Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  22 Muharram 1445 Na: 01 / 1445 H
M.  Jumatano, 09 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Domo Tupu la Serikali ya Australia juu ya 'Maeneo ya Wapalestina Yanayokaliwa Kimabavu' Linaficha Uhalifu wake katika Kuwezesha Ukaliaji Kimabavu wa Palestina Yote

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Kifederali la Labor jana iliongeza mazungumzo yake mtupu juu ya Palestina kwa kuthibitisha Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza kama 'maeneo yaliyokaliwa kimabavu', na makaazi yoyote kwenye ardhi hizi kama 'yasiyo uhalali wa kisheria' na hufanya kuwa 'ukiukaji wa sheria za kimataifa'. Iliendelea zaidi na kufuata uitaji wa utawala wa Marekani wa juhudi za hivi karibuni za makaazi kama 'mashambulizi ya kigaidi'.

Hizb ut Tahrir / Australia angependa kuthibitisha tena yafuatayo kuhusu Palestina inayokaliwa kimabavu:

• Ni Magharibi, pamoja na Australia, ndizo zilizowezesha ukaliaji kimabavu wa Palestina, katika sehemu zake zote, kupitia vurugu, uporaji na uhamishaji kwa nguvu wa watu wake.

• Ni Magharibi ndiyo imekuwa ikitafuta kuhalalisha uhalifu huu mkubwa kupitia juhudi nyingi za kimataifa chini ya bendera ya kanuni ya kimataifa, juhudi ambazo Waislamu wanazikataa katakata na ambazo kamwe hawazizingatii.

• Mapambano ya sasa kati ya utawala wa Marekani na wale wanaoongoza ukaliaji huu wa kimabavu ni sura nyingine ya bwana kumuadhibu mtumwa wake, iliyoanzishwa ili kuhakikisha kuwa ukaliaji huo wa kimabavu wanaendelea kufuata maagizo ya Marekani na kimsingi hutumikia maslahi ya Marekani.

• Hakuna kiasi cha kiburi kitakachoficha ukweli unaong’aa zaidi - kwamba Palestina yote ni ardhi inayokaliwa kimabavu, sio tu sehemu zake pekee; kwamba Waislamu hawataacha hata shubiri moja ya ardhi hii; na kwamba Ummah utaendeleza juhudi zake tukufu za kuhakikisha kuwa uvamizi inapinduliwa.

• Waislamu hawasubiri kulaani kutoka kwa dola za Kimagharibi au madai matupu ya mshikamano, kwa kuwa wanaelewa dola za Magharibi ndizo wawezeshaji wa uvamizi huu dhidi ya Uislamu na Waislamu. Badala yake, mambo hayo yanaongeza maumivu kwenye jeraha, kuchukua kadhia ya Palestina kama mpira wa kisiasa tu, na hivyo kuwakasirisha Waislamu mara mbili zaidi - ya kwanza ikiwa ni uvamizi wa kimabavu, ya pili ni kutumia ukosefu wa haki wa ukaliaji kimabavu huu kuosha mikono yao kutokana na udhalilishaji.

• Tunawakumbusha Waislamu jibu pekee la Kiisilamu linalokubalika kwa ukaliaji kimabavu wa ardhi za Kiislamu ni mageuzi kamili ya uvamizi huu. Tunawakumbusha pia Waislamu kwamba kutegemea dola za Magharibi, au kutarajia kheri kutoka kwao, ni usaliti wa msingi wa Kiislamu na kilele cha kushindwa kisiasa ambako hakustahili kwa Ummah wa Muhammad (saw).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu