Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wito wa Ardhi Iliobarikiwa kwa Wanazuoni wa Ummah wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)

Tunamsifu Mwenyezi Mungu ambaye alijitambulisha kwenu, kwa hivyo mkajua Upweke na upekee wake katika kuamrisha, kukataza, na Tadbir (kupanga). Amekukabidhini amana kwa wahyi na dini yake, kwa hivyo mkawa warithi wa manabii, kwa hivyo mlipaswa kuwa watu wenye kumcha zaidi Mwenyezi Mungu, mkizungumza ukweli na kutoogopa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lawama ya mwenye kulaumu.

Tunashuhudia kwamba hapana Mola anayestahiki kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu peke yake, asiye na mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wake na Mtume wake, ushuhuda ambao kwao tunaahidi utiifu kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake, na waumini, na ambao kwao tunakanusha ukafiri, makafiri, unafiki, wanafiki, usaliti, na wasaliti, na rehma na amani ziwe juu ya uthibitisho wa Mwenyezi Mungu juu ya walimwengu, zaidi ya hayo ...

Tunakuhutubieni kutoka Ardhi Iliyobarikiwa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na hasira kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu inalipuka kutoka pande zetu. Pengine huenda tukapata ndani yenu mwanachuoni mwenye uroho, Izz al-Din Ibn 'Abd al-Salam ambaye aliiamsha Misri na majeshi yake kwa Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na akawashinda Matatari huko Ain Jalut.

Nini kimetokea kwa dini yenu ?!

Ikiwa hamtaenda kuhamasisha Ummah wa Kiislamu na majeshi yake kutangaza Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi je dori yenu na kazi yenu ni nini?!

Umati wa Ummah wa Kiislamu uko kwenye viwanja, ili kusonga kuzipindua serikali za vibaraka na kuunganisha vikosi vya vita na jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Enyi Wanazuoni wa al-Azhar:

Mwenyezi Mungu aliwakirimu wanajeshi wa Misri, na ilikuwa kupitia mikono yao ukombozi wa Bayt al-Maqdis kutoka kwa chukizo la Makruseda, na Mwenyezi Mungu akawakirimu tena wanajeshi wa Misri, na ilikuwa ni ushindi wa wazi juu ya Matatari. Tunaomba kwamba Mwenyezi Mungu Mwenyezi awakirimu wanajeshi wa Misri kwa mara nyingine tena, ili kuandamana kwao hadi Ardhi Iliyobarikiwa iwe ni mlango wa ushindi, izza, na tamkini kwa Uislamu na Waislamu, na kuwang’oa wale ambao wamechochea hasira [Yenu] kutoka katika Ardhi Takatifu. Kwa hivyo, lihamasisheni Jeshi la Misri kupigana Jihad kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hii ndio njia ya waongofu.

Enyi Wanazuoni wa Kiislamu kutoka Mashariki na Magharibi mwa Dunia:

Watawala wa Waislamu wanategemea Marekani na Magharibi, na hatutarajii chochote cha kheri kutoka kwao. Ni walinzi waaminifu wa umbile la Kiyahudi na watetezi wa maslahi ya Marekani. Na kutokana na udhalilifu na uduni wao wangali wanangojea ruhusa kutoka kwa Marekani na umbile la Kiyahudi kutoa misaada ambayo Waislamu waliitoa kwa ajili ya ndugu zao huko Gaza. Je! Mtu ambaye hawezi kutoa kipande cha mkate bila ya ruhusa kutoka kwa maadui wa Ummah anaweza kutuletea fahari au hadhi yoyote?!

Ummah wa Kiislamu leo unahitaji kalima kutoka kwenu ambayo itaendelea, na kuimarisha uamuzi wake, kalima ambayo kwayo maneno haya ya Mwenyezi Mungu yanadhihiri:

[الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَاناً وَقَالُوا ‌حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ]

“Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa.” [Aali’Imran 3:173]. Kalima ambayo kwayo kauli hii ya Mwenyezi Mungu Mtukufu inadhihiri:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ‌انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache * Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawbah 9:38-39].

Enyi Wanazuoni wenye Uroho:

Nyinyi ndio watu wajuzi zaidi kuhusu hukmu ya Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ili kuikomboa Bayt al-Maqdis na kunusuru Uislamu na Waislamu. Hivi kwa nini hamzungumzi?! Je! Munawaogopa watawala vibaraka?!

[فَاللهُ ‌أَحَقُّ أَنْ تَخْشَوْهُ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ] “Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.” [At-Tawbah 9:13].

Mnajua fika kuwa watawala hawa vibaraka wanatutawala kwa yasiyokuwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na wanaufanya Ummah wa Kiislamu kuteseka aina tofauti za udhalilifu kwa kuitikia wito wa maadui wa Uislamu, na wanaufunga minyororo Ummah na majeshi yake na kuunda mgawanyiko kati yao kwa mipaka bandia iliyochorwa na wakoloni makafiri. Kwa hivyo mtafanya nini? Tujibuni, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mtafanya nini?

Je! Hamjui kuwa taarifa za watawala vibaraka na ombi lao la kutekelezwa suluhisho la dola mbili au kutekelezwa uhalali wa kimataifa ni khiyana kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake, na waumini na kuasisiwa kwa umbile la Kiyahudi kwenye Ardhi Iliyobarikiwa?! Kwa hivyo, kemeeni khiyana yao.

Watu wa Gaza hawasubiri dawa au chakula kutoka kwa Ummah wa Kiislamu. Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa hawataki suluhisho la dola mbili na utekelezwaji wa uhalali wa kimataifa, lakini badala yake wanasubiri kwa hamu majeshi ya Waislamu kuandamana kwenda Msikiti wa Al-Aqsa na kusikia kishindo cha ndege zikilivunja vunja umbile la Kiyahudi kabisa, bila kuacha hata jiwe moja juu ya jengine kusalia ndani yake.

Wanazuoni wapendwa:

Damu yetu inayomwagwa, na watoto na wanawake wetu waliokosa makao, ni uthibitisho wetu mbele ya Mwenyezi Mungu dhidi yenu, kwa hivyo tayarisheni uthibitisho wenu kwa ajili ya kukutana na Mwenyezi Mungu ...

Tunakulinganieni mufanye kile ambacho Mwenyezi Mungu amekulazimisheni juu yenu; kwamba unatafuta nusra kutoka kwa Ummah wa Kiislamu na majeshi yake ili kusimamisha Khilafah Rashida na muikomboe Bayt al-Maqdis. Endapo  mutauamsha Ummah wa Kiislamu kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu ardhini, kuondoa mipaka, na kutangaza Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, mutapata ushindi mkubwa pamoja na ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume wake (saw). Hili ndilo linalostahiki kwa wanazuoni wenye uroho. Yeyote kati yenu ambaye ni muoga na anapendelea usalama katika ulimwengu huu, basi kile kinachomngojea ni hasira isiyo na kifani ya Mwenyezi Mungu na hatamdhuru Mwenyezi Mungu hata kidogo.

Kwa kumalizia: tegemeo letu kwa Mwenyezi Mungu ni kubwa. Yeye pekee atatupa Nusrah na msaada kutoka kwake, na tunahakikishiwa ushindi wa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mwenye uwezo, kwa sababu ushindi uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu peke yake, naye ataupeana mikononi mwa waja wake ambao yeye amewachagua kwa heshima hii. Kwa hivyo, mtu yeyote anayetaka kuwa miongoni mwao ameshinda ushindi mkubwa, na mtu yeyote anayemilikiwa na uoga atasikitishwa na kupata hasara hapa ulimwenguni na kesho Akhera. Maadui zetu, haijalishi wana nguvu kiasi gani, ni nguvu yenye kikomo, na kwa hivyo hatuwaoni ni chochote kwa sababu tunaamini na kutegemea nguvu isiyo na kikomo, ambayo ni nguvu ya Mwenyezi Mungu Mwenye uwezo, Mwenye nguvu. Acha Marekani ilete manuari zake za kubebea ndege, kwa kuwa hazitalifaidisha chochote umbile la Kiyahudi ikiwa ahadi ya Mwenyezi Mungu itatimia.

[فَإِذَا جَاءَ ‌وَعْدُ ‌الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيراً]

“Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.” [Al-Isra 17:7]. Hili ndilo ambalo Mwenyezi Mungu na Mtuwe wake wametuahidi, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema Kweli, Mwenyezi Mungu ndiye anayetutosheleza na ndiye mbora wa wenye kutegemewa.

Ewe Mwenyezi Mungu, tumeshawaarifu yale Unayoyapenda. Ewe Mwenyezi Mungu, tuarifu kwa yale tunayoyapenda ya ushindi na tamkini. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Mola wa walimwengu.

H. 3 Rabi' II 1445
M. : Jumatano, 18 Oktoba 2023

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu