upuuzi katika vipengele viwili. Cha kwanza ni kwamba kufuata mwelekeo wa uchumi wa kiulimwengu wa kibepari hakuwezi kulinganishwa na kutoa udhuru na kujificha nyuma yake, kwa sababu wenyewe ndiyo msingi wa ufisadi na sababu ya migogoro ya kiuchumi duniani. Cha pili ni kwamba, uchumi wa nchi za kibepari kupitia ukoloni na uporaji wa nchi za dunia ungali uko mbali na kulinganishwa na hali duni ya kiuchumi katika nchi zote za Kiislamu, ambazo sifa zake mashuhuri zaidi ni takwimu zifuatazo zinazohusishwa na athari zake za kisiasa, kiuchumi na kijamii:

1- Jumla ya mapato ya umma kwa mwaka huu yalifikia dinari bilioni 9.569, nyingi zikiwa zimetokana na ada na ushuru, yaani kutoka kwa mifuko ya watu, na jumla ya matumizi ya umma yalifikia dinari bilioni 11.431, hivyo nakisi ya bajeti ilifikia bilioni 1.862. dinari baada ya kukokotoa ruzuku za nje zinazotarajiwa kwa thamani ya dinari milioni 802.

2- Ongezeko la deni la umma nchini Jordan mwishoni mwa mwaka jana, na kufikia dinari bilioni 38.587, au 114% ya pato la taifa. Mapato ya deni la riba yaliongezeka mwaka jana kwa 10%, kufikia dinari bilioni 1.755.

3- Rasimu ya Bajeti ya 2023 ilionyesha kuwa serikali inakusudia kukopa kiasi cha dinari bilioni 8.8, ili kufidia majukumu ya kifedha ya riba, ikiwa ni pamoja na kufidia nakisi ya bajeti inayoongezeka, na kulipa awamu za mikopo ya ndani na nje na bondi za dolari.

4- Ombi kuu la Kamati ya Fedha ya Bunge lilikuwa kuongeza mishahara ya wafanyikazi wa serikali na wanajeshi na wastaafu. Licha ya majadiliano ya wabunge na ukosoaji wa sera ya uchumi ya serikali, hakuna hata mmoja wao aliyetoa suluhisho msingi linalotoka kwa sera ya uchumi mbali na siasa za kibepari, na kutabanniwa kwa programu za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ambao ulipelekea uchumi wa Jordan kwenye shimo kwa zaidi ya miaka 34.

5- Huduma zilizotolewa - kwa mikopo ya riba - kutoka kwa benki ziliongezeka kwa dinari bilioni 2.6 mwaka wa 2022, hadi kufikia dinari bilioni 32.6, na amana za riba za watu wa Jordan kwenye benki ziliongezeka kwa kiasi sawa; Kufikia dinari bilioni 42.1 mnamo 2022.

6- Kuimarisha sera ya kuunganisha dinari na dolari tangu 1995 inayofuatiliwa na Benki Kuu - yaani, bila ya dhamana halisi ya dhahabu na fedha - inayodai kudumisha utulivu wa kiwango cha ubadilishaji ili kudhibiti shinikizo la mfumko wa bei, na kuongeza viwango vya riba, na inafuata Benki ya Kifederali ya Marekani hatua kwa hatua kwa kuichukulia kama mfano, ikidai kuhifadhiwa kwa dinari.

7- Mikopo ya watu wa Jordan kwa benki imefikia dolari bilioni 16, na zaidi ya wakopaji milioni moja, katika mwaka uliopita. Raia wa Jordan wamelazimika kuvumilia maongezeko mingi ya viwango vya riba, na kufanya uwezekano wa kuregesha mikopo kuwa mgumu. Wadaiwa ni takriban asilimia 16 ya wafungwa katika magereza ya Jordan.

8- Makadirio yanaonyesha kuwa kuna zaidi ya watu milioni moja waliokiuka sheria na waliofilisika nchini Jordan, na takwimu rasmi zinasema kwamba wahalifu hawa wanatakiwa kulipa takriban dolari bilioni mbili na nusu kwa njia ya madeni na hundi za benki zilizokataliwa, na idadi ya watu wa Jordan wanaotaka utekelezaji wa idara ya mahakama wa madeni ni takriban watu155,000.

9- Faida ya benki 15, ambazo zilifichua matokeo yao, katika nusu ya kwanza ya 2022 (baada ya ushuru) zilifikia takriban dinari milioni 425.7, ikilinganishwa na dinari milioni 309.1 katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2021, ikimaanisha kuwa ziliongezeka kwa 37.7 %.

10- Bajeti ya dola ya Jordan inategemea zaidi misaada, ruzuku, na mikopo nafuu ili kufidia matumizi yake makuu na kulipa riba kwa deni la umma. Misaada ya Marekani inachukua sehemu kubwa zaidi ya ruzuku inayotolewa na nchi za Magharibi tangu kuanzishwa kwake. Hivi majuzi, Amerika ilifanya upya mkataba wa nne wa maelewano na kuurefusha kwa miaka saba, na kuongeza msaada kutoka dolari bilioni 1.275 hadi dola bilioni 1.450.

11- Taasisi za kimataifa, ikiwemo Benki ya Dunia, zinakadiria kiwango cha umaskini nchini Jordan kuwa zaidi ya 27%, huku ukosefu wa ajira ukizidi 25%, ambayo ni sawa na robo ya watu wote.

Na kutokana na maelezo haya mafupi kuhusu hali mbaya ya kiuchumi nchini Jordan, ambayo ni sawa katika sababu zake na sera mbaya ya kiuchumi katika nchi zote za Kiislamu, iwe tajiri au maskini, ilikuwa ni lazima kutoa maoni haya na uchunguzi wa uhalisia huu. Masuluhisho msingi ambayo, kama yangetekelezwa, Jordan na nchi zote za Kiislamu, ambazo Mwenyezi Mungu alizijaalia utajiri mkubwa, zingetoka katika migogoro yao ya kiuchumi:

1- Matatizo ya kiuchumi nchini Jordan na nchi zote za Kiislamu kimsingi ni matatizo ya kisiasa, yanayohusishwa na utiifu kwa dola za kikoloni ambazo zinapigania ushawishi na utajiri katika nchi zetu zinazoongozwa na Amerika na Uingereza, na kazi wanazozipa serikali zinazotawala ili kufikia maslahi yao ya kikoloni, ikiwemo kulipa utulivu umbile la Kiyahudi kisiasa na kiusalama na kulioanisha kiuchumi na miradi ya kiuchumi ya ndani na kikanda.

2- Sera ya Uchumi ya Jordan ni sera ya kibepari ya utiifu na kujisalimisha kwa maamuzi ya kisiasa ya Magharibi kwa nje kupitia vyombo vyake katika Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na Benki ya Dunia na kuiwezesha kupora kheri na utajiri wa umma, na msingi wake ni ufisadi, ushuru usio wa haki, na wizi wa mifuko ya watu kindani.

3- Uzoefu wa uchumi wa kibepari umefeli katika kitovu chake, na umesababisha migogoro ya kiuchumi duniani. Unatokana na fahamu ya uhuru wa kumiliki mali na mtazamo kwamba tatizo la kiuchumi ni uhaba wa bidhaa na huduma, na kwamba dawa yake ni kuongeza uzalishaji wa bidhaa na kuongeza utoaji wa huduma, na imepelekea udhibiti wa tabaka kubwa la 1% juu ya utajiri, nguvu na ushawishi katika jamii zao na ulimwenguni.

4- Hakuna tiba ya kweli isipokuwa katika Uislamu unaoamini kuwa tatizo la kiuchumi ni kutogawanya mali ipasavyo, kumuwezesha kila mtu makhsusi kunufaika nayo na kuzuia mrundikano wa fedha kwenye mifuko ya kundi fulani, mgawanyiko wa mali, na kitambulisho cha wamiliki wake; Umiliki wa umma wa mali isiyomalizika ni mali ya raia wote wa Dola ya Khilafah.

5- Mfumo wa benki wa riba ndio kiongozi wa janga la uchumi wa kibepari, ambapo benki zina uwezo wa kukusanya pesa za watu kwa jina la amana, na kuziweka kwenye mifuko ya pesa na wamiliki wa biashara, ambayo ilisababisha kuziweka pesa za watu mikononi mwa wachache. Mfumo wa mikopo yenye riba unajumuisha tatizo kubwa la kiuchumi, pamoja na ukweli kwamba Uislamu umeharamisha riba kwa serikali na watu binafsi.

6- Uislamu umeharamisha kulimbikiza pesa, yaani, kuzikusanya bila ya haja, bali zitumike katika miradi ya viwanda, kilimo, au biashara, au maelezo yoyote mengine yaliyoidhinishwa na Sharia ili mali hiyo ibaki kuwa inazunguka, inatembea, hai katika jamii, kunufaika na mapato yake mmiliki na wafanyakazi wake, na masikini na mafukara na wengineo kutokana na aina nane za zakat yake, na jamii kwa jumla inanufaika na miradi yake.

Amesema Mwenyezi Mungu:

(وَٱلَّذِينَ يَكۡنِزُونَ الذَّهَبَ وَالۡفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ)

Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu.” [At-Tawbah 9: 34].

7- Kutofungamanisha sarafu za karatasi na zile zinazobadilishwa na dhahabu na fedha, yaani, kuzitenganisha na hukmu ya dhahabu na fedha, jambo ambalo linagongana na hukmu ya Kiislamu inayohitaji kufanywa dhahabu na fedha kuwa ndio kipimo pekee cha fedha, hivyo Marekani inapora mali ya ulimwengu kwa kuchapisha doari inazohitaji ambazo thamani yake inapungua.

Enyi Waislamu.. Enyi Watu wa Jordan:

Sera ya uchumi katika Uislamu ni kuhakikisha kwamba mahitaji yote ya kimsingi ya kila mtu yanakidhiwa kikamilifu, na kumwezesha kukidhi mahitaji yake ya anasa kadiri awezavyo, kwani anaishi katika jamii maalum ya Kiislamu ambayo ina njia maalum ya kuishi. Uislamu umechukua tahadhari kubwa katika ugawaji wa mali na kubainisha sababu za umiliki na njia za maendeleo na kueleza njia za matumizi, ili kuondoa mrundikano wa fedha mikononi mwa makundi machache ya jamii, na kuharamisha kuficha mali ambayo huzifanya zizunguke sokoni na kumnufaisha kila mtu kutokana nayo, na kuharamisha riba, ambayo inasababisha matatizo makubwa ya kiuchumi, ikiwemo bei za juu. Bei na mfumko wa bei na kuundwa kwa uchumi wa phantom.

Enyi Waislamu:

Amana ambazo watu huweka kwa riba katika benki, ambazo zilizidi dinari bilioni 42, ni kama tangazo la vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Amesema Mwenyezi Mungu:

(فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ)

Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.” [Al-Baqarah 2:279]. Aidha, ni sehemu ya mfumo fisadi wa kibepari unaotengeneza fedha miongoni mwa matajiri badala ya kuzitumia katika miradi inayosukuma gurudumu la uchumi, licha ya vikwazo vinavyowekwa na serikali vinavyovunja moyo uwekezaji kutokana na kodi, ada na faini.

Mfumo wa Uchumi wa Kiislamu hauwezi kuwepo isipokuwa utekelezwe ndani ya Dola ya Khilafah, siku hizi zinaadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa 102 wa kuvunjwa kwake, hivyo kufanya kazi ya kuusimamisha, Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, na ili kuepuka umaskini, njaa na ukosefu wa ajira na tunakualikeni nyinyi Waislamu kutumia mali zenu.

(هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولاً فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ)

Yeye ndiye aliye idhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa.” [Al-Mulk 67:15]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu