Afisi ya Habari
Australia
H. 19 Dhu al-Qi'dah 1445 | Na: 05 / 1445 H |
M. Jumatatu, 27 Mei 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uvamizi wa Kishenzi Unafuata Hatua Tasa za Mfumo wa Kimataifa Pamoja na Hata Mauaji Zaidi ya Kinyama mjini Rafah
(Imetafsiriwa)
Uvamizi wa Kiyahudi unaendelea kuzidisha ukatili wake wa hapo awali, ukifanya uchinjaji na mauaji dhidi ya walio dhaifu zaidi. Wakati huu, waliangusha mabomu yaliyolenga wanawake na watoto waliokimbia makaazi yao katika kambi za Mahema za Rafah. Katika matukio ya kutisha, maiti za watoto wachanga zilizokatwakatwa na wahasiriwa wengine wasio na hatia wanaonekana kubebwa na raia wenzao waliokimbia makaazi yao, wakiwa hawana pa kuwapeleka. Hospitali na miundombinu mingine yote inaendelea kupigwa makombora na kuharibiwa. Kunyimwa maji, chakula, dawa, na nguvu hutumiwa kukidhi hamu ya Wazayuni ya damu na mateso. Silaha za maangamizi makubwa zinarundikwa juu ya wanawake na watoto wasio na ulinzi ambao waliambiwa wahame, ila tu kulengwa katika eneo hasa linalofikiriwa kuwa salama na Wazayuni wa Kiyahudi na wachungaji wao wa kikoloni wa kimataifa. Haya yote yanafuata maelfu ya hatua tasa na maazimio ya ile inayojulikana kama "jumuiya ya kimataifa," isiyo na maana zaidi ya mkao usio na meno unaolenga kuokoa uso kutokana na aibu ya mtoto wao wa msumbufu anayefanya unyama wake wazi, na ambaye wachungaji wake wanaweza tu kutoa maneno ya upole ya kutia adabu.
Je, kuna Muislamu yeyote ambaye bado ana matumaini katika taasisi hizi ambazo zimejenga migogoro inayozikumba ardhi zetu, maarufu zaidi, ingawa sio pekee, nchini Palestina? Je! Kuna Muislamu yeyote aliye na matumaini ya suluhisho lolote kutoka kwa wakoloni hawa waliozivamia ardhi zetu, kuchora mipaka batili baina yetu, kuunda na kutukabidhi bendera mpya zenye vitambulisho vipya ili kutubakisha dhaifu kupurukushwa na yanayoendelea, na kisha kutulazimishia juu yetu watawala wa kiimla waliowatiifu kwa mabwana zao wa kikoloni ili kudumisha udhibiti wao wa kijeshi, kithaqafa, kiuchumi na kisiasa juu ya Ummah?
Mwenyezi Mungu (swt) anasema:
[وَلَا يَزَالُونَ يُقَـٰتِلُونَكُمْ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ ٱسْتَطَـٰعُواۚ]
“Wala hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza.” [Quran 2:217].
Wakoloni wanalenga kuuvuruga Ummah kwa ahadi za uwongo, huku "suluhisho la dola mbili" likiwa ndio maarufu zaidi. Katika jaribio lao la kujionyesha kama wapenda amani, mkoloni Magharibi, ambayo Australia ni sehemu yake, inatoa suluhisho kulingana na malengo yao ya kibeberu baada ya kuunda tatizo. Ushindi wao mkubwa zaidi ungekuwa kuufanya Ummah ukubali uwepo wa Dola ya Kiyahudi. Kwa kufanya hivyo, tungekuwa tuacha hukmu muhimu ya Kiislamu kwa kukabidhi milele ardhi ya Kiislamu kwa mvamizi. Wangefaulu kuufanya Ummah ukubali mifumo iliyotungwa na mwanadamu kuwa na mamlaka juu ya ardhi badala ya Dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Wangeimarisha mgawanyiko ndani ya Ummah kwa namna ya dola za kuchukiza za kitaifa. Wangejiweka kama walinzi wa ulimwengu pamoja na ufisadi wao wa dhahiri. Wangemruhusu mvamizi huyo mhalifu atunukiwe "dola" juu ya ardhi ambayo ilikuwa ya Waislamu na wale waliowakabidhi Waislamu kusimamia mambo yao. Wangefaulu kudumisha "msingi wao wa mbele" na kituo chao cha Magharibi katika moyo wa Ardhi ya Kiislamu, na wangefaulu kuuchelewesha, kwa muda zaidi, Ummah kuchukua nafasi yake ya haki kama mashahidi wa waadilifu juu ya wanadamu.
Mwenyezi Mungu (swt) anasema:
[وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ قَالُوٓا۟ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ]
“Na wanapo ambiwa:Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji.'” [Quran 2:11]. Na,
[وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَـٰكُمْ أُمَّةًۭ وَسَطًۭا لِّتَكُونُوا۟ شُهَدَآءَ عَلَى ٱلنَّاسِ وَيَكُونَ ٱلرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًۭا]
“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu.” [Quran 2:143].
Ishara nyingine zote za uoga zinazotolewa na mithili ya ICC, ICJ, na Umoja wa Mataifa kwa mapana zaidi ziko katika mkondo ule ule: wahalifu wa asili wanaojifanya wapenda amani baada ya kuwezesha awali mauaji ya halaiki. Bali, taasisi zenye nguvu zaidi katika hizi ni zile zinazochochea Mauaji ya Maangamivu ya Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina.
Waislamu lazima wageukie ndani yao kutafuta suluhu, bila kujali ni ngumu kiasi gani kazi iliyo mbele yao. Kwa kuregea kwa Mwenyezi Mungu (swt), tunaweka ahadi ya kulingania tu yale yanayompendeza Yeye (swt). Uvamizi wa Palestina ni kadhia ya Kiislamu inayohitaji ufumbuzi wa Kiislamu. Ni uovu ambao Umma lazima utafute kuubadilisha sambamba na Hadith mashuhuri: «مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ» “Yeyote anayeuona uovu miongoni mwenu na aubadilishe kwa mkono wake. Ikiwa hawezi kufanya hivyo, basi kwa ulimi wake. Ikiwa hawezi kufanya hivyo, basi kwa moyo wake, ambapo hicho ni kiwango dhaifu zaidi cha imani.” (Sahih Muslim) Na mwenyezi Mungu (swt) asema:
[إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ]
“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Quran 13:11].
Kwa hiyo, mabadiliko lazima yachipuze kutokana na Ummah wenyewe, kutafuta mwongozo kutoka kwa Nususi za Kiislamu.
Mtume (saw) amesema: «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye.”
Katika Hadith hii, Mtume (saw) anaunganisha ulinzi wetu wa kimwili na kusimamisha Uimamu (au Khilafah). Watawala wasaliti wa sasa waliolazimishwa juu yetu ni kivuli cha wakoloni. Utiifu wao umethibitishwa mara kwa mara kuwa umekita katika mahakama ya wakoloni. Wamenyakua utashi wa Ummah kwa kuchukua chini ya uongozi wao vipengele vyenye nguvu vya Ummah, hasa majeshi ya kitaalamu na rasilimali zao zote. Kila mtu ana wajibu wa kufanya kile kilicho katika uwezo wake wa Kiislamu ili kukomesha mauaji na uvamizi. Majeshi, hata hivyo, yana jukumu kubwa na la moja kwa moja katika kujibu uchokozi wa kijeshi kwa ulinzi wa kijeshi wa wasio na ulinzi. Wasiposonga, Ummah una jukumu la kuwakumbusha watoto wake katika majeshi wajibu wao. Huu lazima uwe wito mmoja katika kila mkutano wa hadhara, katika kila meza ya chakula cha jioni, katika kila makala inayozungumzia masuluhisho, katika kila Msikiti, katika kila halaqa, na katika kila dua.
Wito kutoka kwa Ummah kwa rasilimali zake za kitaalamu za kijeshi, ambazo unahaki ya kumiliki ipasavyo, utamaanisha kuvitupilia mbali viti vya watawala na kumteua kiongozi muadilifu anayemtumikia Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw) na Umma wa Muhammad (saw). Itamaanisha kuwa na Imam ambaye nyuma yake Umma unapigana na kujilinda.
Ni wakati ambapo huu uwe ndio wito wa sasa katika wakati muhimu katika uwepo wa Ummah. Wito huu unahitaji kubebwa na kukuzwa na wote, kwani si wito wa mtu binafsi au kundi fulani bali ni faradhi ambayo Maulamaa wote wa kitambo wameafikiana. Ni wito ambao hauhitajiki sana na Ummah tu bali unahitajika na wanadamu. Hadhara ya Kiislamu itarudisha akili timamu kwa ulimwengu ambao umeshikwa na wazimu chini ya Ubepari wa Kisekula wa Kiliberali. Watu wa Gaza wametengeneza njia; Ummah unahitaji kuelekeza wito wake kwa yale yanayomridhia Mwenyezi Mungu (swt).
[يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱسْتَجِيبُوا۟ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Quran 8:24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Australia |
Address & Website Tel: |