Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Pakistan Inahitaji Sheria zinazotokana na Quran Tukufu na Sunnah ya Mtume, na sio Zinazotokana na wingi wa Thuluthi Mbili ya Wabunge

(Imetafsiriwa

Habari:

Allama Dkt Raghib Naeemi, mwenyekiti wa Baraza la Fikra za Kiislamu (CII), alisema mnamo Jumatatu (18/11/2024) kwamba miongoni mwa matumizi “yasiyo ya Kiislamu” ya Mitandao ya Kibinafsi (VPNs) ni kutoa kauli “dhidi ya usalama wa kitaifa” na kumchafulia mtu jina. [Dawn]

Maoni:

Haishangazi kwamba Baraza la Fikra za Kiislamu limewavunja moyo Waislamu wa Pakistan kwa mara nyengine tena. Kuwepo kwa Baraza la Fikra za Kiislamu kunatokana na katiba ambayo imejikita katika kanuni ya wingi wa thuluthi mbili ya kura za wabunge. Dori ya Baraza hilo ni ushauri tu. Mapendekezo yake hayalazimishi taasisi yoyote ya kiserikali isipokuwa mamlaka zenyewe ziamue kuyafanyia kazi. Kuhusu kuruhusiwa au kuharamishwa kwa matumizi ya VPN, Baraza halijaleta dalili za Kiislamu kutoka katika Quran Tukufu na Sunnah ya Mtume, au hata hukmu za Shariah, lilizotumia kutoa rai yake.

Ni vyema kutambua kwamba Baraza hilo linatoa ushauri pale ambapo hakuna nafasi ya kushauriana kwa sababu hukmu ya kukatikiwa ya Kiislamu (hukm qati’i) ipo, kama vile kuharamisha riba. Baraza pia limekaa kimya juu ya amri nyingi na maharamisho ya Mwenyezi Mungu (swt).

Hivyo Baraza hilo haliitishi kutabanniwa kwa Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume kama msingi wa sheria, badala ya wingi wa thuluthi mbili ya kura za wabunge. Uislamu umefafanua mamlaka ya Kiislamu (sultan) kuwa ni hukumu kwa yale yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَأَنْ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Maida 5:49]. Hata kama bunge zima lilipiga kura kuruhusu nyama ya nguruwe au kileo, haina uzito katika mtazamo wa Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) ndiye Mtungaji Sheria na Yeye Peke Yake ndiye mwenye haki ya Kutunga Sheria. Kumuhesabia mtawala kwa kupuuza kwake Uislamu sio kumchafulia jina, ni faradhi ya Shariah. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«أَلاَ إِنَّ أَفْضَلَ الْجِهَادِ كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ»

“Hakika jihadi iliyo bora zaidi ni kusema neno la haki mbele ya mtawala jeuri,” (Ahmad) na yeye (saw) akasema:

«سَـيِّدُ الشُّهَدَاءِ حَمْزَةُ بْنُ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ وَرَجُلٌ قَامَ إِلَى إِمَامٍ جَائِرٍ فَأَمَرَهُ وَنَهَاهُ فَقَتَلَهُ»

“Bwana wa mashahidi wote ni Hamza bin Abd il-Muttalib na mtu yeyote atakayesimama mbele ya mtawala jeuri, akamuamuru mema na kumkataza maovu, kisha jeuri huyo akamuua.” [Al-Haakim katika Al-Mustadrak]. Mbali na kupuuza Uislamu, watawala wa Pakistan ni vibaraka wa wakoloni, wanaodhuru usalama wa Waislamu ili kusimamisha utawala wa maslahi ya wakoloni.

Baraza hilo haliitishi kuhamasishwa kwa vikosi vya jeshi kuhusiana na ukombozi wa Kashmir na Palestina. Mwenyezi Mungu (swt) ameifanya kuwa ni faradhi ya Shariah kukomesha unyakuzi wa ardhi za Waislamu na makafirini. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“Na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah 2:191].

Baraza hilo halipingi utaratibu wa kifedha wenye msingi wa riba nchini Pakistan, ambao umekandamiza nchi na watu chini ya deni kubwa. Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha waziwazi riba. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ * فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ]

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” [Surah Al-Baqarah 2:278-279].

Hata hivyo, Baraza hilo linakwenda zaidi ya mapendekezo tu, na linatabanni sauti ya kutoa fatwa (hukmu ya Kiislamu), katika kutetea sera za watawala wanaotawala kwa hukmu na katiba ya sheria za Magharibi, ambazo zimeegemezwa juu ya msingi wa kutenganisha dini na maisha.

Pakistan inahitaji katiba, sheria na sera zinazotokana na Dini ya watu wake. Hizb ut Tahrir imetayarisha rasimu ya katiba inayotokana na Quran Tukufu na Sunnah. Ibara ya 1 inasema, “Aqeedah ya Kiislamu ndio msingi wa dola. Hii ina maana kwamba kuwepo kwa dola, muundo wake, uwajibikaji wake, na chochote kinachohusiana nayo lazima kiwe na msingi tu juu ya itikadi ya Kiislamu. Vile vile itikadi hii ndio msingi wa katiba na sheria, na hakuna chochote juu yake kitakachoruhusiwa isipokuwa kitokane na Aqida ya Kiislamu.” Hizb ut Tahrir inataja dalili za kina za Kiislamu kwa ibara hii na ibara zote 191 za rasimu ya katiba.

Hebu Waislamu wa Pakistan na washirikiane na Hizb ut Tahrir kusimamisha Uislamu katika kutawala. Hebu na wasome maelezo ya mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu na waibebe Dawah ya Uislamu. Hebu na wawatake jamaa zao na marafiki katika jeshi kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dawood Ibrahim – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu