Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ewe, Erdogan, Je, Uadui wa Makafiri dhidi ya Uislamu kamwe ushawahi Kuisha?!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alizungumza kwenye "Mkutano Mkuu wa Wapalestina", ambao ulifanyika katika Uwanja wa Ndege wa Ataturk wa Istanbul kupinga hatua za kijeshi za 'Israel' katika Ukanda wa Gaza, TRT Haber inaripoti.

"Namshukuru kila mmoja wenu kwa kutetea kadhia ya Palestina na kutoa matumaini kwa wanyonge wa Gaza," alisema. Aliitaja Magharibi kuwa mhusika mkuu wa mzozo huo wa kijeshi, ambao hutenda, kwa maneno yake, "bila kuchafua mikono yake wenyewe," na Israel kuwa ni "kikaragosi ambacho siku moja kitatolewa kafara."

Kulingana na kiongozi huyo wa Uturuki, wale "waliomwaga machozi ya uongo kwa wale waliouawa nchini Ukraine" hawakuonyesha huruma kwa wale waliouawa Gaza. "Ewe Magharibi, nakuuliza, unataka kuchochea upya vita kati ya mwezi na msalaba?" - Erdogan alisema. (Chanzo: rbc.ru)

Maoni:

Hebu mtu yeyote na asidanganywe na ustadi wa Erdogan katika kucheza na maneno mazuri, sawa na ustadi wa wachawi ambao, kwa amri ya Firauni, walitupa kamba mbele ya Musa (as) ili kukanusha ishara za Mwenyezi Mungu. Lakini tofauti na Erdogan, wachawi walikuwa na akili na ujasiri wa kukubali wa haki. Hadi Siku ya Kiyama, watabakia kuwa kielelezo cha imani ya kweli na ustahamilivu, wakifadhilisha kifo cha uchungu katika kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu, kuliko maisha ya anasa kwenye kiti cha dhalimu asiyemcha Mungu.

Hebu mtu yeyote na asidanganywe na tuhuma kali za Erdogan dhidi ya Magharibi, akiongozwa na firauni wa zama zetu - Marekani. Je, Jamhuri ya Uturuki, inayoongozwa leo na Erdogan, sio mshirika wao? Je, hakuna kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Uturuki? Je, Uturuki, ikiwa kama mwanachama wa NATO, haikushiriki katika kuivamia Afghanistan? Na hili ni jambo ambalo liko wazi kwa kila mtu, bila kuhesabu dori ya hila ya serikali ya Uturuki katika matukio nchi Syria, Libya na nchi zingine za Kiislamu.

Akiita "Israel" kikaragosi, Erdogan ananyamaza kuwa Uturuki ilikuwa moja ya nchi za kwanza kutambua kuundwa kwake katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu na wakoloni wa Magharibi. Je, hakuna mahusiano ya kidiplomasia na ushirikiano kati ya Uturuki na umbile hili linalokalia kwa mabavu? Je, hakuna makubaliano huru ya kibiashara kati yao, yanayohusisha, kati ya mambo mengine, nyanja ya silaha na teknolojia za kijeshi, yenye mizani ya kila mwaka ya dolari bilioni kadhaa?

Akizituhumu nchi za Magharibi kwa kutaka kuchochea vita "kati ya mwezi na msalaba," Erdogan anazibadilisha fahamu, akitaka kujiondolea jukumu la mauaji ya Waislamu bila kuadhibiwa huko Palestina. Lakini je, vita hivi vya ukafiri na Uislamu, ambavyo ni vya kimfumo na sio vya baina ya imani, kama walivyokiri wanasiasa wa Marekani na Ulaya wenyewe, vimesimama hata kwa muda mfupi?

Je! Dola kubwa za Magharibi, zinazoongozwa na Marekani, hazina uadui na Waislamu, zikitangaza Uislamu kuwa ndio tishio pekee kwa upanuzi wao wa kikoloni chini ya kauli mbiu ya "kueneza demokrasia na kulinda haki za binadamu"? Je! Haziko vitani na Uislamu, zikimtukana Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kuchoma Qur’an, zikishambulia vazi la mwanamke wa Kiislamu, zikifungua "misikiti" yao ya mashoga, ambayo kwayo wazinzi wamewekwa kama Maimamu? Je! Hawakuzindua "Uislamu" wao wenyewe wa Ulaya au Amerika ambao ungelingana na itikadi yao ya uvumbuzi ya usekula?

Uko upande wa nani, Ewe Erdogan? Je! Ni kwa nini, unapozuru kaburi la mhalifu muovu Ataturk hulitemei mate, lakini, unaweka shada la maua kwa huzuni, ukiapa "kutetea urithi wake"? Je! Huu sio "urithi", ambao ni kukomesha Sharia ili kuwaridhisha Makafiri, na kuweka mahali pake sheria za ukafiri, sio ukatili mkubwa dhidi ya Ummah wa Kiislamu? Je! Kwa nini unakubali pongezi kutoka kwa maadui wa Uislamu wakati wa sikukuu ya kuanzishwa kwa jamhuri ya kisekula juu ya magofu ya Khilafah, ambapo, hata katika kipindi cha udhaifu mkubwa, ilibaki kama mtetezi mkali wa Waislamu?

Ewe Erdogan! Je! damu ya wazee, wanawake na watoto wa Gaza yenye thamani zaidi ya machozi na hotuba zako za hasira sio yenye kutikisa hewa? Je! Kwa nini basi jeshi la nchi kavu na maji la Uturuki linafanya gwaride na sio kukimbilia kuwasaidia? Je! Hujayasikia maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako?” [4:75].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mustafa Amin
Mjumbe wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu