Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Amerika na Miungano yake imeingiwa na Wazimu wa Kupindukia kwa Kufeli kwao Kuwanyamazisha Watu wa Ash-Sham Wamezidisha Uingiliajikati wa Kijeshi Kiwanjani, sio tu Angani, ili Kulazimisha Kujisalamisha kwa Madai yao!

(Imetafsiriwa)

Ndani ya miaka sita, Amerika imefanyakazi kwa nguvu kupitia njia zake tofauti tofauti ili kuwasalimisha watu wa Ash-Sham mbele ya dhalimu ili kukubali mashambulizi na mauaji yake. Lakini hawakufaulu na licha ya kutumia kila njia zikiwemo za umwagaji damu na za kikatili. Ilitumia mizinga ya angani na baharini. Kisha ikawatumia Iran na kufuatiwa na Urusi. Kisha polepole ikafuatiwa na wanamgambo wa kiwanjani kuanzia wadogo hadi wakubwa kwa jina la nchi za maeneo, wakati mwengine kama Uturuki na Iran na wanamgambo washirika wa Iran ambao huwasili kwa majina tofauti tofauti na kisha kuhusishwa na miungano ya makundi ya kindani… Yote hayo yametekelezwa kiuwazi nayo na wakati mwengine na miungano yake na majambazi wake wakati mwengine…

Kilichotia hofu miungano hii ni kuwa hakuna mzozo wa kimataifa ndani ya Syria, bali Amerika ndiyo inayoshikilia nguzo za ushawishi na sio kama hali ya Libya au Yemen… Pia nguvu za maeneo yaliyo jirani na Syria ni tiifu kwa Amerika, vibaraka na wafuasi; hata wale ambao wamekita katika kuegemea Uingereza kama vile Jordan wamefungwa na sera ya Uingereza kutoipinga Amerika lakini wanaweza kuwa kikwazo lau wataweza kufanya hivyo… Kwa kuongezea, upinzani ulioko, wengi wao wanatumia pesa chafu na msaada wa kisilaha dhidi ya ndugu zao na yote hayo ni kwa maagizo ya Amerika…

Kwa kuongezea katika njama zilizowekwa na Amerika kama vile kupunguza vita na makubaliano ili kusitisha kupigana ambayo yamelazimishiwa upinzani lakini sio kwa utawala! Na udhibiti wake wa msaada wa pesa chafu na uzuiaji wa silaha na hatimaye kuweka maeneo yaliyopungua vita… Na wakati huo huo hakuna yeyote anayesimama mbele ya Amerika na washirika wake na vibaraka wake isipokuwa makundi ambayo si makubwa na kwa kuongezea ni watu wa Ash-Sham ambao ni mukhlisina na wakweli kwa Mola wao, dini yao na Ummah wao. Yote haya yanaashiria kuweko kwa nguvu za kimwili katika mikono ya maadui wa Uislamu: Amerika, miungano yake, vibaraka wake na wanafiki… sio kuwa ndiyo itakayoamua ushindi na kushindwa…

Hivyo basi, Amerika pamoja na washirika na vibaraka wake walishtushwa na kuingia wazimu na inawastahili kuingiwa na wazimu. Kwa kuwa imemaliza njia zake zote za kutekeleza mipango yake ya kuhakiksha kuwa inapata uungwaji mkono kutoka katika baadhi ya watu mukhlisina wa Ash-Sham lakini ilifeli… Inaonekana kwamba hawana tena mbadala isipokuwa kulazimisha suluhisho walilopanga kwa kuzidisha vitendo vya kijeshi na sio tu kwa mashambulizi ya angani na baharini au timu maalumu, wajuzi, washauri na mfano wake lakini kwa kuzidisha jeshi la kiwajani kufikia kiwango cha kufanana na ukoloni wa kijeshi lakini wanaipa sura tofauti na kudai kuwa ni “vita dhidi ya ugaidi” ilhali wao ndio asili ya ugaidi na matawi yake.


(قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُون)َ“Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Al-Munafiqun: 4]

Kwa kuongezea sio jambo la kushangaza kwamba wanatoa sababu nyingine kama uungwaji mkono kutokana na maamuzi ya kimataifa!... Hivyo basi mazingira ya mzunguko wa sita wa mikutano ya Astana mnamo 15/9/2017:” … Waziri wa Kigeni wa Kazakhstan akiwa katika mkutano uliofanyika Ijumaa ili kutangaza taarifa ya mwisho ya mazungumzo ya Astana alisema: maeneo yaliyopungua vita yatabakia katika hali hiyo kwa kipindi cha miezi sita na kuna uwezekano wa kuendelea … Mzunguko wa sita wa mazungumzo ya Astana ni rasmi kuwa yanaendelea ndani ya mji mkuu wa Kazakhstan kwa siku ya pili huku yakiongozwa na msururu wa mikutano baina ya wajuzi wa dola wadhamini za Urusi, Iran na Uturuki… shirika la habari la Anatolia liliripoti kwamba “kuna makubaliano yaliyoafikiwa ndani ya Astana kuhusu mipaka ya maeneo yaliyopungua vita ndani ya Idlib, Syria na kuongezea kwamba mazungumzo yanaendelea ili kujaribu kufikia makubaliano juu ya vikosi vipi vielekezwe katika mkoa wa Syria wa Idlib… Siku ya kwanza ya mikutano mnamo Alhamisi, Rais wa Kazakhstan” alitangaza kuwa nchi yake ilikuwa tayari kutuma vikosi vya amani nchini Syria lau Baraza la Usalama litakubaliana juu ya hilo…” Taarifa ya Nazarbayev pia ilithibitishwa na Orient.net mnamo 14/9/2017 ambapo ilimnukuu akisema katika mkutano wa waandishi wa habari ndani ya Astana mnamo Alhamisi ikisadifiana na uzinduzi wa mzunguko wa sita: “Lau UN itaamua kutuma kikosi kama hicho [kwenda Syria] basi sisi, kama wanachama wa UN, tunaweza kutuma jeshi letu kushiriki [katika oparesheni ya kuweka amani].”

Taarifa hizi ziko wazi katika dhamira yake ya kijeshi. Kujumuishwa kwa Idlib katika mzozo kunatofautiana na maeneo mengine, kwa kuwa wamewakusanya wapiganaji ndani yake ambao wanawaita ni magaidi au wasiokuwa na misimamo laini, wamewakusanya kupitia makubaliano ya usitishaji upiganaji na mfano wake… Hili liliashiriwa na taarifa zilizotolewa na maafisa wa dola hizo hususan Uturuki na makundi yake ndani ya Idlib. Sputnik ilichapisha mnamo 17/9/2017: Chanzo cha ndani katika mji wa mpakani wa Kielce unaopakana na Syria kilisema kuwa Jumatatu kwamba mji unashuhudia kukithiri kwa wanajeshi wiki moja iliyopita na vikosi vya kujihami vya Uturuki vimekuwa vikituma vikosi vya kuimarisha katika mpaka wa Syria takribani wiki moja iliyopita… Kwa upande wake, mwanajeshi wa Kiuturuki aliyeko katika mpaka wa Syria aliiambia Sputnik kwamba jeshi la Uturuki limekuwa likikusanya vikosi vyake vya kijeshi na zana zake kwa siku tatu ndani ya mji wa Rihaniyah, mkoa wa Iskenderun mkabala na mji wa Syria wa Idlib…

Hili ni kuongezea katika kiashirio, bali tangazo la Rais wa Kazakhstan kuhusiana na uingiliajikati wa kijeshi kutokana na maamuzi ya Baraza la Usalama. Na kwa kuwa hatoi taarifa hiyo kwa mawazo yake mwenyewe (kwani sio wa mkono wa kulia!), hivyo basi hatamki kwa ulimi wake lile ambalo mkono wake hauwezi kufikia bali anazungumza lile ambalo Amerika na vibaraka wake wamemuamrisha… Kwa hiyo inaonekana kwamba muhalifu Amerika alikuwa hana muda wa kupoteza katika kumlinda dhalimu wa Ash-Sham kuwa hai kwa kumpa pumzi za kirongo mpaka pale itakapopata mbadala lakini ilionelea kulichangamkia suala hilo ambalo ni uvamizi wa kijeshi kwa jina la uhalali wa kupigana na ugaidi na uhalalishwaji wa jamii ya kimataifa! Ili kuwalazimisha watu wa Ash-Sham kukubali dhalimu mpya msekula kwa kudhania lau maadui wa Uislamu watafaulu kufanya hivyo. Dhana yao hiyo imewapelekea kuangamia na itawapelekea kuangamia kwa uwezo wake Al-Qawee, mwenye Nguvu, Al-Aziz, Mtukufu Muweza.

Enyi Watu Mukhlisina wa Ash-Sham: Mumewashtusha Amerika na washirika wake kwa kuwa makini kwenu katika maamuzi na ikhlass yenu kwa Mola wenu. Yote haya na licha ya kuwa makundi ya upinzani yanayopambana nayo ni madogo kiidadi na yaliyotapakaa hapa na kule na yasiyokuwa na uongozi wa kisiasa unaoyaunganisha pamoja. Kwa hiyo itakuwaje lau makundi yaliyotapakaa lau yataunganishwa chini ya kundi moja katika chungu kimoja ambacho ndani yake na nje yake kinamulikwa na nura ya Uislamu? Zaidi ya hilo, makundi ambayo yanakula pesa chafu na kupigana miongoni mwao, na kumuacha adui wa nchi yao na watu wao, hawa ni watoto wenu na ndugu zenu, kwa hiyo washikeni mikono yao na muwe katika kambi ya Iman na musiegemee kwa maadui wa Uislamu…

Masuala haya mawili: kukosekana uongozi wa kisiasa ambao unayaunganisha makundi haya na kuyaongoza pamoja na uegemeaji wa makundi hayo kwa maadui wa Uislamu na kuwategemea kwa pesa chafu, mambo haya mawili ni mpasuko hatari wa kuta zenu za ndani na tiba ya nyufa hizi zipo mikononi mwenu kwa hiyo zipeni umuhimu na uvumilivu unaostahili.

Enyi Waislamu kokotemliko: Amerika na washirika wake wanapanga kuweka uvamizi wa kijeshi kwa kutumia majina mapya, na wanataka sio tu kutumia uingiliajikati wa angani na sio kwa vikosi vyao au wajuzi wao maalum… bali ni kutumia vikosi sawa na majeshi na kuzalisha majina ya uhadaifu kwa ajili yake: kupigana dhidi ya ugaidi au maamuzi ya jamii ya kimataifa. Hili ni jambo hatari ambalo litalirudisha eneo katika sura mbaya ya zamani ya ukoloni wa kijeshi hata kama itakuwa katika vazi la kisasa linalozungukwa na kambi za wavamizi… Kufaulu kwao katika kutekeleza hili ndani ya ardhi ya Ash-Sham itakuwa ndio mwanzo wa kuingia kwao ndani ya ardhi nje ya Ash-Sham na kisha ule msemo wa zamani wa “Nilimalizwa siku ile ambapo ngómbe mweupe alipoliwa” na itakuwa ni kwa kila mtu na kila mmoja atakuwa anajuta lakini itakuwa sio muda wa kujutia. Hili ni jambo la kufanyiwa maamuzi na sio la mzaha. Linahitaji mtu kuwa makini sana na mipango mizuri na kufikiria kwa kina. Kwa kuwa lililowafanya maadui zenu kuwa na ujasiri dhidi yenu ni kuanguka kwa muundo wa Khilafah, ambao ulikuwa unawapa kivuli na kusimamishwa kwa muundo huu kupo katika mikono yenu hususan ya wale walio na nguvu miongoni mwenu, ili kuwaondosha watawala Ruwaibidhah wanaowasifu wakoloni Makafiri na kisha miungano yao itakimbia na maadui wa Uislamu hawatonufaika na kambi zao.

(...وَظَنُّوا أَنَّهُمْ مانِعَتُهُمْ حُصُونُهُمْ مِنَ اللَّهِ فَأَتاهُمُ اللَّهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُو) “nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda na Mwenyezi Mungu. Lakini Mwenyezi Mungu aliwafikia kwa mahali wasipo patazamia...” [Al-Hashr: 2]

Enyi Watu wa Syria na Enyi Waislamu kokotemliko: Mumeona namna gani maadui zenu licha ya nguvu zao kubwa hawajaweza kuwalazimisha katika miradi yao kwa miaka yote hii. Kuweko kwenu na msimamo kumeonyesha kuwa kupitia msaada na muongozo wa Mwenyezi Mungu kwamba maamuzi ya maadui zenu ni dhaifu na mioyo yao ni mitupu licha ya nguvu zao kuwa kubwa. Ni madhaifu katika kupambana na waoga wanapo kutana na hatari… Lakini muoga anaweza kupatiliza nyufa zilizomo ndani ya ukuta wa adui wake na kuvunjika kwa muundo wa adui wake na kisha muoga akawa jasiri kama simba. Sio kwa kuwa ana nguvu za kweli bali ni kutokana na nyufa katika ukuta wa adui na kuvunjika kwa muundo wa adui…Na kwamba Hizb ut Tahrir, muasisi asiyedanganya watu wake, anawaonya kuwa musiwache nyufa hizi na kuanguka pasina na suluhisho ambalo ni sahihi na linalothibitiwa na Uislamu. Suala hili halitokuwa sawa isipokuwa kwa lile ambalo ni sahihi kutokea mwanzo nalo ni kutawaliwa na lile ambalo Mwenyezi Mungu ameleta wahyi juu yake na majeshi kusonga mbele kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na hakuna suluhisho jengine… Na kwamba jibu kwa Hizb ut Tahrir kuhusiana na onyo lake na kutahadharisha kwake litawafaulisha kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kupata utukufu hapa duniani na utukufu Akhera.

(يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ * وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِنَ اللَّهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ) “Atakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani nzuri nzuri katika Bustani za milele. Huko ndio kufuzu kukubwa. Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini” [As-Saf: 12-13]

(إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ) “Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa wenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia” [Qaf: 37]


H. 2 Muharram 1439
M. : Ijumaa, 22 Septemba 2017

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu