Jumatano, 27 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Enyi Wanajeshi wa Kiislamu, Je, Hakuna Salahuddin Mpya Miongoni Mwenu?
Kukuongozeni Katika Kuwanusuru Mashahidi na Kuliondoa Umbile la Kiyahudi?
(Imetafsiriwa)

Mayahudi wanaikalia kimabavu ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, wanaua watu, wanachoma miti na wanabomoa mawe, na nyinyi mmenyamaza kimya bila kutikisika!

Mayahudi wanaikalia kimabavu ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, wakiua vikongwe, wanawake na watoto... na nyinyi mmenyamaza kimya bila kutikisika!

Mayahudi wanaikalia kimabavu ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, wanavunja misikiti, shule na hospitali na wanaua wagonjwa, na nyinyi mumetulia tuli!

Mayahudi wanaikalia kimabavu ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, wakiua shahidi baada ya shahidi mjini Gaza na hata ardhi yote ya Ash-Sham, na nyinyi mumenyamaza kimya bila kutikisika!

Mayahudi wanaikalia kimabavu ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, wamemfikia kiongozi wa Hamas, mtu shujaa, mchamungu na msafi, Mwenyezi Mungu akipenda, Yahya Sinwar, ambaye amepata moja ya kheri mbili baada ya ushujaa wake kulichosha umbile la Kiyahudi kwa Kimbunga cha Al-Aqsa kwa mwaka mzima wa mapigano, na kwa idadi na vifaa vichache kuliko Mayahudi waliokuwa na silaha nzito… na yote hayo bila ya ninyi kumnusuru! Na munaizunguka Palestina kutoka ardhi ya Misri (Kinanah) mpaka Jordan, Saudi Arabia, Syria, Iraq, Uturuki na Iran kana kwamba jambo hilo haliwahusu, kana kwamba muko katika ardhi fulani ya mbali, na mumekaa kimya bila kusonga!

Enyi Wanajeshi katika nchi za Waislamu… Je! nyinyi sio askari wa Umma bora kabisa ulioletwa kwa ajili ya Wanadamu?

Je, damu yenu haichemki katika mishipa yenu munapoona uvamizi wa kikatili wa Mayahudi dhidi ya ndugu zenu kila siku, hakika kila saa usiku au mchana?

Je, hamutamani kuwa miongoni mwa Ahlul-Bushra (watu wa bishara njema) kupitia jihad yenu?

[يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُمْ بِرَحْمَةٍ مِنْهُ وَرِضْوَانٍ وَجَنَّاتٍ لَهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُقِيمٌ]

Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu. [At-Tawbah: 21]?

Je! hazikutikisini Aya za Mwenyezi Mungu kwa kupigana na walio watoa kaka zenu na dada zenu majumbani mwao?

[وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni [Al-Baqarah: 191]?

Je, humkukumbuka Mwenyezi Mungu alivyowaandalia askari mujahidina katika mema mawili?

[قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَا إِلَّا إِحْدَى الْحُسْنَيَيْنِ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَنْ يُصِيبَكُمُ اللَّهُ بِعَذَابٍ مِنْ عِنْدِهِ أَوْ بِأَيْدِينَا فَتَرَبَّصُوا إِنَّا مَعَكُمْ مُتَرَبِّصُونَ]

Sema: Hivyo mnatutazamia litupate lolote isipo kuwa moja katika mema mawili? Na sisi tunakutazamieni kuwa Mwenyezi Mungu akufikishieni adhabu itokayo kwake, au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeni, nasi tunangoja pamoja nanyi.” [At-Tawbah: 52]?

Je, hamkukumbuka misimamo ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) dhidi ya Mayahudi wa Banu Qaynuqa, Banu Nadhir, Quraydhah na Khaybar walipofanya ufisadi na kueneza ufisadi katika ardhi?

Je, hamkuwakumbuka Khulafaa’ ar-Rashideen (Makhalifa Waongofu) walioutukuza Uislamu na Waislamu na wakapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kikweli, Mwenyezi Mungu awe radhi nao na wao wawe radhi Naye?

Je, hakuna Qutaybah, mfunguzi wa Bukhara na Samarkand, miongoni mwenu? Je, hakuna Ibn al-Qasim, mfunguzi wa India na Sindh, miongoni mwenu? Je, hakuna Ibn Ziyad, mfunguzi wa Andalusia, miongoni mwenu? Mlango-Bahari wa Gibraltar ungali unaitwa kwa jina lake, ufunguo wa Andalusia. Je! hakuna al-Mu'tasim miongoni mwenu, msfunguzi wa Amuriyya?

Je, hakuna Salahuddin, mshindi wa Wapiganaji Msalaba na mkombozi wa Bayt al-Maqdis miongoni mwenu? Je! hakuna Qutuz na Baybars, washindi wa Wamongoli huko Ain Jalut nchini Palestina?

Je, hakuna miongoni mwenu mfunguzi wa Konstantinopoli, ushahidi wa Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambayo imepokewa na Ahmad, ambaye alisema: Abdullah bin Bishr Al-Khath'ami aliniambia kutoka kwa baba yake kwamba alimsikia Mtume (saw) akisema:

«لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

“Kwa yakini mtaifungua Konstantinopoli. Kamanda bora ni kamanda wake, na jeshi bora ni jeshi hilo (litakaloifungua).”

Je, hakuna miongoni mwenu Abdul-Hamid, mlinzi wa Palestina kutokana na Mayahudi… ambaye alimrudisha mwakilishi wao akiwa amekata tamaa na kushindwa, bila kupata chochote, na akamfundisha somo la hekima, akisema: “Siwezi kupeana hata shubiri moja ya ardhi ya Palestina?, kwani sio mali yangu, bali ni mali ya Ummah wa Kiislamu. Watu wangu waliipigania ardhi hii na kuinywesha kwa damu yao… Mayahudi nawabakie na mamilioni yao, kwani ikiwa Dola ya Khilafah itasambaratika siku moja, basi hapo wanaweza kuichukua Palestina bila thamani yoyote, lakini maadamu niko hai, hilo halitafanyika…”?

Enyi Askari katika Majeshi ya Waislamu: Ikiwa mmoja wenu atasema kwamba watawala wanatuzuia kutokana na nusrah (kuiunga mkono) Palestina na viunga vyake, na kwamba hamuwezi kupigana jihad bila ya idhini yao, basi kauli yako ni hoja inayokanushwa. Kuwatii katika kuzuia jihad sio sahihi na wala hairuhusiwi, hawatokunufaisheni duniani na wala hawatakunufaisheni kesho Akhera. Ama katika ulimwengu huu, wao ni vibaraka wa wakoloni Makafiri na ni walinzi wa Mayahudi. Kuwatii wao kunajumuisha udhalilifu wenu na sio kutopigana na adui yenu, ingawa wao sio watu wa ushindi katika vita.

[وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]

Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa. [Aal-i-Imran: 111].

Ama kesho Akhera, hatma ni mbaya na adhabu ni kali zaidi:

[وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا]

Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia. [Al-Ahzab: 67]

[إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ * وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُمْ بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ]

Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao * Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni. [Al-Baqara: 166-7].

Enyi Wanajeshi katika Majeshi ya Waislamu: Kuondolewa kwa umbile la Kiyahudi ni ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kadiri wanavyoinuka na kufisidi, ndivyo watakavyopigwa na umbile lao kuangamizwa.

[فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيراً]

Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.[Al-Isra: 7].

Kila wanaporudi kwenye ufisadi na kufisidi, wanashindwa na umbile lao kuangamizwa.

[وإنْ عُدْتُمْ عُدْنَا وَجَعَلْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ حَصِيراً]

“Na mkirudia na Sisi tutarudia. Na tumeifanya Jahannamu kuwa ni gereza kwa ajili ya makafiri.” [Al-Isra: 8].

Wanaendelea katika ufisadi wao na upotovu wao, vivyo umbile lao litaangamizwa kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu. Na vile vile ni katika Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kwamba watauawa.

«لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ...»

“Kwa yakini mtapigana na Mayahudi na kwa yakini mtawauwa…” (Imepokewa na Muslim kutoka kwa Nafi’ kutoka kwa Ibn Umar). Umbile lao litatoweka na hili halina budi kutokea, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, enyi wanajeshi, hakikisheni kwamba hili liko mikononi mwenu, vyenginevyo Mwenyezi Mungu atakubadilisheni na watu wengine ambao hawatakuwa kama nyinyi.

[وَإِنْ تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُمْ]

Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi. [Muhammad: 38].

Kwa kumalizia, Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi na awajaalie makao katika Mabustani yake makubwa, na Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi na awajaalie afya njema, na Mwenyezi Mungu aubariki Ummah huu kwa kuregea kwa Khilafah yake kwa njia ya Utume, hapo utakuwa na ushindi na izza.

[وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ]

Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui. [Al-Munafiqun: 8].

H. 15 Rabi' II 1446
M. : Ijumaa, 18 Oktoba 2024

Hizb-ut-Tahrir
 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu