Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 “Makubaliano” Yaliyo Kuwa Katika Uchungu wa Uzazi Sasa Yamezaa Serikali ya Diab! Mawaziri Kutoka Tabaka la Kisiasa Waliingizwa Kupitia Kila Mlango!
(Imetafsiriwa)

Kwa takribani siku mia moja, watu wanaandamana mabarabarani wakitaka kuporomoka kwa nidhamu fisidifu na kuondolewa kwa tabaka fisadi la kisiasa, kwa kutumia kauli mbiu "Wote Humaanisha Wote", msemo wa umma wa kupinga chama chochote kinacho wakilisha tabaka fisadi la kisiasa nchini humu.  

Mashetani wa kisiasa waliitumia harakati hii ya ghafla na watu wake, kuwashughulisha watu usiku na mchana kwa kupunguza thamani ya pauni ya Lebanon dhidi ya dola ya Amerika, kisha ndani ya wasaa wa kisanii, katika mkesha wa kuamkia tangazo la serikali mnamo 20/1/2020, Muungano wa Ubadilishanaji wa Pesa ukatangaza, chini ya shinikizo kutoka kwa benki, mtawala na mamlaka yake, kupitia taarifa rasmi, ambayo haina uwezo wa kisheria, ulitangaza kukifunga kiwango cha ubadilishanaji wa pauni kwa dola kwa kiwango maalumu kisicho badilika katika soko la sambamba, kwa pauni elfu mbili kwa dola! Ndio, hivyo tu, kwa sababu mamlaka haya na mtawala huyu hayakuwaepusha kutokana na mgogoro huu mkali wala kuilinda nchi kutokana na kuporomoka, bali uamuzi halisi wa kisiasa uliopitishwa na serikali ulitangazwa saa chache tu baada ya taarifa ya muungano huo! Kiuhakika ulitangazwa siku chache tu baada ya ziara ya kisiri ya mweka hazina wa Amerika Richard Harvey!!     

Serikali ya Diab, ambayo ilitangazwa mnamo Jumanne jioni, 21/1/2020, baada ya kwenda mbele na nyuma mabarabarani, kuwashinikiza wale waliomharibu mtawala wa nchi upande wa Iran na nyuma yake ni Amerika kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kupitia dola inayozunguka pambizoni mwake ikimaanisha Iran, au kupitia kibaraka jirani wa Amerika, serikali katili ya Bashar, ambayo utawala wa Amerika unatafuta kuiokoa kupitia pafu la Lebanon, baada kuzorota kukubwa kwa pauni ya Syria, na hofu ya kupamba moto kwa mapinduzi ya watu huko. Muundo wa serikali, ambayo Diab anadai, unatokana na wataalamu, na kwa uchache majina yanaonyesha utiifu wa mawaziri hawa na utumishi wao kwa mashetani wa tabaka fisadi la kisiasa, kwani inaonekana kwamba wao ni mgao wa wanasiasa pasi na aibu. Natija yake, wengine wote walio salia katika waandamanaji waliiita serikali hiyo (serikali ya mgao), msemo unaoonyesha kuwa inadhihirika kuwa ni serikali ya wataalamu bandia, huku kiuhalisia ikiwa ni serikali inayowakilisha mgao wa wanasiasa.  

Serikali ya kuchekesha inayokufanya ulie wakati huo huo kutokana na kuwa mawaziri, ambao hawana taaluma isipokuwa kwa majina tu au ambao wamewekwa kama mawaziri sio kutokana na uwezo wao bali ili kumridhisha rais na mkwe wake pekee, au upande wa Iran, au rais wa baraza, au "zimwi" la Zgharta, au "mwanamfalme" wa milimani… Na kabla ya yote haya, la muhimu zaidi, ni ridhaa ya bwana wao Amerika. Ama kuhusu watu, mwendo, uchungu, makelele yao na kupinga kwao, hukabiliwa kwa gesi ya kutoa machozi, magari ya kufyatua maji, sauti za mabomu, risasi za mpira, sanaa za ukandamizaji na kuvunja vunja katika umbile la wababe wa kivita na madhehebu ya kisiasa, na dhehebu la migao… Serikali ambayo inaanza kazi yake kwa taarifa kutoka kwa Waziri wa Kawi Raymond Roma aliyesema: "Umeme 24/24 hautapatikana ndani ya miezi sita…" hivyo pokeeni bishara njema ya usalama wa muda mrefu enyi Mirba! 

Njia zozote zile zitakazokuwa zimetumiwa kuunda serikali hii, kwa yakini ni serikali inayopitisha muda, ili kuavya harakati za watu waliosalia na kujaribu kuwaondoa mabarabarani, na kuzuia uchaguzi wa mapema unaofichua kina cha mgogoro huu wa wanasiasa wa kawaida, ambao wangali wanataka kuamiliana na Amerika, ingawa mfuko wa uchaguzi nchini Lebanon uko mikononi mwa tabaka hilo fisadi, linalo uendesha kwa maslahi yao wenyewe na yale ya mabwana zao. Serikali, ambayo ingawa ni ya muda, ni natija ya mbinu ya Amerika ya kukataa kuibadilisha serikali ya vibaraka wake kupitia mapinduzi au maandamano barabarani, kwa gharama yoyote ile, na yale yaliyojiri nchini Syria na Misri na yale yanayojiri nchini Iraq hayako mbali.

Enyi watu, tunawaambieni kwa kinywa kipana: Hakuna mabadiliko ndani kwa ndani ya nidhamu hii, wala mageuzi kwa wanasiasa kama hawa au mithili yao, bali suluhisho ni kuigeuza nidhamu hii yote iliyo juu ya vichwa vya watu hawa, na kuibadilisha kwa nidhamu inayo wawakilisheni. Na hatuioni nyingine ila nidhamu ya Mola wa Walimwengu na nyinyi ungeni bogi la mabadiliko katika eneo hili kwa jumla na Ash-Sham haswa, inayolingania kusimamisha nidhamu ya uadilifu na uongofu, Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, inayochunga mambo ya watu, watu wote, hivyo fanye uamuzi, ili Mwenyezi Mungu Mtukufu awaleteeni afueni kwa haraka.

 (قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ قُلِ اللَّهُ يَهْدِي لِلْحَقِّ أَفَمَن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّي إِلَّا أَن يُهْدَىٰ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ)

“Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina anaye ongoa kwendea Haki? Sema: Mwenyezi Mungu anaongoa kwendea Haki. Basi, je, anaye stahiki kufuatwa ni yule Mwenye kuongoa kwendea Haki au asiye ongoa ila aongozwe yeye? Basi nyinyi mna nini? Mnahukumu namna gani?” [Yunus: 35]

H. 28 Jumada I 1441
M. : Alhamisi, 23 Januari 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu