Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Enyi Watawala wa Nchi za Waislamu... Hamuoni Aibu?
Je, Hamuogopi Kufedheheka hapa Duniani na Adhabu Kesho Akhera? Je, Hamuelewi?
(Imetafsiriwa)

Munasikia na kuona uhalifu wa Mayahudi; wanavunja majumba juu ya vichwa vya wakaazi wake, na wanawaandama wapiganaji wa upinzani na kuwaua, chini ya ardhi na juu ya ardhi. Uhalifu wao ulianzia katika Ukanda wa Gaza, na kisha kuenea hadi Palestina yote, na bado wanaendelea. Wameua maelfu, na kujeruhi makumi ya maelfu. Kisha wakaongeza vitongoji kwenye uhalifu wao, hadi wakamfikia mkuu wa upinzani katika kitongoji, wakati wa mkutano wake na viongozi wengine. Kisha uhalifu wao ukaenea katika maeneo mapana ya Lebanon, huku jinai za Mayahudi dhidi ya watu wa Ash-Sham nazo zikiongezeka. Licha ya haya na hayo yote, hamkusanyi jeshi, si kutoka karibu wala kutoka mbali, na ilhali hakuna maumivu au madhara kutoka kwenu yanayowagusa Mayahudi! Badala yake, mfano bora miongoni mwenu ni yule anayehesabu mashahidi na kuwaita maiti ili asiumize hisia za Mayahudi! Mwenyezi Mungu awalaani! Wanawezaje kudanganywa kutoka kwenye ukweli?

Kilichowatia ujasiri Mayahudi kufanya walichofanya ni kutokuwepo kwa kizuizi kutoka kwa nchi jirani. Hakuna hata nchi moja iliyosimama dhidi yao! Kwa hakika, Iran, ambayo ilianzisha Hizb yake nchini Lebanon, iliiacha wakati mashambulizi kwenye kitongoji hicho yalipopamba moto. Haikutuma ndege zake, droni, au makombora kuilinda, na kuokoa kitongoji kutokana na uharibifu! Ama nchi nyingine jirani, zinazoizunguka Palestina na zisizoizunguka...kama Misri, Saudi Arabia, Jordan, Iraq, Syria, Uturuki... na kadhalika, ni kana kwamba jambo hilo haliwahusu. Wanafuatilia jeshi lao kutoka kushoto na kulia, kwa hofu ya kuhamasika. Kwa kweli, ikiwa watu watasonga kwa matembezi au maandamano, na hotuba ya kutaka majeshi yakusanye itatoka kwao, watawala huona hilo kuwa ni uvunjaji sheria na kuwakamata! Ama nchi zisizo karibu zinashangilia kwa sababu hazipo karibu!!

[أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ]

Tazama uovu wa wanavyohukumu!” [Surah An-Nahl: 59]

Enyi Waislamu: Mayahudi si watu wa kupigana, kwani Al-Qawi Al-Aziz anasema:

[لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]

Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa. [Surah Al-i-Imran: 111] Hawataweza kusimama ila kwa kamba kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kamba ya watu:

[ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِنَ اللهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ]

Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. [Surah Al-i-Imran: 112] Kamba yao kwa Mwenyezi Mungu imekatika tangu walipowaasi Mitume wao (as), na kinachobakia kwao ni kamba ya watu. Uingereza na vibaraka wake walikuwa kamba yao, wakati umbile la Kiyahudi lilipoanzishwa. Sasa Amerika na vibaraka wake kutoka kwa watawala katika nchi za Waislamu ndio kamba yao mpya. Watawala vibaraka ndio sehemu yenye ushawishi mkubwa katika kuzuia majeshi yasipigane na Mayahudi, katika utekelezaji wa amri za wakoloni makafiri, na katika kunyoosha kamba hii, kuwaunga mkono Mayahudi na kuhifadhi umoja wao. Kamba hii haitakatwa ila kwa vita vinavyoongozwa na kiongozi mkweli na mwenye ikhlasi, ambaye atawatawanya kutoka nyuma yao, na kutimiza kauli ya Mtume (saw): Muslim ameipokea katika Sahih yake... kwa idhini ya Nafi' kutoka kwa Ibn Umar kutoka kwa Mtume (saw), ambaye alisema:

«لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ..»

“Mtapigana na Mayahudi na Mtawaua ...”

Enyi askari katika ardhi za Waislamu: Je, hakuna miongoni mwenu mwenye hekima? Ambaye anawaongoza askari, hasa kutoka katika nchi ya Misri (Kinanah), Ash-Sham na ardhi ya Al-Fatih, ili majeshi yaliyosalia yamfuate, yakiimba Allahu Akbar, ili Ummah ufuate Takbira hizo nyuma yao kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt)?

[إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi [Ghafir: 51] Inatosha sasa, enyi majeshi! Hakuna udhuru uliobakia kwa wenye kuomba radhi wala hoja yoyote kwa mwenye kulaani. Haitoshi kwenu kusaga meno yenu kwa hasira kwa adui yenu, pasi na kufanya chochote. Badala yake, fuateni maneno ya Mwenyezi Mungu Al- Aziz Al- Hakeem (Mwenye nguvu, Mwenye hekima):

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [Surah At-Tawbah: 14]

Basi enukeni, enyi askari, muwanusuru ndugu zenu. Mnusuruni Mwenyezi Mungu (swt) na Yeye atakunusuruni:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ * وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْساً لَهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ * ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنْزَلَ اللهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ]

Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu * Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao * Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.[Surah Muhammad: 7-9]

H. 26 Rabi' I 1446
M. : Jumapili, 29 Septemba 2024

Hizb-ut-Tahrir
 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu