Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
H. 3 Dhu al-Qi'dah 1445 | Na: Afg. 1445 H / 23 |
M. Jumamosi, 11 Mei 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rambirambi na Ujumbe wa Pole wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan Kuhusiana na Mafuriko ya Hivi Karibuni katika Mikoa Mbalimbali!
(Imetafsiriwa)
Kutokana na mvua za msimu na mafuriko katika mikoa ya Kati na Kaskazini mwa Afghanistan, zaidi ya watu mia tatu wamepoteza maisha huku makumi ya wengine wakitoweka. Idadi kubwa ya nyumba na mashamba ya kilimo pia imeharibiwa.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Afghanistan inatoa pole na rambirambi za dhati kwa wahanga wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mikoa mbalimbali ya Afghanistan na inamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awahesabu watu hao waliopoteza maisha kama mashahidi na awape afueni kamili waliojeruhiwa. Tunaomba walio athiriwa wapate subira.
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (ra) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«الشُّهَدَاءُ خَمْسَةٌ؛ الْمَطْعُونُ، وَالْمَبْطُونُ، وَالْغَرِيقُ، وَصَاحِبُ الْهَدْمِ، وَالشَّهِيدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ»
“Mashahidi ni aina tano: aliyekufa kwa ugonjwa wa tauni; aliyekufa kwa ugonjwa wat umbo; aliyekufa kwa kuzama maji, aliyekufa chini ya kifusi, na aliyekufa katika vita kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.”
Maisha haya bila shaka yamejawa na Ibtila' (mateso na balaa), na kila balaa inayowajia watu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ina Hikmah yake na muumini lazima awe na subira (Sabr), imani na kumtegemea (Tawakul) Mwenyezi Mungu (swt) wakati wa misiba na wajifunze mafunzo muhimu kutokana na matukio haya.
Zaidi ya hayo, ni faradhi kwa mtawala (anayewajibika kwa Waislamu) kuchukua hatua zinazofaa na kuzingatia kwa hekima mambo yao. Ni jukumu kubwa la mtawala kuwa na mkakati na mpango uliopangwa tayari unaolenga kulinda maisha na mali za watu dhidi ya maafa ya asili kabla ya maafa yoyote kutokea, na kufanya juhudi muhimu na kamili za kuwafikia wahanga wa maafa baadaye. Bila shaka, moja ya sababu za “majanga ya kimaumbile” kama hayo ni kutabikishwa kwa mfumo wa kibepari na ukosefu wa ubwana wa Dini (mfumo) ya Mwenyezi Mungu (swt) duniani - matokeo yake mazingira yameharibika, na kusababisha mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la joto duniani. Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, Afghanistan ina hisa ya 0.08% katika uzalishaji wa gesi chafu duniani, lakini ni nchi ya sita ambayo iko katika hatari kubwa ya mabadiliko ya tabianachi - na kuongeza matatizo ya maji na majanga ya mazingira nchini Afghanistan. Kwa bahati mbaya, kutokana na ukosefu wa umakini wa watawala na ukosefu wa miundombinu msingi, matukio ya aina hii hutokea kila mwaka; na mvua ambayo ni neema ya Mwenyezi Mungu (swt) hugeuka kuwa njia ya kuangamiza maisha ya watu, mali, nyumba, wanyama na mashamba. «الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Hakika Imam (mtawala) ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake.”
Sasa kwa vile tukio hili limewakumba watu wa Afghanistan, tunatumai kwamba Waislamu wote katika ngazi zote watashikana mikono na kukimbilia kuwasaidia waathiriwa wa ajali hiyo.
[الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُواْ إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ * أُولَـئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُولَـئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ]
“Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.” [Surah Al-Baqarah:156-7]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Afghanistan |
Address & Website Tel: http://hizb-afghanistan.org/ |
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org |