Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 16 Ramadan 1439 | Na: 1439/026 |
M. Ijumaa, 01 Juni 2018 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kurudi kwa Shughuli katika Jukwaa la Al-Okab
(Imetafsiriwa)
Sifa njema ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye kwa neema yake matendo mema hutimia, na sala na amani ziwe juu ya Mbora wa viumbe Muhammad (saw). Kwa zaidi ya muongo mmoja na nusu, Jukwaa la Al-Okab limekuwa kina cha mawazo, kilichojaa majadiliano na uchangamfu kuhusu hali halisi ya Ummah wa Kiislamu na changamoto zinazoukabili. Linatizama mbele kwa upeo wa baadaye na mipango yake, inaleta kazi isiyo na upungufu wa kuanza kwa njia ya maisha ya Kiislamu, linaonyesha mawazo ya Kiislamu, linaharibu na kupinga mawazo ya kisekula na mfano wake. Nasi hapa katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tukiwa wajumbe wa Ummah wa Kiislamu tunawafikishia kuanza tena kwa shughuli za Jukwaa, kuendelea na safari yake pamoja na kituo mwenza cha Jukwaa la Habari la Naqed, pamoja na kurasa za Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir na tovuti nyingine za Hizb, na kurasa za Hizb kwenye mitandao ya kijamii, hususan kutokana na mashambulizi makubwa dhidi ya tovuti na kurasa hizo, ambazo zilikuwa zimelengwa na kampeni za kimataifa kuzifunga na kuzichafua.
Tumeona kuwa mawasiliano na majadiliano kwenye kurasa za mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Twitter yanafutwa ndani ya dakika, na mawazo hupotea kwenye vifungo vya tovuti ambazo zimefanywa upya kila wakati, hivyo, mawazo hayo na matunda ya akili hazifikii isipokuwa wafuasi wachache, hivyo juhudi kubwa na uzalishaji wa mawazo ya ubunifu ni hupotea kwa hasara ya kufungwa. Ilhali, tumegundua kwamba kurasa za jukwaa huhifadhi matunda hayo kwa miongo kadhaa, ambayo humfikia msomaji na mfuasi kwa namna ya hali na mpangilio msafi unaostahiki kuwa matunda ya akili.
Tuligundua pia kuwa mawazo yanahitajika kupanuliwa, hayawezi kufikiwa kwa kasi ya mitandao ya kijamii, kwa hiyo Jukwaa lilistahili zaidi kuwepo na ili kuhifadhi mawazo haya. Ummah ambao uko makini na umefahamu njia yake ya kurudisha hadhi kama bwana wa mataifa na bora wa Ummah uliowahi kuletwa kwa ajili ya mwanadamu unahitaji umakinifu, midahalo, upangiliaji, ushaurianaji na kuzungumza. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu ayajaalie majukwaa na tovuti zetu ziweze kuboresha shughuli za wasomi wetu, mashababu wetu na Ummah wetu katika kazi ya kutekeleza jukumu la kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha serikali ya Khilafah ya pili kwa kutumia njia ya Utume, dola ambayo ndani yake Mwenyezi Mungu atawasimamishia Waislamu dini yao ambayo amewaridhia.
Usajili kwa ajili ya jukwaa uko wazi, na Mwenyezi Mungu aufanye mchango wako katika jukwaa uwe ni wenye kheri, na tufanye kazi yetu iwe ni kwa Ajili yake tu, na atusaidia na kutupa ufanisi tufanye kile anachokipenda na kinachompendeza Yeye. Sifa ni kwa Mwenyezi Mungu Mola wa Ulimwengu.
Mtandao wa jukwaa hili: https://www.alokab.com
Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi ya Kuu ya Habari ya
Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |