Alhamisi, 02 Rajab 1446 | 2025/01/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Waislamu Lazima Wasimame Pamoja Dhidi ya Maadui wa Uislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

PESHAWAR, Pakistan - Pakistan katika mashambulizi ya nadra ya anga yalilenga maficho mengi ya washukiwa wa Taliban ya Pakistan ndani ya nchi jirani ya Afghanistan siku ya Jumanne, na kubomoa kituo cha mafunzo na kuua baadhi ya waasi, maafisa wanne wa usalama walisema. (Washington Post)

Maoni:

Enayatullah Khwarazmi, msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Taliban, alikanusha madai hayo ya Pakistan na kuchapisha kwenye X (zamani Twitter) kwamba “raia wa kawaida, wengi wao wakiwa wakimbizi wa Waziristan,” wameuawa katika shambulizi hilo la anga. Khwarazmi ameongeza kuwa “watoto kadhaa na raia wengine waliuawa shahidi na kujeruhiwa” katika shambulizi hilo.

Shambulizi hilo lilitokea wakati ambapo viongozi wa Taliban walikuwa wakiandaa mikutano pamoja na ujumbe wa ngazi ya juu wa Pakistan, kuashiria kuanza kwa maingiliano kama hayo baada ya kusimama kwa mwaka mzima kutokana na madai ya ugaidi, na Balozi wa Pakistan Sadiq alikuwa katika ziara ya kujenga uhusiano na aliandika kwenye ukurasa wa X. Akisema: “Nimekutana na Waziri wa Mambo ya Nje Amir Khan Muttaqi leo. Tulifanya mazungumzo mapana. Tumekubaliana kufanya kazi pamoja ili kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na pia kwa ajili ya amani na maendeleo katika kanda hii.”

Ulafi huu wa amani na maendeleo yaliyofafanuliwa na Magharibi umeupofusha uongozi wa Waislamu katika majukumu yao ya awali na matokeo yake tunashuhudia kumwagika kwa damu ya Waislamu katika kila kona ya dunia. Ikiwa upanga umetolewa kati ya ndugu, hili hutumikia maslahi ya Marekani kwa njia nyingi. Waislamu wanaonekana kutokuwa na umoja kiasi kwamba wazo la kuunganishwa linaonekana kutowezekana. Kujionyesha kwa Magharibi kama mlezi na mwokozi wa ulimwengu, mamlaka pekee yenye akili timamu na iliyosafishwa ambayo inawasimamia washenzi wa dunia, Waislamu wakiwa ndio wanaohitajika zaidi katika vizuizi vyake. Baada ya Marekani kuondoka Afghanistan, na kuunda Serikali ya Taliban, jeshi la Pakistan lilijaribu kuchukua hatua za tahadhari za kujitenga na machafuko yaliyoachwa nyuma na Marekani. Viongozi walijua vyema zaidi juu ya uwongo ambao umeishi na mazimwi ambao wameundwa kulingana na hitaji la wakati huo. Moja ya hatua hizi za ulinzi ilikuwa kuwafukuza karibu wakimbizi 800,000 wa Afghanistan kutoka Pakistan. Wengi wa hawa wameishi hapa kwa miongo kadhaa na walipaona kuwa nyumbani kwao. Wengi walizaliwa hapa.

Wanajeshi wa Pakistan wanatakiwa kukumbuka kuwa wao ni wa nchi ambayo iliundwa kwa jina la Uislamu huku watu wakiacha kila kitu nyuma ili kufikia ardhi ambayo Waislamu wote watakuwa salama. Ardhi hii haikuwa ya kabila lolote. Ufafanuzi huu ulitolewa baadaye kwamba Muislamu aliye upande wa mstari ulionyoshwa ni tofauti na Muislamu aliye upande mwingine. Hapa tunatakiwa kufuta mistari badala ya kuwaondoa watu wasioendana na utaifa. Watu wa Afghanistan na watu wa maeneo ya kikabila ya Pakistan wanaweza kuwa rasilimali kwa jeshi letu. Vita vitatu vya Anglo Afghan hadi 2021 Marekani kuondoka kutoka Afghanistan historia imeona mifano mingi ya nguvu ya watu hawa. Wana wetu katika majeshi ya Pakistan na watu wa Afghanistan wanasujudu mbele ya Mungu mmoja. Haki na majukumu yao yanatokana na Aqida ya Kiislamu, na sio juu ya utaifa. Fikra ya Kitaifa inatokana na eneo unalojitambulisha nalo, au eneo linalokupa ukubali wa kimaandishi, kwa hivyo aina yoyote ya mabadiliko ya kijiografia yanaweza kubadilisha utaifa wako. Hali ya Afghanistan, KPK na hata Balochistan inadhihirisha wazi kwamba mipaka ya Dola za Kitaifa ilishindwa kuvunja mafungamano ya karne nyingi ya ukabila. Kinyume na hayo, ukabila umejidhihirisha kuwa na nguvu zaidi kuliko fungamano la kitaifa. Kulinda ubwana na uadilifu wa kieneo kwa misingi ya maeneo yaliyoainishwa na mwanadamu hubadilisha maana ya kulinda kwa ajili ya Uislamu. Inafafanua upya madhumuni ya kupigana na askari atalazimika kupigana na yeyote ambaye mtawala wa Kirasilimali atamtaka kupigana naye na kumuua. Hata akiwa ni ndugu yake Muislamu aliyesimama upande wa pili wa mstari. Sisi kama Waislamu Ahadi yetu iko kwa Mwenyezi Mungu. Damu, upendo, ardhi na manufaa haviwezi kuchukua mamlaka. Kuna methali ya zamani “Niko dhidi ya kaka yangu. Mimi na kaka yangu dhidi ya binamu yangu. Mimi, kaka yangu, na binamu yangu dhidi ya ulimwengu.” Hivi sivyo tulivyo. Sisi ni ndugu katika Uislamu na tunapaswa kusimama kidete dhidi ya adui wa Uislamu.

Askari wa jeshi la Pakistan ni wana na ndugu zetu na tunatimiza jukumu letu kwa kuwakumbusha kufanya lao. Uaminifu na utiifu ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) pekee na kwa mtawala anayetabikisha sheria kwa mujibu wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt). Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) haitaokoa tu maisha ya Waislamu bali itawalingania wengi kwenye Uislamu na itawaletea kheri ya duniani na akhera.

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Unyonyaji Mbaya wa Bima ya Afya na Takaful

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu