Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urasilimali Umetulazimisha Kuchagua Ima Ugonjwa wa Virusi vya Korona au Njaa kupitia Amri ya Kutotoka Nje, ilhali Watawala Waislamu Wanaendelea na Utabikishaji Wake, Badala ya Kutawala kwa Uislamu.

Hata pamoja na kuruhusiwa kwa baadhi ya viwanda, kuzuiliwa kabisa kutotoka nje nchini Pakistan, kwa sababu ya mripuko wa ugonjwa wa Korona (Covid-19), kumekuwa ni mzigo mkubwa juu ya watu. Inasemekana kwamba Waislamu sasa wamebakia kuchagua ima njaa, kupitia kufungwa kwa miji, ama ugonjwa, kupitia kusambaa kwake kwa kasi. Hivyo, kwa upande mmoja wanashuhudia kusambaa kwa haraka kwa ugonjwa. Hata hivyo kwa upande mwingine, Waislamu wanapata tabu kwa kuongezeka umaskini, hali ngumu, kuanguka kwa biashara, kufungwa kwa viwanda na ukosefu wa ajira.

Hakika kuchagua njaa ama virusi ni utata wa kiulimwengu. Dola za Kimagharibi zinakabiliwa na shinikizo la kusitisha au kupunguza, ufungwaji wa miji, ili kupunguza mateso ya kiuchumi kwa watu. Kiulimwengu, ufungwaji wa miji umesimamisha sekta zote za kiuchumi, mamilioni ya watu kukosa ajira, kusababisha hasara ya matrilioni ya dolari na kulazimisha dola za kirasilimali kupeana mifuko mikubwa ya dhamana ya kifedha, ili kustawisha uchumi unao poromoka. Kwa upande mwingine, visa vya ugonjwa wa virusi vya Korona vimefikia mamilioni ya watu, huku vifo kwa ugonjwa huo vikizidi 100,000, ikisababisha uoga na hofu kote ulimwenguni.

Kiulimwengu, imani juu ya Urasilimali, kama mfumo ambao unaweza kuhudumia wanadamu, imetingishika kote ulimwenguni. Hata miongoni mwa dola za kirasilimali za Kimagharibi, watu wanatetemeka kwa kufeli kwa dola za kirasilimali kuwalinda kutokana na njaa na maradhi.

Kuhusiana na mkurupuko huu wa virusi, Uislamu wenyewe umepeana muongozo uliowazi juu ya njia mwafaka ya kupunguza athari za kiafya na hali ngumu za kiuchumi. Ziada ya hayo, kushikamana thabiti na Uislamu huhakikisha kudhibitiwa kwa mkurupuko wa ugonjwa, bila hata kuchukua hatua kali za kufunga nchi.

Uislamu umewajibisha karantini ya maeneo mkurupuko utakapoanzia. Mtume (saw) amesema,

«إِذَا سَمِعْتُمْ بِالطَّاعُونِ بِأَرْضٍ فَلَا تَدْخُلُوهَا وَإِذَا وَقَعَ بِأَرْضٍ وَأَنْتُمْ بِهَا فَلَا تَخْرُجُوا مِنْهَا»

“Mtakapo sikia mkurupuko wa ugonjwa katika eneo, msiliingie; na utakapotokea katika eneo mlilopo, msitoke.”[Bukhari]. Hakika kufeli kukarantini, ni sababu ya janga kubwa. Katika njia ya kuficha mkurupuko. China haiku karantini eneo la mkurupuko mapema, Wuhan, ikiruhusu kusambaa kwa virusi ndani ya China, na pia nchi nyengine kupitia safari za kimataifa, ikiwemo Iran, ambako ulisambaa hadi Pakistan. Katika suala la Pakistan, mkurupuko wa kindani ulianzia Taftan, kituo cha mpakani kwa wale waliotembelea mji wa Qom uliopo Irani, ambao ulikuwa na wafanyikazi wa Kichina kutoka katika Shirika la Reli la Kichina. Serikali ya Pakistan haiku karantini vikali eneo la Taftan, wakiwaachilia huru walio athirika, hivyo kuruhusu ugonjwa kusambaa sehemu zote za nchi. Kisha wakaacha wazi usafiri wa angani kwa mda mrefu, ikawa kama njia ya virusi kuingia nchini.

Zaidi, kote ulimwenguni, dola za kirasilimali, ambazo haziku karantini vikali na mara moja, zimeathirika na idadi kubwa ya walio athirika kwa ugonjwa na kufariki. 430,000 walisafiri kwenda Marekani kutoka China, ikiwemo kutoka katika eneo kitovu cha Mkurupuko, Wuhan, baada ya hatimaye China kufichua janga hili hali. Marekani ndio iliyo na idadi ya juu zaidi ya vifo kutokana na Covid-19, isiyo pungua 25,000, kufikia 14 Aprili 2020, na visa 603,694 vilivyo thibitishwa vya maambukizi, karibu ya thuluthi moja ya idadi jumla ya watu walio ambukizwa ulimwenguni.

Muongozo wa Uislamu kuhusiana na ugonjwa wa kuambukiza ni kwamba wagonjwa watenganishwe na walio wazima. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) asema,

«لاَ تُورِدُوا المُمْرِضَ عَلَى المُصِحِّ»

 “Msiwachanganye wagonjwa na walio ambukizwa” [Bukhari].

Walio ambukizwa lazima wawekwe mbali na walio wazima, ama kuwe na vizuizi vya kimada baina yao, au kwa wote. Serikali lazima ipeana usaidizi kwa ufanisi wa karantini ya majumbani, ndani ya vituo vya karantini na hospitalini. Pia ni jukumu la serikali kupeana vifaa vya kujikinga kwa wale wanao washughulikia walio athirika, popote walipo. Tayari watawala wa Pakistan wamezembea, ambapo imesababisha kuenea kwa virusi kwa jamii na pia wahudumu wa afya.

Zaidi ya hayo, kote ulimwenguni, dola za kirasilimali zimezembea katika kufaulisha kuwatenga walio athirika, ikiruhusu kusambaa kwa ugonjwa mijini, na pia hospitalini, ikipelekea vifo vya wahudumu wengi wa afya.

Uislamu pia umepeana muongozo juu ya ile idadi kubwa ya wabebaji virusi kisiri, wana maambukizi lakini sio ugonjwa, ambao husababisha mkurupuko wa haraka na kwa eneo kubwa. Uislamu umejukumisha serikali kuwa mlezi mwenye kujali mambo ya watu wake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) asema,

«كُلُّكُمْ رَاعٍ، وَكُلُّكُمْ مَسْؤولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، فَالأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ»

“Kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mmoja atahesabiwa juu ya kile anacho kichunga, na kiongozi wa watu ni mchungaji na atahesabiwa juu ya raia wake” [Bukhari,Muslim]. Hivyo, dola yaweza kuchukua vipimo vya halaiki mamilioni katika nchi yenye ukubwa kama Pakistan, ili kuwatambua wabebaji virusi kimya kimya katika wakati fulani. Dola kisha yaweza kuwatenga walio athirika na kufaulisha kuwatafuta walio jumuika nao, ikitoa umakini kwa wale wenye kinga dhaifu, kama vile wazee au wenye magonjwa kama pumu na kisukari. Vilevile dola inaweza kupeana barakoa na viyeuzi ili kupunguza kusambaa kwa ugonjwa. Dola inaweza kuelimisha watu juu ya kuweka umbali wa kijamii baina yao, inapohitajika, ili kupunguza kusambaa kwa maradhi haya, kuliko kutumia nguvu au kutia hofu.

Katika njia hii, Uislamu unahakikisha kwamba serikali inapunguza mkurupuko kutoka mwanzo, kudhibiti ukuwaji wake na kuzuilia balaa kwa nchi, mpaka isifikie hatua ya kufunga miji kabisa, kama ilivyo tokea katika dola nyingi za kirasilimali ikiwemo Marekani. Hakika kufungwa kikamilifu kwa miji huongezea tu tatizo juu ya tatizo la virusi, kwa kubuni tatizo la njaa kali. Hivyo, kushikama na Uislamu kunahakikisha kwamba maisha yanaendelea vizuri, ikiruhusu Waislamu kutimiza majukumu yote ya Kiislamu, huku wakichukua tahadhari, kama vile uchumaji, kukimu familia, kutafuta elimu na kuswali kwa jamaa misikitini.

Ama kuhusu jambo la kupeana fedha za kutosha ili kusimamia mkurupuko kama huo, Uislamu ni bora kuliko Urasilimali, mfumo uliotungwa na mwanadamu unaotawala dunia kwa sasa. Hakika, mkurupuko wa maradhi ya virusi vya Korona umefichua dosari na umbile tete la uchumi wa kirasilimali. Urasilimali umehakikisha kuwa utajiri mwingi wa nchi umejazana mikononi mwa watu wachache. Ni kwa ukweli huu, ndio uliozifanya hata dola za kirasilimali za Kimagharibi kushindwa kuwawajibikia raia wake, huku hali hii ikiwa mbaya zaidi nchini Pakistan. Hakika, Urasilimali wenyewe ni mzigo juu ya wanadamu, ukiwalazimisha kuchagua kati ya njaa na virusi.

Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاء مِنكُمْ)

“…ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu..” [Al-Hashr 57:7]. Kipekee Uislamu unakataa muundo wa ukuwaji wa uchumi wa kirasilimali, ambao unaangazia uzalishaji, kupitia muundo fulani wa kiuchumi, kwa muundo wa kiuchumi, unao angazia usambazaji na mzunguko wa mali.

Ili kusiwe na ulegevu wa mambo msingi, kama vile matumizi ya rasilimali za afya, Uislamu unahakikisha mapato mingi kwa dola, kupitia dola kuzitawala sekta zenye mitaji mikubwa, ikiwemo utengenezaji kwa wingi. Sunnah zenye Baraka za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) zilizindua miundo ya kampuni za ‘Inaan, Abdaan na Mudarabah’ ambazo kimaumbile zinaweka kikomo kiwango cha mitaji uliopo kwa sekta za kibinafsi, ikiuwekea kikomo uwezo wake wa kumiliki sekta zinazo hitaji mtaji mkubwa zinazo hitaji msaada mkubwa wa kifedha, wakati wa majanga. Uislamu unahakikisha kwamba mapato yanayo patikana katika kawi na madini yanatumika kunufaisha Ummah mzima wala si watu wachache, kupitia ubinafsishaji. Hakika, Sunnah zenye Baraka za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) zimelazimisha kwamba rasilimali za kawi na madini ziwe ni mali ya Ummah, na faida yake ni kwa mambo ya Ummah. Uislamu pia umekataza dhambi la madeni yenye riba, iwe ni kwa muundo wa mikopo ya nje au bondo za hazina za ndani. Dhambi baya la riba ndio chanzo cha madeni makubwa ya kitaifa kote ulimwenguni na, katika swala la Pakistan, nyingi ya bajeti yake hutumika juu ya madeni ya riba.

Hivyo, badala ya kupoteza mapato kwa kulipa madeni yenye riba,serikali inaeza kutimiza majukumu yake kwa raia, wakati wa majanga na wakawaida. Hakika, Uislamu haukuacha ugonjwa ama njaa kama chaguo, kwani ni jukumu la serikali kutatua shida zote za njaa na maradhi. Sunnah zanye Baraka za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) zilibuni huduma za afya na utoaji wa mahitaji kama majukumu ya serikali. Mtume (saw) amesema,

«مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ آمِنًا فِي سِرْبِهِ، مُعَافًى فِي جَسَدِهِ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ، فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا»

 “Yeyote atakaye pambaukiwa miongoni huku akiwa na amani katika familia yake, wenye afya nzuri katika mwili wake; akiwa na chakula cha siku yake, ni kama anaye miliki dunia nzima” [At-Tirmidhi]

Ama katika kupeana huduma imara ya afya, kwa uwezo mkubwa wa hazina kushughulikia dharura, mkurupuko wa ugonjwa wa virusi vya Korona umefichua umbile tete la mifumo ya afya ya kirasilimali. Urasilimali umelazimisha mapungufu katika uwezo wa sekta za afya, kwa kusisitiza juu ya faida kubwa bila hasara, kote katika sekta ya afya ya kibinafsi na ya dola. Lakini, Uislamu huichukulia dola kama msimamizi na kulinda afya ya raia kama wajibu ambao ni lazima iutimize. Muslim ameripoti kutoka kwa jabir (ra) ambaye amesema

«بَعَثَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم إِلَى أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ طَبِيبًا فَقَطَعَ مِنْهُ عِرْقًا ثُمَّ كَوَاهُ عَلَيْهِ»

“Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alituma daktari kwa Ubay bin Kaab, akaukata mshipa wake kisha akauchoma.” Katika uwezo wake kama kiongozi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alituma daktari kwa Ubay, hili ni dhihirisho kwamba afya na huduma za madawa ni miongoni mwa mahitaji msingi kwa raia, kwamba dola ni lazima ihakikishe huduma hizi zinapatikana kwa kila anaye hitaji bila malipo.

Hivyo, katika Uislamu, dola ni lazima ipeane viwango vya kutosha vya vifaa vya kiafya vinavyo zalishwa ndani ya nchi, ikiwemo vidirishi (ventilators) na vifaa vya kujilinda. Dola ni lazima iasisi vituo vya utafiti, ili kuchunguza njia zote za kuimarisha kinga kwa maambukizi, iwe ni kupitia lishe, mazoezi au madawa, katika njia zote, ikiwemo mitishamba ama nyongeza za vitamini.

Dola ni lazima pia itafiti uwezekano wa idadi ya watu kuendeleza kinga asili kwa mikurupuko fulani ya maambukizi, pamoja na usalama na ufanisi wa chanjo.

Uislamu haukupeana tu muongozo wa kupunguza madhara ya kiafya na ugumu wa kiuchumi kutokana na mikurupuko ya maambukizi pekee, pia umepeana muongozo wa namna Waislamu wanavyo stahili kuchukulia upoteaji wowote wa uhai, wakati wa mikurupuko kama hiyo. Bukhari amesimulia kutoka kwa mama wa waumini, Aisha (ra), mke wa Mtume (saw), amesema kwamba, “Nilimuuliza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw) kuhusu tauni. Akaniambia kwamba,

«أَنَّهُ عَذَابٌ يَبْعَثُهُ اللَّهُ عَلَى مَنْ يَشَاءُ وَأَنَّ اللَّهَ جَعَلَهُ رَحْمَةً لِلْمُؤْمِنِينَ لَيْسَ مِنْ أَحَدٍ يَقَعُ الطَّاعُونُ فَيَمْكُثُ فِي بَلَدِهِ صَابِراً مُحْتَسِباً يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا يُصِيبُهُ إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَهُ إِلَّا كَانَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ شَهِيدٍ»

“Hakika yake ni adhabu iliyotumwa na Mwenyezi Mungu kwa yule amtakaye, na hakika Mwenyezi Mungu akaijaalia ni chanzo cha huruma kwa walio amini, na hakuna yeyote atakaye patwa na tauni kisha akabakia ndani ya mji wake akiwa mvumilivu akitarajia malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na akijua kuwa halimsibu jambo isipokuwa lile aliloandikiwa na Mwenyezi Mungu, isipokuwa atapata malipo mithili ya shahidi.” Hivyo mbali na kuzama kwenye hofu na uoga, Waislamu huwa na uvumilivu katika mtihani wao, wakitarajia malipo na kudumu katika kuomba Dua kwa Mola wa Walimwengu (swt), Mwenyezi Mungu, kwa msaada wake katika kuhimili mtihani huo.

Enyi Waislamu wa Pakistan kwa jumla na haswa Watoto Wetu Watukufu katika Vikosi vya Majeshi!

Kupitia kimoja kati ya viumbe vyake (swt), Mwenyezi Mungu (swt) amedhihirisha kwa viumbe vyote, kufeli na batili ya sheria za mwanadamu, za Urasilimali, iwe inatabanniwa Mashariki, na China, ama katika Magharibi, na Marekani. Jukwaa litengenezwa kwa ajili ya Ummah bora ulioletwa kwa wanadamu, Ummah wa Kiislamu, ili upeane muongozo kwa Wanadamu, kwa kutabikisha yote aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«اَلْإِسْلَامِ يَعْلُو وَلَا يُعْلَى»

“Uislamu unaelea na wala hakuna kinacho elea juu yake kuwa” [Ad-Daraqutni]. Hakika, Dini yetu adhimu, Dini ya Haki, Uislamu, iko juu kuliko mifumo yote ya maisha iliyo undwa na mwanadamu, ikiwemo Urasilimali, ambao tumeuona. Uislamu umeteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) na unapeana muongozo bora na ufafanuzi wa kila tatizo la mwanadamu.

Ulimwengu umeshuhudia kufeli kwa Urasilimali kivitendo, hata katika vigogo wao, dola za Kimagharibi, ikiwemo Amerika. Ulimwengu uko zaidi ya tayari kuuona Uislamu unatabikishwa kivitendo, na Khilafah kwa njia ya Utume.

Lakini, badala ya kutabikisha Uislamu, watawala wa Pakistan wao huigiza kile wanachoona washirika wao Wamagharibi wanacho kifanya, bila ya kuzingatia utata na udhaifu wa mifumo ya wanadamu, ukilinganisha na ukamilifu na nguvu za sheria za mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنْكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ)

“Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la Buibui, laiti kuwa wanajua.”[Surah al-Ankabut 29:41]. Watawala waliofilisika wa Waislamu wanafuata sheria, maadili  na sera za mfumo wa kikafiri, wa Urasilimali, kiupofu, ingawa Mtume (saw) ameonya,

«لَتَتَّبِعُنَّ سُنَّةَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ بَاعًا بِبَاعٍ وَذِرَاعًا بِذِرَاعٍ وَشِبْرًا بِشِبْرٍ حَتَّى لَوْ دَخَلُوا فِي جُحْرِ ضَبٍّ لَدَخَلْتُمْ فِيهِ»

“Mtafuata mienendo ya wale waliokuwa kabla yenu, mkono kwa mkono, dhiraa kwa dhiraa, shubiri kwa shubiri, mpaka wakiingia katika shimo la mburukenge nanyi mtaingia” Wakasela: “Ewe mtume wa Mwenyezi Mungu, (unamaanisha) mayahudi na manaswara?” Mtume (saw) akasema, «فَمَنْ إِذًا؟» “Nani wengine?” [ibn Majah]

Hakuna matumaini katika watawala wa Pakistan, kutuongoza ama kuwasilisha Uislamu kama mfano wenye kung’aa kwa wanadamu katika muda huu unapo hitajika. Mwezi ulio barikiwa wa Ramadhan na neema zake nyingi, hakika ni muda wetu sote kujitahidi katika kuisimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume, kupitia kuilingania, upande wa Muislamu kawaida, na kupitia kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir ili utabikishwe mara moja, upande wa wale Waislamu walio katika vikosi vya majeshi. Tujitahidi kupata radhi za Mwenyezi Mungu (swt), tukitafuta ushindi wake (swt), ili utukufu wa Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) usimamishwe dhahiri kivitendo kwa kila nafsi ione, itoe njia kwa wanadamu kuukubali Uislamu makundi kwa makundi, kama ilivyo tokea baada ya Ufunguzi wa Makka na Dola ya Kiislamu ya Madina, katika mwezi ulio barikiwa wa Ramadhan. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

(إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ * وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّهِ أَفْوَاجًا * فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا)

“Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na Ushindi.Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu Kwa makundi, zitakase sifa za Mola wako mlezi, na umwombe msamaha; hakika yeye ndiye anaye pokea toba.” [An-Nasri 1-3]

#Covid19     #Korona    كورونا#

H. 22 Sha'aban 1441
M. : Jumatano, 15 Aprili 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu