Jumatatu, 16 Muharram 1446 | 2024/07/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Sheria za Kijamii za Kiliberali za Indonesia Zinawasaliti Wanawake wa Kiislamu kwa Uhuru Bandia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wagombea kadhaa wa ‘Miss Universe’ wa Indonesia wamesajili malalamishi kwa polisi wakiwatuhumu waandaaji kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Mmoja wa mawakili wao alisema kuwa wagombea hao waliambiwa wavue nguo zao kwa ajili ya "ukaguzi wa mwili" na picha siku mbili kabla ya fainali mnamo 3 Agosti. Waandaaji hao ilidaiwa waliwaambia wanawake "walipaswa kuchunguza makovu yoyote, uvimbe au michoro ya tattoo kwenye miili yao". "Ninahisi kwamba haki zangu zimekiukwa," mmoja wa wagombea alisema. "Imeniathiri kiakili. Nimekuwa na shida kulala," alisema, akizungumza na wanahabari, pamoja na walalamishi wengine, mapema wiki hii. Televisheni ya eneo hilo iliziba sura zao kwenye matangazo ili kulinda utambulisho wao. Mellisa Anggraeni, wakili anayewakilisha wagombea watatu ambao walilalamika, alisema wengine wengi watajitokeza. Polisi katika mji mkuu Jakarta walitoa taarifa wakisema watachunguza zaidi.

Maoni:

Ni utata kamili kutarajia kwamba mashindano yanayowafanya wanawake kuwa vyombo na kupima mafanikio yao na kushinda kwao kwa msingi wa picha ya mwili yaheshimu wanawake.

Serikali ya Indonesia tayari imeruhusu kukiuka na kuwafanya wanawake kuwa vyombo kwa kuruhusu hafla kama hizi za Haram awali ya yote kufanyika. Sera za kibepari za kuifanya miili ya wanawake kuwa kitega uchumi kwa matangazo ya biashara na madhumuni ya utangazaji soko yatavutia watu wabaya zaidi ya kusimamia hafla hizi. Umasikini na ukosefu wa fursa kwa wanawake kupata mshahara mkubwa kutoka kwa kazi zenye heshima husababisha kutapatapa kwa wanawake kuingia kwenye maonyesho haya ya udhalilishaji ambapo wanafunuliwa uchi wao mbele ya watazamaji au kupiga kura ni nani anayepokelewa kuwa "bora" kwa kujidhalilisha. Khilafah atapiga marufuku ufikiaji wa Umma kwa hafla kama hizo na kuwaadhibu wale ambao wanaokiuka heshima ya wanawake, kwani hakuna nafasi ya hili katika jamii za kweli za Kiislamu.

[وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا]

“Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu!” [4:34]. Insha’ Allah hivi karibuni tutaona binti zetu mustakabali wakitamani shakhsiya tukufu na kazi za mama yetu mpendwa wa waumini Khadija (ra) badala ya kujiunga na soko la nyama ya kijamii lililoundwa na mabepari kiliberali na washawishi wa kikoloni katika ardhi zetu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu