Jumatano, 29 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  21 Dhu al-Hijjah 1446 Na: H 1446 / 124
M.  Jumanne, 17 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Waislamu: Adui Yenu Anaujua Uzito Wenu Vizuri Kuliko Mnavyoujua nyinyi, na Anakuogopeni Nyinyi na Anakuchukulieni Kwa Umakini Mara Elfu!

(Imetafsiriwa)

Siku baada ya siku, matukio na misimamo inafichua ushahidi mwingi wa dola za kikoloni za kikafiri kuwaogopa Waislamu, ikiwemo umbile vamizi la Kiyahudi. Pia inaonyesha kwamba wanapoamiliana na Waislamu, wanawachukulia kwa uzito mara elfu moja. Baada ya zaidi ya karne moja, baada ya kuvunjwa kwa Khilafah, kugawanyika kwa Waislamu na kuwa maumbo dhaifu, nyenyekevu, ikifuatwa na udanganyifu na uvamizi wa kifikra, kujitenga kwa Waislamu na imani yao, kuporwa mali ya Waislamu, kupanuka kwa ushawishi wa wakoloni hao makafiri katika ardhi zao, na kudhoofika kwao na kudhalilika, baadhi wanasema: Waislamu kamwe hawatainuka tena, na baada ya haya yote, tunasikia na kuona kauli kutoka kwa viongozi wa Magharibi na viongozi wa umbile vamizi la Kiyahudi, ambazo zinaonyesha hofu yao ya Uislamu na hofu iliyojaa nyoyoni mwao kutoka kwa Waislamu katika hali hii.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël anaelezea wasiwasi wake kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, akisema unaleta tishio kwa kile kinachoitwa "Israel" na kwa Ulaya, ingawa Iran, kama nchi nyengine na taasisi katika nchi za Kiislamu, hazitawali kwa Uislamu. Waziri Mkuu wa umbile vamizi la Kiyahudi anasema atafikia malengo ya vita na kuondoa tishio la nyuklia linaloletwa na Iran. Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen, katika ujumbe wake wa Twitter, anathibitisha msimamo wa Ulaya wa kukataa umiliki wa Iran wa silaha za nyuklia. Amerika mara kwa mara hutuma meli zake za kivita na meli za kubeba ndege kwenye eneo hilo,  ya hivi punde ilikuwa ni meli ya kubeba ndege ya Nimitz. Ilituma ndege ishirini na nne za kujaza mafuta katika eneo hilo, ikihofia kwamba hali inaweza kuongezeka huko na kulihakikishia umbile la Kiyahudi, ambalo linategemea Amerika na Magharibi katika vita vyake na Waislamu.

Haya ni pamoja na kauli zao za kuelezea hofu yao ya umoja wa Waislamu, kusimamisha dola ya Khilafah, na hofu yao ya miito ya kukusanya majeshi katika nchi za Waislamu. Wanafahamu hatari kubwa waliyonayo Waislamu kwa nchi za Magharibi na hadhara yake iwapo wataungana ndani ya dola moja. Wanalizingatia hili mara elfu na wanajaribu kwa nguvu zao zote, ujanja na hila, pamoja na vibaraka wao katika nchi za Kiislamu kutoka miongoni mwa watawala na wengineo; wanajaribu kwa haya yote kuzuia kuasisiwa dola ya Khilafah, ambayo imekuwa tumaini la Waislamu na matarajio ambayo macho na nyoyo zao yanatamani, kuanzishwa kwake hivi sasa kumekaribia.

Hakika enyi Waislamu, adui yenu anaogopa kwamba baadhi yenu wanaweza kumiliki silaha zinazoweza kumtishia. Adui yenu anajua uzito wenu wa kweli na siri ya nguvu yenu, ambayo ni katika imani yenu na itikadi yenu. Imani yenu imekufanyeni kuwa umma bora ulio tolewa kwa ajili ya watu. Imani yenu imekufanyeni kuwa mashahidi juu ya wanadamu kwa kuwafikishia ujumbe wa Uislamu. Imani yenu imelazimisha umoja wenu, imefanya vita vyenu kuwa vimoja, na amani yenu kuwa moja. Imani yenu imeunganisha uwepo wenu kwa Mwenyezi Mungu (swt); mnamtegemea Yeye, mnatafuta msaada Wake, na pamoja naye munamshinda adui yenu.

Enyi Waislamu, baadhi yenu watasema: Watawala wenu wanakuzuieni kupigana na kutokana na jihad, na kwamba majeshi katika nchi yenu yamefungwa kwa amri za watawala hao. Hii ina maana kwamba mumepata kujua sababu ya hali muliyomo ndani yake, na munajua sababu ya kushindwa kwenu mikononi mwa kikundi kidogo cha Wayahudi waliolaaniwa, na munajua sababu ya kutawala  kwa nchi za kikoloni za makafiri juu ya nchi yenu. Kwa hivyo, elekezeni mishale yenu kwa watawala hao wajinga (ruwaibidha) wasio na maana, na muunganishe juhudi zenu za kuwaondoa na musimamishe Khalifa mmoja ambaye atakutawaleni kwa mujibu wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunna za Mtume wake (saw). Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, mbebaji wa mradi wa Khilafah, inakuombeni nusra yenu ili kufikia umoja wenu, mumridhishe Mola wenu Mlezi, na akurudishieni heshima na adhama yenu, basi ipeni nusra yenu.

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu