Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vifo vya Hajj ni Kosa la Utawala wa Saudi kutokana na Ukosefu wao wa Ustawi kwa Wageni wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Zaidi ya mahujaji Waislamu 1,300 waliripotiwa kufariki wakati wa Hija ya kila mwaka, au hija ya Makka, mwezi huu nchini Saudi Arabia, ambapo halijoto imepanda zaidi ya nyuzi joto 50 (nyuzi 122 za Fahrenheit). Mfiduo usiodhibitiwa wa joto kali unaweza kusababisha aina mbalimbali za madhara ya kiafya yanayojulikana ikiwemo kufeli kwa viungo vya mwili na hata kifo. Mkazo wa joto unaaminika kusababisha vifo vingi, tukio linaloweza kuzuiliwa kabisa. Hili linaimarisha haja ya hatua madhubuti za ulinzi dhidi ya joto, haswa kwa makundi yaliyo katika hatari ya kuathiriwa na joto kama vile wazee na watu wenye ulemavu. (Human Rights Watch)

Maoni:

“Saudi Arabia imetumia mabilioni ya dolari kudhibiti umati na hatua za usalama kwa wale wanaohudhuria Hija ya kila mwaka ya siku tano, lakini idadi kubwa ya washiriki inahakikisha usalama wao kuwa mgumu.” (Chanzo) Hiki ni kisingizio duni cha miradi ya utawala wa Saudia kwa watu wake na kwa vyombo vya habari vya kimataifa; lakini udhuru huu umekataliwa kabisa kutokana na madai yao ya kuwa ni Wasimamizi wa Haramain. Lau wangekuwa na uadilifu au heshima yoyote kwa dori yao kama wasimamizi, katika zama za leo na maendeleo, masuala ya upangiliaji, urahisi na ukarimu kwa hakika yanngefikiwa na kila hujaji wa Hajj licha ya mamilioni ya watu wanaotafuta Hija. Wizara ya Hijja na Umra kila mwaka hujitayarisha kwa ajili ya msimu wa Hijja na inajua idadi na viwango vinavyowasili kutoka kila nchi duniani kote na hivyo kuwa na uwezo wa kutengeneza malazi yanayohitajika na kutoruhusu mahujaji kufariki kwa kukosa matunzo na kupata huduma ya matibabu. Wao pia wanashiriki uzito wa janga hili linaloweza kuzuilika. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَآ أَحْيَا ٱلنَّاسَ جَمِيعًا]

“Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.” [Al-Maidah 5:32].

Ukosefu wa uwajibikaji ulidhihirisha uzembe mkubwa kwa Umma wa Kiislamu ambao ulisafiri karibu na mbali, mamia ya maelfu wakiweka akiba kwa miongo kadhaa ili kumudu gharama kubwa za Hijja, inathibitisha uadui wa utawala wa Saudi dhidi ya Ummah kuufanya kufikiri mara mbili kabla ya kuanza kufanya safari za kifo. Hata hivyo habari za kushangaza ni kwamba mkuu wa Mamlaka ya Burudani ya Saudi, Turki Al-Sheikh, alitangaza kuwa Riyadh itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la Michezo ya Kielektroniki, litakalofanyika “Boulevard” na ushiriki wa timu 30 za kimataifa, kutoa zawadi kubwa zenye thamani hadi dolari milioni 60! Tuzo kubwa zaidi ya pesa katika historia!!

Kiasi kikubwa cha pesa kilichomwagwa kwa ajili ya burudani wakati baadhi ya mahujaji wanaotafuta Hija walinyimwa faradhi hii ya Kisharia kwa sababu ya kutokuwa na visa maalum na/au vibali sahihi. Kulikuwa na maelfu ya watu ambao walilazimika kuregea katika nchi zao waliopigwa marufuku kuhiji baada ya kutozwa faini kubwa na hata kufungwa jela, bila kujali umri. HRW iliripoti kuwa mahujaji ambao hawajasajiliwa waliripotiwa kunyimwa ufikiaji wa huduma za umma kama vile mahema yenye viyoyozi, vituo vya ukungu, usafiri, au maeneo ya kunywesha maji. “Asilimia 83 ya [wafu] hawakuwa na vibali, maana yake walianikwa kwenye masafa marefu na vipindi virefu chini ya jua bila vivuli…” Kwa Waislamu kunyimwa maji na makaazi katika sehemu takatifu zaidi duniani, uko wapi uwajibikaji na utu!? Abu Huraira aliripoti Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saw) akisema: «إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ... يَا ابْنَ آدَمَ اسْتَسْقَيْتُكَ فَلَمْ تَسْقِنِي‏.‏ قَالَ يَا رَبِّ كَيْفَ أَسْقِيكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ قَالَ اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلاَنٌ فَلَمْ تَسْقِهِ أَمَا إِنَّكَ لَوْ سَقَيْتَهُ وَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي‏»‏‏‏ “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu, Atasema Siku ya Kiyama: ... Ewe mwanadamu, nilikuomba uninyweshe na hukuninywesha. Atasema: Ewe Mola Mlezi, vipi nikunyweshe na hali Wewe ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote? Atasema: Mja wangu fulani alikuomba umpe maji, nawe hukumpa anywe, lau kama ungemnywesha ungelikuta hilo kwangu.” Je, hivi ndivyo wanavyopaswa kufanyiwa wageni wa Haramain!? Hawasimamii faradhi ya ustawi wa Ummah na Waislamu wamejitenga na hawa wanaoitwa “wasimamizi wa madhara.” Hakika ukoo wa Saudia si wa damu moja na Ummah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Manal Bader

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu