Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali

Siasa ya Kivitendo ya Marekani Juu ya Urusi Na China

(Imetafsiriwa)

Swali:

Ametangaza Rais wa Marekani Obama katika tarehe 29/12/2016 ambapo ni wiki tatu kabla ya kuondoka kwake (madarakani), mfulululizo wa adhabu kali dhidi ya Urusi zenye kujumuisha kufukuzwa kutoka Marekani kwa idadi kubwa ya wanadiplomasia wa Urusi “ambao ni 35” na kufungwa kwa balozi/majumba ya wanadiplomasia wa Urusi huko Maryland na New York kwa kisingizio cha ujasusi… Hali yote hii tete inatokana na tuhuma za Marekani dhidi ya Urusi juu ya udukuzi wa kielektroniki katika uchaguzi wa Marekani…Je, jambo hili ndilo lililolazimisha hatua zote hizi? Au kuna sababu nyenginezo na hasa kwa kuwa Trump anatangaza kuboresha uhusiano na Urusi wakati ambapo Obama anauchafua! WajazakMwenyezi Munguu Khayraa.

Jibu:

Ili jawabu liwe wazi, na tuchunguze waqia iliyotokea kisha tuchunguze maswali yaliyoulizwa.

Kwanza: Ama uhalisia uliotokea ni sahihi; kwamba uongozi wa Marekani uliopo hivi sasa unatekeleza kivitendo kuchafua mahusiano ya Marekani na Urusi, na Urusi imefahamu ujumbe huu, ikawa majibu yake ya haraka kupitia msemaji wa Kremlin, Peskov kwamba “Adhabu za Marekani zina mwelekeo wa uvunjifu na uadui na si zakutegemea." Na akaendelea “Uongozi wa Obama unavunja mahusiano ya Urusi na Marekani kwa kuyamaliza baada ya kuwa tayari yamefikia hatua ya chini. Na akatangaza kwamba “Moscow itarejesha majibu muwafaka dhidi ya hatua za Marekani…” (Russia Today na French Channel, 29/12/2016). Na katika kuchafua mahusiano hayo, hatua za Marekani zilikuwa kama ifuatavyo:

1. Rais wa Marekani Barak Obama amesema tarehe 15/12/2016 kwamba “Marekani italipiza dhidi ya udukuzi wa Urusi kuathiri uchaguzi wa Marekani. Na Obama akaeleza katika idhaa ya “NPR” “Naamini kwamba hapana shaka ikiwa serikali yoyote ya kigeni inajaribu kuathiri kiwango kizuri cha uchaguzi wetu, sisi tuna haja ya kuchukua hatua.” Akaongeza: “Na sisi tutajibu katika wakati na pahala tunamomuchagua”. Na akaendelea “Baadhi (ya hayo malipizo) yatakua wazi na dhahiri. Na baadhi si hivyo…” (French 24, 16/12/2016). Na haya ndio majibu ya Marekani yamedhihiri katika adhabu alizozitangaza Obama dhidi ya Urusi.

2. Rais wa Marekani Obama ameishambulia Urusi kwa dhihaka na akaieleza kwamba Urusi ni “Dola ndogo”. Na akasema “Wao ni wadogo na madhaifu, uchumi wao hauzalishi kitu kinachohitajika na wengine, mapato yake (Urusi ya mauzo hayatokani na chochote) isipokuwa mafuta, gesi, na silaha, na wala haiendelei…” (Russia Today, 17/12/2016)

3. Wizara ya hazina ya Marekani imetangaza tarehe 20/12/2016 kuweka vikwazo vipya dhidi ya wafanyabiashara saba wa Kirusi na mashirika manane ikiwa ni hatua ya kupinga Urusi kuichukua Crimea na mapambano yanayoendelea huko Ukraine. Haya ni kwa mujibu wa maelezo ya Wakala wa Habari “Reuters” …Na vikwazo hivi vinawalenga watu saba miongoni mwao ni makada kadhaa wa “Benki ya Urusi” ambayo huchukuliwa kwamba ipo karibu zaidi na mamlaka za Urusi, vile vile mashirika manne ya ujenzi na usafirishaji yanayofanya kazi Crimea iliyochukuliwa na Moscow… Na ukaongeza uongozi wa Marekani kwamba hatua hizi “Zinathibitisha kupinga ukoloni wa Urusi kwa Crimea, na kupinga kutambua jaribio la kuichukua rasmi…” (Dot Misr, 20/12/2016)

4. Mchezo wa Kimarekani wa kurejea kwa barnamiji ya vita vya nyota/sayari kulipiza dhidi ya kuendelea kwa Urusi kukuza silaha zake za nyuklia. Na katika muktadha huu sheria za Marekani zimebadilishwa ili kuruhusu kuongoza nguvu za kijeshi katika anga (hapana budi hapa kuonyesha kwamba baraza la Congress la Marekani limeingiza marekebisho mawili muhimu katika kielelezo cha kanuni wakati wa hatua ya kuithibitisha. Moja kati ya hayo yanafuta Washington kutuma kwa kiwango maalum cha missile shield. Wakati ya pili yanapelekea kuanzishwa kwa kazi ya kusaniisha imara vijengwa vipya katika mfumo huu kwa matayarisho ya kuutuma angani hapo mbeleni. Na gazeti la “Los Angeles Times” limemnukuu Trent Franks, mwanachama wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama cha Republican, na ni mkubwa katika walioleta marekebisho haya mawili, kukubali kwake kwamba hayo (marekebisho mawili) yanategemea mpango wa “Ari ya Kinga ya Kimkakati” uliozinduliwa na Rais Ronald Reagan katika mwaka 1983 na unajulikana vile vile kwa jina la “Vita vya Nyota/Sayari” …(Tovuti ya Dar el-Ikhbar, 24/12/2016). Na kinacholengwa ni (kuongeza) hali tete na Urusi.

5. Baraza la Wawakilishi la Marekani jana Ijumaa, 02/12/2016 limeridhia muswada wa sheria kuipa Wizara ya ulinzi ya Marekani dola bilioni 3.4 katika mwaka 2017 ili “kuizuia Urusi” na walioukubali ni 390 katika Baraza la Wawakilishi, walioupinga ni 30 tu mswada huu wa sheria. Na waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter alikuwa ameshatangaza wakati wa kuwasilisha kwa Congress muswada wa bajeti ya ulinzi kwamba Marekani inaongeza nguvu maeneo yake katika Ulaya kwa ajili ya washirika wake ndani ya NATO ili kukabiliana na uadui wa Urusi…” (Sputnik Russian Agency, 03/12/2016)

6. Na zaidi ya hayo, Marekani imeishusha hadhi ya Urusi katika kutatua mzozo wa Syria ikaifanya kuwa uwili wa Kerry – Lavrov ambao Moscow inaufurahia sana, na inautizama kama ni ishara ya kurejea ukubwa wa Urusi (Pia) ikaubadilisha na kuwa uwili wa Urusi – Uturuki. Na Marekani ijapokuwa ina mawasiliano ya kuendelea na msaada wa kuendelea juu ya juhudi za Urusi – Uturuki nchini Syria kulinda ushawishi wa pande (husika) kwa ajili ya kadhia zake nchini Syria. Isipokuwa muktadha wa Urusi – Uturuki badala ya Urusi – Marekani huzingatiwa ni kuishusha hadhi Urusi kimataifa na kuiweka katika hadhi ya dola kama Uturuki. Na hili yawezekana kuliona katika duru ya mbinu ya Marekani dhidi ya Urusi.

7. Hali hii ya kuongezeka kwa hali tete kwa hakika imeitisha Urusi. Basi katika majibu yake dhidi ya adhabu za Marekani alizoweka Obama, rais was Urusi alisema “Hakika Moscow inahifadhi haki yake ya majibu dhidi ya adhabu mpya za Marekani dhidi yake lakini haitoelemea katika kiwango cha uongozi wa Marekani wa sasa na wala haitolenga wanadiplomasia…" Na akaongeza kwa kusema: “Hatutowapa matatizo wanadiplomasia wa Marekani, wala hatutomfukuza yeyote. Na wala hatutomzuia mtu yeyote wa familia yao na watoto wao kutumia sehemu za umma walizozizoea katika sherehe za mwaka mpya. Zaidi ya hayo tunawaalika watoto wa wanadiplomasia wa Kimarekani wanaotambulika nchini Urusi kuhudhuria sherehe za mwaka mpya miladiya Kremlin…” (Russia Today, 30/12/2016). Na Moscow kutotoa majibu ya maana ya kutarajiwa, ambayo ni majibu mfano wake, kuna maana mbili:

Ya Kwanza: Khofu kubwa iliyonayo Moscow juu ya malengo na matokeo ya mzozo huu wake na Washington.

Ya Pili: Moscow inapiga hisabu kukabidhiwa uongozi mpya wa Trump Washington ili kurejesha muundo wa mahusiano ya nchi mbili juu ya misingi ambayo Moscow itairidhia. Na kwa kutokana Urusi ilivyo dhaifu kimtazamo wa kisiasa, inadhani kuwa Rais ajae, Trump atakua tofauti na Obama aliyemtangualia katika kuitazama Urusi, wakiwa wameghafilika kwamba asasi kubwa za uongozi nchini Marekani zote humuongoza Rais yeyote yule na kutoka chama chochote kile ili kuendelea katika kutekeleza siasa ya nje ya nchi yake. Na kwamba tofauti baina ya Obama na Trump ikitokezea hukusudiwa kutekeleza siasa ya Marekani iliyopangwa.

Pili: Kuchunguza yaliyojitokeza katika swali lililoulizwa:

1. Hakika adhabu hizi nzito kutoka uongozi wa Obama dhidi ya Urusi zinakuja katika hali ya Marekani kuridhika na uthabiti wa dori (jukumu) ya Urusi katika kutekeleza jukumu la kimataifa nchini Syria na Urusi itatekeleza jukumu hili kwa sura timilifu. Marekani imekamilisha kuihusisha Urusi katika (mzozo wa) Syria kwa kiasi ambacho haiwezekani kwa Urusi kutoka katika dimbwi la Syria. Na Marekani ilipokinai hilo ikaishusha hadhi ya Urusi ili iwe Serikali ya Uturuki ni wakala mshirika wake katika (mzozo wa) Syria badala ya kuwa serikali ya Marekani yenyewe… Yote hayo, kuzorota kwa mahusiano Marekani na Urusi na kuzidi mbinu dhidi yake hakuhusiani na mas-ala ya Syria. Basi Urusi inatekeleza kwa ithibati maslahi ya Marekani nchini Syria, na hili katu halina shaka kwa Marekani, bali hakika siasa ya Urusi nchini Syria imekuwa mtego kwa wafuasi wa Marekani – Irani na makundi yake, serikali ya Syria na Uturuki na wapinzani wenye kuelemea kwake – na haiwezi kutafuta siasa yake peke yake, na haiwezi kujitoa na kuiwacha Syria kwa jambo lisilojulikana. Na kwa ajili hiyo basi, inaimarisha na kutanua kambi zake za kijeshi Latakia na Tartous…Na haiwezi pia kudhibiti hali ya vita kwa kukosa wanajeshi wa ardhini iliowatayarisha hasa nchini Syria. Yote haya yanamaanisha dori ya Urusi nchini Syria imekuwa thabiti, bali imefungwa na siasa ya Marekani na wafuasi wake, wadau katika mzozo wa Syria… Na kwasababu hii basi, uzorotefu huu si kwa sababu ya Urusi kujiweka mbali na dori iliyopangwa kwa ajili yake na Marekani katika Syria, kwa sababu haijajivua dori yake iliyopangiwa na Marekani. 

2. Na haifai mtu kufikiri kwamba vikwazo vya Marekani vilivyotangazwa na Rais Obama ni malipizo ya hasira dhidi ya udukuzi wa kielektroniki ambao huenda umechangia kushindwa chama cha Democrat na mgombea wake wa urais, Hillary Clinton. Hii ni kwasababu ingelikuwa hivyo, basi utawala wa Obama ungeliharakisha jambo hili la vikwazo kabla ya Baraza la Uchaguzi (Electoral College) halijathibitisha kuchaguliwa Trump kuwa Rais rasmi wa Marekani tarehe 19/12/2016… Ama kuianzisha kadhia hii baada ya kufuzu Rais mteule na kuthibitishwa na asasi za katiba kwao, hili hutia shaka sana uhalali wa uchaguzi huu na pia uhalali wa Rais ajae, na hili, muda wa kwamba hakuna idara yoyote ya Marekani iliyokubali kushiriki (katika jambo hili)… Na lau tutajaalia kujadili kwamba, kuna hali zilizozuia kuwekwa vikwazo kabla ya kuthibitisha matokeo, basi yanayopelekea fahamu ya kisiasa ya madola makubwa (huwa) kama hawakulazimika kutangaza matokeo baada ya kuthibitika matokeo ya ushindi wa Rais, yatazaa dharura nyengine na sio udukuzi ili kuepuka kutiliwa mashaka ushindi wa Rais ajae. Na kwa kua vikwazo vimewekwa baada ya kuthibitisha rasmi ushindi wa Rais kwa hoja ya Urusi kujiingiza katika uchaguzi kwahiyo hii huwa si sababu ya kweli.

3. Na huenda ikasemwa kwamba maendeleo ya Urusi ya silaha zake za nyuklia na makombora ya mashambulizi (offensive missile) ndio sababu ya mbinu ya Marekani hivi sasa ndio majibu dhidi ya kauli za Rais wa Urusi. (Na kasema Rais Putin kauli yake katika mkutano na uongozi wa wizara ya ulinzi katika mji mkuu Moscow: “Ni wajibu kuinua ufanisi wa nguvu za kistretejia za kinyuklia (nuclear strategic forces) uwe katika kiwango kipya cha aina yake, kitakachoruhusu kuikabili hatari yoyote ya kijeshi itakayoitishia Urusi…” (Anatolia website, 22/12/2016).

 Jambo hili likiwa na athari kiasi kidogo cha uchumi wa Urusi kinaifanya juhudi ya Moscow upande huu kuwa si ya dhati. Haya ni baada ya kufaulu Marekani na magharibi kijumla kuua nguzo kuu za viwanda vya Urusi baada ya kuvunjika kwa Umoja wa Kisovieti, Urusi ikawa nchi yenye kusafirisha nje mali ghafi ijapokuwa imebakiwa na kiasi kikubwa cha viwanda vyake vya kijeshi, yaani Urusi haina juhudi za kushindana na Marekani kimataifa bali inaihitaji Marekani kuikubali dori ya Urusi katika siasa za kimataifa, mahitaji ambayo Marekani inayakataa yote kijumla. Hata Urusi inavyoitumikia Marekani Syria haijatosha kwa Marekani kuitambua Urusi kuwa ni dola kubwa na kuishirikisha katika kadhia nyengine za kimataifa, yaani (kuwa) Urusi ambayo imerithi Umoja wa Kisovieti na ikarithi kurasa kutoka katika historia ya makubaliano ya Marekani – Sovieti, ilikua inataraji kwamba ushirikiano wake na Marekani katika Syria utapelekea makubaliano kamili na ikawa inaiomba Marekani kushirikiana katika uwanja wa kimataifa. Na haya ikiwa yanaonesha dalili (ya matumaini) yoyote, basi yaonesha kasoro ya mtazamo wa kisiasa wa Urusi. Marekani imezichanachana kurasa za makubaliano na Umoja wa Kisovieti tangu wakati ilipokua (Sovieti) kuwepo kwake kulikua na athari yenye kuhisika ulimwenguni, vipi hivi sasa (Marekani) ikubali jambo hilo na dola ndogo – Urusi, kama alivyoielezea Obama?! Na Urusi kwa udogo huu mpya haiwakilishi utisho hasa kwa Marekani kuingia katika mvutano huu. Na yote haya yanamaanisha kwamba kauli za Urusi juu ya maendeleo ya silaha za nyuklia sio sababu ya uhakika ya Obama kuzorotesha mahusiano na Urusi.

Tatu: Hivi ndivyo ilivyo sio hali zilizotangulia kutajwa ni sababu za kweli za uzorotefu huu, bali ni jambo jengine na inawezekana kulifahamu kwa kuzingatia mambo yafuatayo:

1. Inawezekana kwa mwanasiasa yeyote na kwa wepesi kabisa kufahamu mtanziko wa kimataifa wa kimsingi unaoikabili Marekani leo ni kuinuka kwa China na kuweza kujenga uchumi mkubwa ambao unaweza kihalisi kutishia uchumi wa Marekani ulio wa aina ya kipekee duniani. Na zaidi ya hayo ni matumizi ya kijeshi ya China yanayoshika kasi ambayo yanapita matumizi nchi kama Urusi, Uingereza na Ufaransa kwa pamoja. Pia programu zake nyingi za kijeshi za kisiri. Kwa hiyo China imekua ni jambo lenye kuwashughulisha wanasiasa wa Marekani. Na kauli zote za maofisa wa Marekani hivi karibuni zimeelekezwa upande huu. Waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter ameeleza kwamba China imeinua uwezekano wa kuzidisha nguvu za kijeshi, na akasema kuwa Marekani ipo katika kipindi cha mpito… (Washington– “DPA”: Kasema waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter katika kongamano la ulinzi jimboni California “Baada ya miaka 14 ya kupambana na waasi na kupambana na ugaidi… sisi tupo katikati ya kipindi cha mpito kimkakati ili kujibu changamoto za kiusalama ambazo zitazingatia mustakbali wetu. Na akasema Carter “China kutengeneza ardhi kwa kufukia bahari katika bahari ya China ya kusini (south China sea) kumenyanyua uwezekano wa kuongeza nguvu za kijeshi na hatari kubwa kutokana na makadirio mabaya...” (Al-Quds Al-Arabi, 08/11/2015). Na Rais Obama ana amini kwamba mustakabali wa Marekani una amuliwa leo katika Asia. Kasema Rais Barack Obama wa Marekani kuwa kampeni yake ya kurejesha uwiano ya siasa ya nje ya Marekani ili ishughulike kwa kiasi kikubwa Asia sio “uzushi wa kupita” wa urais wake… (Vientiane, Reuters. Siku ya saba, 06/09/2016). Na kusisitiza kwake Asia maana yake ni kukabiliana na China.

2. Imetangulia huko nyuma Marekani, katika kipindi cha Muungano wa Kisovieti kwamba kulikuwa kuna ukaribu baina ya China na Muungano kwasababu ya umoja wa chama cha kikomunisti, na ilivyokuwa Marekani wakati ule infanya kazi kidhati kuushinda Muungano wa Kisoveti, ikauchukulia kidhati ukaribu wake na China. Na ikawa inakwenda mbio kutenganisha ukaribu huu (wa Muunngano wa Kisovieti na China) na kuwa ni hatua ya kidharura ili kudhofisha Muungano wa Kisovieti na kuushinda. Na mpango wa Kissinger ukadhihiri katika wakati wake wa kuharibu mahusiano baina ya China na Muungano wa Kisovieti na alifaulu kiasi kikubwa kwa hilo… Lakini sasa hali halisi imebadilika, Marekani inahofu nguvu za China na inaona ukaribifu wake na Urusi kwahiyo inataka kuutenganisha ukaribu huu kama hatua ya kidharura ili kuiweka mbali China na kuidhoofisha, kama ilivyofanya hapo nyuma ila sasa ni kwa njia tofauti na haya ndio yaliyobainishwa na gazeti la Washington Post. Likayanukuu haya Russia Today 18/12/2016 ifuatavyo: (Na iliandikwa katika makala kuwa kabla ya mwaka 45 Rais wa Marekani Nixon alijaribu kubadilisha muundo wa “pembe tatu” Muungano wa Sovieti – Marekani – China kwa kuweka rehani kuharibu maendeleo ya mahusiano na Beijing. Na katika tarehe 04/02/1972 Nixon akafanya mkutano na mshauri wake wa mambo ya usalama wa taifa wa wakati huo, Kissinger, ili kujadili ziara yake “Nixon” ijayo kuelekea China. Kissinger akasema kumwambia Rais Nixon katika mkutano huu kwamba “Wachina ni hatari sawa sawa kama Warusi na kihistoria ni hatari zaidi kuliko Warusi” Akamwambia zaidi Rais Nixon kwamba baada ya miaka 20 “Rais wa Marekani ajae akiwa mwenye hekima kama ninyi, atategemea Urusi katika siasa yake dhidi ya Wachina”

3. Kwa haya, inawezekana kufahamu vikwazo vya karibuni vya Marekani dhidi ya Urusi, pia shinikizo la Marekani dhidi ya Urusi linaloendelea kwa kitambo sasa. Na shinikizo hili ndilo walilonalo wanachama wengi wa Republican ndani ya Congress, yaani Rais ajae karibuni, Trump. Na zaidi pia chama cha Democrat. Shinikizo hili ndio siasa mpya dhidi ya Urusi kwa lengo la kuivuta iungane pamoja na Marekani dhidi ya China, kama kwamba Marekani inatamka , na pia ndio matamshi ya Urusi wazi wazi, ya kuwa uongozi wa Obama umevunja mahusiano ya Marekani – Urusi na kuyafikisha kuwa duni. Lakini Urusi ina fursa ya dhahabu kwa kuja Rais Trump ili kuboresha mahusiano yake na Washington! Yaani taasisi thabiti za utawala nchini Marekani kwa makusudi zinatumia muda uliobakia wa uongozi wa Obama kuharakisha hali ya mvutano na Urusi ili Urusi isiwe na njia ya uokovu na matarajio isipokuwa kwa maelewano na uongozi ujao wa Trump, uongozi ambao una amini maelewano ya kimaslahi (deal). Kwamba kuboresha mahusiano na Urusi hakupatikani ila baada ya maelewano ya kimaslahi makubwa pamoja nayo kuhusu China yenye faida. Ili kufikia jambo hili ni kwa kutumia udaku wa Rais ajae Trump wa kumheshimu Rais Putin. Na wawili hao yawezekana kuwa na itifaki kama marafiki dhidi ya China.

4. Kinachotilia nguvu hilo ni kuwa Rais ajae Trump tayari ameshazidisha uzorotefu wa mahusiano ya Marekani na China hata kabla hajashika wadhifa wake. Na anatangaza kuwa atatekeleza ahadi zake za uchaguzi kwa kuziwekea kodi kubwa bidhaa za China na kuzishajiisha kampuni za Marekani kurudi. Na hichi ni kitisho kikubwa cha kibiashara kwa China. Na akafanya haraka kufanya mawasiliano na Rais wa Taiwan katika jambo hatari kutangulizwa linaloashiria kwamba Marekani inazipekua nyaraka zake ili kuishinikiza China ikiwemo kitisho kwa Marekani kuachana na siasa “China moja” na kitisho hichi cha kisiasa ni kikubwa kwa China. Kwahiyo basi, la kwanza kati ya vipaumbele vya uongozi mpya wa Marekani ni kutibu kuinuka kwa China. Russia Today limenukuu tarehe 18/12/2016 kutoka Washington Post (Njia ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump anasema kuwa yeye anaudurusu uwezekano wa kuangalia upya siasa ya Marekani kuelekea China. Na Trump akatoa wito wa kuanzisha sera kali kuelekea Beijing kwa njia ya kauli zake na maneno yake ya simu. Na Rais mteule wa Marekani alikua ameshafanya mawasiliano ya simu na Rais wa Taiwan na ndio mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka kadhaa. Na baadae Trump akaeleza katika mahojiano na chombo cha habari cha “Fox News” cha Marekani wasiwasi wake kuhusu usahihi wa Marekani kushikamana na misingi ya siasa ya “China Moja” ambayo Marekani imeiandaa tangu ziara ya kihistoria ya Rais Nixon kuelekea nchini China, katika jambo lililopelekea Trump kuituhumu China kufanya ujanja wa kibiashara).

5. Ama vipi yatakuwa maelewano ya kimaslahi ya Trump na Urusi dhidi ya China. Hakika Marekani haipangi kwa ajili ya uchumi wa Urusi ulio dhaifu katika kukabiliana na China. Wala vilevile haiweki mipango ya kutumia thakafa ya Urusi dhidi ya China. Urusi ni nchi ambayo haina thakafa yake hasa, baada ya kuporomoka ujamaa. Na jicho la Marekani liko wazi juu ya uwezo wa kijeshi wa Urusi ambao inawezekana kwa Marekani kuuwekeza juu ya China. Mfano kuilazimisha Urusi kushirikiana dhidi ya silaha za nyuklia za Korea ya kaskazini au kushirikiana juu ya kuitishia China katika usambazaji wa nishati kutoka Urusi au kutoka Asia ya kati, au hata kushirikiana kulazimisha siasa maalumu ya uhuru wa mambo ya usafiri wa bahari katika bahari ya China. Na kushiriki Marekani kwa bidii ili kuitoa China katika visiwa… Khiyari zote hizo, bila ya kutaja pia (amabalo linawezekana) kuisukuma Urusi kukabiliana na China moja kwa moja. Yote haya kwa Urusi ni kujiua yenyewe kimataifa. Lakini (ubaya wa mambo) Urusi yaweza kujikuta yenyewe imejiingiza katika siasa hizo za Marekani ili kujikweza nafsi yake eti kuwa dola kubwa!! Na katika jambo gumu kutafakari kwa Urusi ni kuweza kuzikimbia shinikizo za Marekani na kuziweka pembeni katika kuikabili China. Urusi ni mgonjwa kwa kuwa na kasoro ya mtazamo wa kisiasa, na maradhi yake haya yamekua sugu kwahiyo haiwezi kukadiria matokeo, kama inavyodhihirisha kuwa haijali kuwa Waislamu watafanya nini kwasababu ya kujiingiza kinyama Syria. Nayo ni kwasababu ya kasoro ya muono (wa kisiasa), inawaona Waislamu kwa wafalme na marais waliopo. Haioni kwao chochote kinachoitisha. Na wala haifahamu kuwa Marekani imejizuia yenyewe kutekeleza majukumu haya Syria kwasababu inajua kilicho mbali kwa hawa marais na wafalme. Kwa hivyo, vikwazo vya Obama na mvutano huu wa makusudi ni kwa lengo la kuiweka Urusi kipembeni na kuiburuza kwa Trump “rafiki yake” na njia kuwa safi kwa makubaliano ya kimaslahi ya Trump na Urusi ili kuitenga na China, bali ni kufanya uadui dhidi ya China! Hii ndio sababu yenye nguvu ya mvutano huo ambao Obama anaukusudia katika mwisho wa utawala wake ili kumuandalia njia Trump kulifikia lengo la kisiasa la Marekani lililotajwa ambalo limewekwa na asasi za Marekani kwa ajili ya zama mpya kama inavyooneshwa na viashiria… Basi siasa ya Marekani huamuliwa na asasi na kutekelezwa na marais, (haijalishi) chochote kiwacho chama cha Rais.

6. Ama China inaelewa hatari inayoinyemelea kwa hiyo inaihadaa Urusi kwa vitega uchumi ijapokua kwa hadhari na inafanya mazoezi ya kijeshi kwa kushirikiana nayo. Na pia inapiga kura pamoja ya turufu pamoja nayo katika baraza la usalama hasa kuhusu Syria. Yote hayo kwa lengo la kuizuia Washington kuitumia dhidi yake. Lakini mtizamo wa uadui wa Urusi walionao wanasiasa wa Kichina umekita. Isipokua lugha ya maslahi mapya yanayolazimishwa na uchumi mkubwa wa China, na shida yake ya mali ghafi na raslimali ya nishati, ambavyo vyote hivyo vimejaa Urusi, hupelekea mtizamo huo wa uadui kuuficha nyuma ya pazia. Pia China inafahamu uadui wa Marekani upande wake, na si jambo la mbali kuwa yaliyotokea kwa Obama wakati wa ziara yake ya mwisho nchini China kuidhalilisha (China) ni miongoni yanayoashiria hayo (Katika ziara yake ya mwisho nchini China kama Rais wa Marekani alijikuta binafsi Rais Barack Obama akilazimika kutumia ngazi ya dharura sehemu ya mwisho ya ndege iliyomchukua kuelekea uwanja wa ndege wa Guangzhou kuhudhuria mkutano wa kilele wa G20. Hayo si kwasababu ya (dharura ya) moto au tatizo la kiufundi, bali mamlaka za China hazikumpatia ngazi maalumu kwa ajili yake ya kushuka upande wa mbele wa ndege kama ilivyo kawaida. Wachunguzi wanaona kwamba China imefanya makusudi kitendo hicho kumdhalilisha Rais wa Marekani na hilo laonyesha ukubwa wa mvutano wa mahusiano baina ya nchi mbili (hizi) zinazotofautiana katika faili na kadhia kadhaa. Tangu mwanzo wake kutangaza Marekani na Korea ya Kusini kutuma makombora ya kinga (missile shield) kwenye ardhi ya Korea ya Kusini. Vilevile msimamo wa Marekani kuhusu mzozo uliopo baina ya China na Ufilipino katika bahari ya kusini ya China, na maamuzi ya karibuni ya Marekani kulazimisha ada ya ziada juu ya malighafi ya chuma cha pua cha China…) (Aljazeerah, 05/09/2016).

7. Na katika mikinzano ya wakati, mshauri wa usalama wa taifa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani alietangulia, Kissinger, yeye leo mwenyewe ijapokua umri wake mkubwa ni bingwa wa upatanishi wa Urusi na Rais matarajiwa Trump. Na mwenyewe hufanya ziara Moscow na mikutano na Putin ili kumuelekeza upande huu, yaani upande wa ushirika na Urusi dhidi ya China. Na Urusi inalishabikia hilo ikidhania kwamba Kissinger anayapa umuhimu maslahi yake! (Amesema Dmitry Peskov, msemaji kwa vyombo vya habari wa Rais wa Urusi, kwamba Moscow inakaribisha ushiriki wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani wa zamani, Henry Kissingerkatika kurejesha mahusiano baina ya Urusi na Marekani. Na Peskov akasema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Jumane kwamba Kisssinger, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani ni mmoja kati ya wanasiasa wenye hekima nyingi, akili, na umahiri, na ana umahiri mkubwa katika mambo ya Urusi na katika kiwango cha mahusiano ya Marekani – Urusi…) (Arab Media Website, 27/12/2016) Na mwelekeo huu ndio vilevile unaooneshwa na baadhi ya vyanzo vinavyofuatilia mambo Ulaya. Russia Today tarehe 28/12/2016 limenukuu yafuatayo: (Gazeti la “Bild” la Ujerumani limeandika kwamba Kissinger anaamini kuboresha mahusiano na Urusi ni jambo la dharura akiangalia kuongezeka kwa nguvu za China. Na kwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani ni mpatanishi mwenye ujuzi na kwa kuwa yeye mwenyewe binafsi amekutana na Rais Putin, basi karibu atakuwa mpatanishi wa kuyarejesha katika hali ya kawaida mahusiano baina ya nchi mbili. Na gazeti hili la Ujerumani linasema kuwa Trump anafanya bidii kuondoa vikwazo dhidi ya Urusi “kwa kuzingatia nasaha za Henry Kissinger” na una ashiria hayo vilevile “uchambuzi uliofanywa kutokana na ombi la vyombo maalumu vya Ulaya”, unaotegemea taarifa ambazo zimepatikana kutoka katika timu ya mpito ya Rais Trump…) Yote haya yanaonesha kuwa Marekani inatekeleza siasa (yake) kivitendo dhidi ya pande mbili, Urusi na China, nguzo yake ya msingi ni kuisukuma Urusi kuitumikia katika medani ya China. Na uongozi wa Obama umeshaanza kwa kutilia mkazo hatua ya shinikizo dhidi ya Urusi, unapanga ili Rais ajae, Trump, awe ndie atakae ingia makubaliano ya kimaslahi (na Urusi). Wala Marekani haidhihirishi shaka yoyote juu ya ulazima wa Urusi kukubali shinikizo la Marekani na kuchangamka pamoja nayo dhidi ya China.

Nne: Namna hii ndio dola kubwa zinavyopambana na hata zisizokua kubwa pia katika kufanikisha maslahi yake, ijapokua kuna tofauti katika hili kulingana na tofauti za ushawishi baina ya dola hizo. Na asili wanayoshirikiana ni uovu na shari unaoonekanwa wazi (leo) ulimwenguni…

Na liumizalo ni kuwa Uislamu hauna serikali iliyoshika hatamu za mambo na kuurejesha Ulimwengu huu katika hali yake ya sawa na kueneza kheri kwenye pembe zake zote, si tu katika miji ya Uislamu bali pia pembezoni mwa miji ya Uislamu. Pamoja na hayo, Uislamu una wanaume

صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا ﴿

(waliosadikisha yale waliyomuahidi Mwenyezi Mungu, wapo ambao uhai wao umekwisha na wapo wanaosubiri, wala hawakubadili kabisa – ahadi yao) [Ahzaab: 23]

Na watairejesha Serikali ya Kiislamu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Khilafah Rashidah ambayo itabadili uwiano katika dunia kuupeleka kwenye kheri,

إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا.﴿

(Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kutimiza tu jambo lake, na hakika amejaalia Mwenyezi Mungu kila kitu kiwango maalum) [At-Talaq:3]

7 Rabiu thani,1438H                                                                                                         

Alhamisi, 05/01/2017 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 21:30

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu