Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Udanganyifu wa Chaguo: Kwa nini Upigaji Kura katika Mfumo wa Kisekula Unawabwaga Waislamu

(Imetafsiriwa)

Kila baada ya miaka minne, uchaguzi unapokaribia, shauku kubwa ya kupiga kura hufurika kwenye vyombo vya habari, washawishi wa mitandao ya kijamii na mashirika mbalimbali. Waislamu pia wanahimizwa kushiriki, mara nyingi kupitia mashirika ya Kiislamu ya ndani. Kwa zaidi ya miongo miwili, wamehimizwa kupigia kura vyama maalum au watu binafsi, wakitumaini kupata manufaa au kuzuia madhara. Mnamo 2000, Waislamu walihimizwa kumpigia kura George W. Bush, ambaye alianzisha Vita dhidi ya Ugaidi, na kuharibu ardhi za Waislamu na kusababisha vifo vya Waislamu karibu milioni 1. Mnamo 2008, Waislamu walimuunga mkono Barack Obama, wakitarajia mabadiliko chanya. Badala yake, Obama alipanua programu za uchunguzi na utegaji za FBI zinazolenga Waislamu nchini Marekani na kuunga mkono madikteta kama Al-Sisi nchini Misri, na kuchochea zaidi migogoro katika Mashariki ya Kati. Mnamo 2020, Waislamu walimpigia kura Joe Biden, ambaye ameunga mkono na kufadhili mauaji ya halaiki huko Gaza huku akiendeleza ajenda ya LGBTQ ndani ya nchi. Hata maandamano ya amani dhidi ya mauaji ya halaiki ya wanafunzi wa asili zote yalikandamizwa kwa usaidizi kutoka kwa Chama cha Kidemokrasia, huku Wana republican wakihimiza ukandamizaji zaidi.

Matukio ya Gaza yanafichua uhalisia wa mfumo wa sasa wa dunia. Mauaji ya halaiki huko, yakiungwa mkono na mataifa yenye nguvu, yanaonyesha jinsi mifumo ya “kidemokrasia” inavyoweza kusaidia ukandamizaji. Uhuru wa maoni huadhimishwa pale tu unapounga mkono mfumo uliopo. Mienendo ya kihistoria inafichua kwamba, bila kujali chaguo la watu wengi, maamuzi mara nyingi yanaegemea maslahi ya kipote cha tawala, na ahadi za uchaguzi zinazotishia maslahi hayo hutupwa mbali haraka. Wananchi wamesalia na mfumo unaodhibitiwa unaowanufaisha wenye nguvu huku ukiweka kando mabadiliko ya kweli.

Sauti za Waislamu, hata hivyo, zina umuhimu kwa watoa maamuzi wa kisekula, lakini hasa kuwaoanisha Waislamu katika usekula, na kuwataka kuacha maadili ya Kiislamu kwa ajili ya kuoanishwa. Mbinu hii inalenga kufuta kitambulisho cha kipekee cha jamii ya Kiislamu, na kuwataka Waislamu kushiriki katika mfumo wa kisiasa wa kisekula ambao hatimaye unahujumu kanuni za Kiislamu.

Wengine wanapendekeza kuwapigia kura wagombea huru ili kuvuruga mfumo wa vyama viwili, wakidhani kuwa inaweza kuwapa Waislamu nguvu. Walakini, uhalisia wa nani anayedhibiti mfumo unabaki. Upigaji kura kwa wagombea huru hutoa tu udanganyifu wa ushawishi katika muundo ulioundwa ili kudumisha mamlaka ya vyama viwili vikuu. Kwa mfano, licha ya mifumo ya vyama vingi vya Ulaya, Waislamu huko wanakabiliwa na sheria kali dhidi ya Uislamu. Mienendo ile ile ya utawala inabakia, bila kujali idadi ya vyama, ikithibitisha Hadith ya Mtume (saw): «لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ» “Muumini hang’atwi mara mbili kutoka kwenye shimo moja.” (Al-Bukhari na Muslim).

Waislamu mara nyingi huuliza, “Ikiwa hatutapiga kura, je, tunapaswa kutokuwa wachangamfu kisiasa?” Kinyume chake, Uislamu unawaamuru Waislamu kushiriki kikamilifu na kuendeleza uadilifu ndani ya jamii. Mwenyezi Mungu asema,

[ادْعُ إِلَى سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ]

“Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora.” (Quran, Surah An-Nahl, Ayah 125). Mtume (saw) akasema zaidi, «مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلْسَلَ فَبِيْسْتَعْ فَعَسْتَعْ فَهُمْ فَعَسْتَعْ فَبِيْسِفَ فَإِنْ فَبِقَلْبِهِ وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ» “Mwenye kuona uovu miongoni mwenu, na aubadilishe kwa mkono wake; ikiwa hawezi, basi kwa ulimi wake; ikiwa hawezi, basi kwa moyo wake, na hiyo ndiyo imani dhaifu zaidi.” (Sahih Muslim). Uanaharakati wa kisiasa wa Kiislamu hauhitaji ushiriki katika upigaji kura wa kisekula bali ni ushiriki wa vitendo kupitia kuamrisha mema na kukataza maovu.

Kushiriki lazima kuegemee kwenye Aqidah na kuwiana na hukmu za Kiislamu. Upigaji kura katika mifumo inayotunga sheria kinyume na mwongozo wa Mwenyezi Mungu ni haramu, kwani inaidhinisha sheria zilizotungwa na mwanadamu juu ya sheria za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema,

[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْمًا لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ]

“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” (Quran, Surah Al-Ma’idah, Ayah 50). Uchaguzi wa urais na bunge, ambapo wagombea huidhinisha sheria kinyume na Uislamu, wanalegeza msimamo kwa kanuni za Kiislamu, na kuunga mkono mfumo wa utawala usio wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu anaonya,

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ]

“Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” (Quran, Surah Al-Ma’idah, Ayah 44).

Njia bora zaidi kuelekea mbele inaakisi njia ya Mtume Muhammad (saw) na Maswahaba zake, ambao hawakulegeza msimamo kwa maadili ya Kiislamu kwa ajili ya mapato ya muda mfupi. Mwenyezi Mungu ameamuru,

[لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ]

“Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” (Quran, Surah Al-Ahzab, Ayah 21). Mwongozo huu unawataka Waislamu kuunda Kitambulisho cha kisiasa cha Kiislamu kinachowiana na kanuni za Mwenyezi Mungu.

Jamii ya Kiislamu ina majukumu muhimu, ndani na kimataifa. Ndani ya nchi, Waislamu wanapaswa kuunda majukwaa yao ya kisiasa, si kwa madhumuni ya kupiga kura, bali kuimarisha kitambulisho cha Kiislamu, kujenga mafungamano ya jamii, na kushiriki katika dawah. Kwa kushughulikia masuala ya kijamii kama vile ukosefu wa makao, mwanya wa kiuchumi, na maadili ya kifamilia, Waislamu wanaweza kuonyesha masuluhisho ya Uislamu kwa matatizo ya kijamii, wakiyawasilisha kama jibu kwa changamoto za kisasa. Uwepo imara wa Waislamu, katika jamii na kwenye mitandao ya kijamii, unaweza kushajiisha kutafakari juu ya hekima ya mafundisho ya Kiislamu.

Ulimwenguni kote, Umma wa Kiislamu lazima ushirikiane ili kuregesha umoja na mamlaka, kuondoa ufisadi, na kufukuza ushawishi wa kikoloni. Ruwaza hii inayoegemezwa katika mfumo wa Kiislamu, inalenga kuondosha tawala za kidhalimu na kusimamisha utawala wa uadilifu na huruma wa Uislamu kupitia Khilafah. Mtume (saw) alibashiri maregeo hayo, akasema: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo  Khilafah kwa njia ya utume.” (Musnad Ahmad). Kusimamishwa tena kwa Khilafah kunaahidi kuhuisha uadilifu na amani, kutekeleza maneno ya Mwenyezi Mungu.

[وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ]

“Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” (Quran, Surah 21:107).

Kwa kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu, Waislamu wamefaradhishwa kufanya kazi kuelekea ruwaza hii, wakiungana chini ya bendera ya Uislamu kuongoza jamii kwa huruma na uadilifu. Mwenyezi Mungu anakumbusha,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” (Quran, Surah Al-Anfal, Ayah 24).

H. 22 Rabi' II 1446
M. : Ijumaa, 25 Oktoba 2024

Hizb-ut-Tahrir
Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu