Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  7 Sha'aban 1439 Na: 1439/022
M.  Jumatatu, 23 Aprili 2018

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waziri wa Wakf wa Misri Atetea Sanamu la “Uzalendo”
(Imetafsiriwa)

Waziri wa Wakf wa Misri, Dkt. Mohamed Mokhtar Gomaa, alishindwa kuzuia hasira zake katika taasisi ya elimu, Chuo Kikuu cha Zagazig, wakati wa mjadala wa utafiti wa kufuzu kwa shahada ya uzamili uliowasilishwa na mwanafunzi Waidi Abdul Qadir kwa anwani “Kuhuisha Fikra ya Dini katika Uislamu… Mfano wa Muhammad Iqbal”. Waziri huyu alifoka kwa mori na kutoa vitisho huku akikurupuka kutoka kitini mwake kuelekea jukwaani, huku akitamka kwa kelele maneno yaliyotajwa katika utafiti huo ambayo aliyakadiria kukiuka “dhati ya uzalendo”, ikiwemo: “Sanamu jipya lenye hatari zaidi ni “uzalendo”, kuivisha Dini kwalo ni kama kuivisha sanda kwalo.” Ghadhabu za waziri huyu zilimfanya kumwita mwanafunzi huyu, aliyefanya bidii katika kutayarisha utafiti wake chini ya usimamizi wa Dkt. Sabir Abdel Dayem, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha Lugha ya Kiarabu, kama “mpumbavu”, “mjinga” na “punda”. Waziri huyu alisema: “Utafiti huu wa shahada ya uzamili umeamsha hasira zangu kwa sababu unajumuisha paragrafu ambazo zinabeba fikra zenye kuhatarisha nchi. Umenisababishia uchungu mkubwa na huzuni, kwani ulinzi wa nchi umezama ndani ya nyoyo zetu na akilini mwetu”.  

Waziri huyu anatetea kwa kujitolea ili kulinda sanamu la “uzalendo”. Inajulikana na kila mmoja mwenye elimu ya chini kabisa ya Uislamu na hukmu zake, kuwa fahamu ya “uzalendo” ni ngeni katika Dini na Waislamu hivyo haina mfano wala msingi katika nususi za kisheria, si katika Kitabu cha Allah wala katika Sunnah za Mtume. Wa kwanza kuileta fahamu ya uzalendo alikuwa ni Sheikh Al-Azhar Rafa’a Rafi al-Tahtawi, aliyetumwa na Muhammad Ali Pasha (mnamo 1826) ili awe kiigizo cha kidini kwa wanafunzi wanaosoma sayansi muhimu nchini Ufaransa, badala yake alirudi kutoka Ufaransa huku akiwa amebeba viini vya hadhara ya kisekula ya kimagharibi, na fahamu na fikra zake chafu ambazo hazikujengwa juu ya mijadala na dalili.  Moja ya fahamu hizi ni fahamu ya “Uzalendo”, inayowalazimisha watu kujifunga na maeneo, na kuchukuliwa kama “masanamu” ikiwafanya wanasiasa kuhalalisha vita na umwagaji damu “kwa ajili ya nchi”. Si ajabu kuwa katika karne ya kumi na tisa ilishuhudia mwanzo wa wimbi la ukoloni wa Kimagharibi uliozichoma nchi dhaifu ulizoziingia; Wazungu walionja matunda ya sanamu la “Uzalendo” walipopigana vita baina yao ambavyo havikumalizika mpaka mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia!   

Fahamu ya “Uzalendo” inahusishwa moja kwa moja na fahamu ya ubwana wa kitaifa na ubwana wa sheria zilizotungwa na mwanadamu; sheria hii, inayofafanua haki na majukumu kwa mujibu wa matamanio ya watunzi wa sheria mabungeni: kwa hivyo mhalifu ambaye anapaswa kuadhibiwa kwa “Hudud” katika eneo moja, hukumu yake yaweza kubatilishwa katika mipaka ya eneo jengine, yote ikiwa ni kwa mujibu wa matamanio na hawaa za watunzi wa sheria katika mipaka ya sehemu zote hizi mbili! Ingawa Ulaya imedai, na inaendelea kudai, kuwa kinara wa ubebaji hadhara yenye ukombozi wa watu, inakereka pindi isikiapo kuhusu kuwasili kwa wale wanaokimbia mateso ya sera zake za kibepari, na kwa hivyo inafunga mipaka yake kuwazuia “makatili” hawa, ingawa mfumo wao wa “ubinadamu”, kama kweli una ubinadamu, ungewapokea wale wanaotafuta usaidizi wake, weka kando wahanga wa ukatili wa sera za kikoloni. Hakika hili ndilo Uislamu inalotafuta wakati unapoamiliana na mataifa mengine: Waislamu walijitolea muhanga damu zao ili kuwawezesha wengine kupata ujumbe wa haki wa Uislamu, ambao haubagui baina ya mtu na mtu mwengine isipokuwa kwa msingi wa uchaMungu.   

Ama kuhusu Waziri huyu wa Wakf, alipaswa kukasirika zaidi na kuchafuliwa kwa utukufu wa Allah na kuondolewa kwa sheria yake na kufanya urafiki na maadui zake, Mayahudi na Waamerika. Au kughadhabika kwa sababu ya kuchafuliwa kwa eneo tukufu la Aqsa na Mayahudi, au kwa sababu ya kumwagwa damu ya Waislamu katika ardhi ya Ash-Sham. Tunamnasihi kukumbuka msimamo wa kiimani wa wachawi wa Firauni, waliochagua radhi za Allah licha ya vitisho vya Firauni, na kuchagua maisha ya Akhera juu ya maisha haya potevu, na wakatangaza haki mbele ya katili Firauni pasi na kusitasita. Tunamwambia Dkt. Gomaa kwamba sanamu la “Uzalendo”, linalotukuzwa na sheria ya makafiri wa Kimagharibi, Uislamu unasema ni lazima liangamizwe, kama vile unavyohitaji kuabudiwa kwa Allah pekee katika Rububiya yake na Uluhiya yake. Na ujumbe wa Uislamu na rehma zake na uadilifu wake uweze kutawala watu wote bila ya ubaguzi, ulifanya hivyo mwanzoni na utafanya tena hivyo, mpaka siku ya Kiyama, na Sharia ya Allah ndio ya haki pekee na sheria zote za kibinadamu ni batili. Ni bora kwako kutafuta radhi za Allah na wala sio kuliridhisha Shirika la Rand au wakoloni wa Kimagharibi, ikiwa hutafanya hivyo, basi twakuonya kwa maneno ya Allah:    

وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ﴿

“Na wasomee (Ewe Muhammad) habari za yule tuliyempa aya zetu, lakini akajitenga nazo; akamfuata shetani, na akawa miongoni mwa wapotevu.” [Al-A’raf: 175]  

 Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu