Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  26 Safar 1442 Na: 1442/26
M.  Jumanne, 13 Oktoba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Kuogopa Maandamano ya Ummah Serikali Inayotapatapa Inajaribu Kuwanyamazisha Wanafunzi wa Shule
Vitendo Hivi Viovu Kamwe Havitaiokoa Serikali ya Hasina na Nidhamu Yake Tawala ya Kisekula

Idara ya Elimu ya Sekondari na Elimu ya Juu (DSHE) ilitoa maagizo mnamo Alhamisi, tarehe 8 Oktoba, kwa wanafunzi na walimu nchini, ambapo waliamriwa kuacha kupakia, kutoa maoni, ku-like au kusambaza ujumbe wowote, picha, video au sauti kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii ambayo yanachafua taswira ya serikali au dola hii. Waliamriwa pia kuacha kuchapisha maudhui yoyote ya kashfa juu ya watu muhimu serikalini, taasisi au taaluma yoyote kwenye mitandao ya kijamii. Na pia ilionywa kuwa yeyote atakayekiuka hili atachukuliwa hatua za sheria. Hatua hii ya kutapatapa ni sehemu ya msako mkali unaoendelea wa serikali ili kuzima sauti ya Ummah kupitia hofu na vitisho. Ijapokuwa utawala dhalimu wa Hasina umefanikiwa kufunga midomo ya vyombo vya habari, umeshindwa kudhibiti sauti ya watu katika mitandao ya kijamii. Serikali sasa inaogopa kuona kuwa hawawezi kuacha hasa kwa kuibuka kwa nyuso za vijana jasiri kama Abrar Fahad hata baada ya ukamataji wao wa kiholela usokwisha, na utesaji na mauaji yanayofadhiliwa na serikali kwa jumbe za mitandao ya kijamii zilizo dhidi ya udhalimu wa serikali, ufisadi na zinazopingana dhidi ya shughuli za serikali za kutumikia maslahi ya Mabeberu makafiri wa kishirikina. Hili ni dhahiri katika hatua hii ya hivi karibuni ya serikali hii ya kiimla ambayo sasa inawachukulia hata vijana wa shule na vyuo kama wapinzani wake, ambao wameonyesha hasira yao na kutokuwa na uaminifu kwa nidhamu ya sasa ya kisekula na tabaka lake la watawala katika harakati anuwai za kijamii na majukwaa ya mitandao ya kijamii katika "harakati ya usalama barabarani”, "harakati ya kupambana na ubakaji", nk. Inawashtua mno pia mabwana wakoloni wa serikali hii kuwa watu nchini Bangladesh sasa wamezinduka kikamilifu kutokana na nidhamu ya kidemokrasia ya kirasilimali ambayo inazalisha mithili ya utawala wa Awami-BNP, na sasa wanaunga mkono kwa shauku ulinganizi wa nidhamu ya utawala ya Khilafah. Sasa, chaguo pekee lililobakia kwa serikali hii ya vibaraka iliyofilisika ya kukwamia mamlaka ni kuongeza hofu, mateso na vitisho.

Enyi watu, utawala wa Hasina unatetemeka kwa kuona kwamba watu katika kila rika la umri sasa hawalemazwi tena na utawala wao wala nidhamu yenyewe ya kidemokrasia. Pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha dhulma na mazingira ya hofu, serikali hizi vibaraka wa kimagharibi zinaweza tu kusubutu kuchelewesha kurudi kwa suluhisho la pekee la matatizo yenu - Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume - ambayo itarudi hivi karibuni, insh'Allah, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoa bishara hii njema:

 «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” (Imepokewa na Ahmad).

Kwa hivyo, msiogope wala msikate tamaa, na simameni pambizoni mwa chama cha kweli cha Hizb ut Tahrir ambacho kamwe hakiwadanganyi juu ya uokozi wenu wa kweli, na harakisheni juhudi zenu za kuing'oa serikali hii ovu ya kisekula pamoja na watawala wake madhalimu. Haijalishi namna serikali hizi zinavyoonekana kuwa na nguvu na jinsi zinavyotapatapa kwa kuongeza ubabe wao ili kukwamia mamlakani, Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal ameyasifia maumbile yao kuwa ni kama ya nyumba dhaifu zaidi:

(مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنْكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ)

“Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.” [Surah Al-'Ankabut, Ayat 41].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu