Jumanne, 17 Sha'aban 1445 | 2024/02/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Taarifa ya Tanzia
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Syria Inaomboleza Mmoja wa Wanachama Wake
Hussain Othman Jummu’ah Abu Othman
(Imetafsiriwa)

Twamuomba Mwenyezi Mungu amfinike kwa Rehema zake na amjaalie Firdaus ya juu kabisa Peponi.

Marehemu ndugu, Mwenyezi Mungu amrehemu, Mwenyezi Mungu akipenda, alitumia miongo kadhaa ya maisha yake kubeba dawah ya Khilafah ndani ya safu za Hizb ut Tahrir, bila kulegea katika kujitolea kwake wala kuyumba katika azma yake.

Aliingia kwenye magereza ya dhalimu wa Ash-Sham, baba, katika mwaka wa 2000 M, na akatoka mwaka mmoja baadaye kuendelea kubeba dawah katika miaka hiyo migumu. Alibeba ulinganizi huu na akakamatwa tena wakati wa dhalimu, mwana, mwaka wa 2004, kwa karibu miaka saba, aliendelea kubeba ulinganizi baada ya kuachiliwa tena. Aliendelea kuwa na msimamo na kujitoa muhanga mpaka alipokwenda kwa Mola wake mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 10 Jumada al-Akhirah 1445 H, sawia na 23/12/2023 M.

Macho yamejaa machozi na moyo unanyenyekea. Tumehuzunishwa na kuondoka kwako, ewe Abu Uthman, na tunasema tu yanayomridhisha Mwenyezi Mungu:

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 156]. 

H. 10 Jumada II 1445
M. : Jumamosi, 23 Disemba 2023

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Syria

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu