- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Marufuku Iyopendekezwa ya Hijab katika Shule za Denmark ni Shambulizi kwa Kitambulisho cha Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo tarehe 24 Agosti, tume inayoitwa "Tume ya mapambano ya wanawake yaliyosahaulika" iliyopewa kazi na serikali ya Denmark, ilichapisha mambo tisa ya kupambana na kile ambacho kimeanzishwa katika siasa za Denmark kama "udhibiti hasi wa kijamii". Pendekezo, lililopata mjadala mkali zaidi katika vyombo vya habari vya Denmark na kwenye mitandao ya kijamii, lilikuwa ni pendekezo la kupiga marufuku hijab za Kiislamu katika shule za msingi. Serikali ya Denmark imeibua swali kuhusu kupigwa marufuku kwa Hijab shuleni kwa miaka mingi, na makundi mengi ya watu wa Denmark yametabanni mtazamo wa hijab kama tatizo. Vyama vyote vya pande zote za kisiasa nchini Denmark vina chuki dhidi ya maadili ya Kiislamu na tamaduni za familia.
Maoni:
Sasa, huku wiki mbili zikiwa zimepita, Waislamu wengi wamejibu kwa kupinga pendekezo hili. Wahadhiri, watafiti, wataalamu, viongozi wa shule, mameya na mabaraza wamekashifu pendekezo hilo kwa sababu ya mgongano wa wazi na uhuru ambao Denmark inadai kuubeba na msingi wa maisha na jamii. Tume hiyo pia imekuwa ikikashifiwa vikali na kuchunguzwa kwa ukosefu wa utafiti nyuma ya pendekezo hilo na kwa maswala ya kibinafsi yanayosukuma mapendekezo yao.
Sio siri kwamba watu hawa wanachochewa na chuki na visasi vya kibinafsi dhidi ya Uislamu na Waislamu. Mapambano dhidi ya udhibiti hasi wa kijamii, ambayo ni mbiu yao, kivitendo ina maanisha kuwashambulia Waislamu wanaolea watoto na kujenga familia kulingana na maadili ya Kiislamu. Hii kidhati ina maanisha, kushambulia kitambulisho cha Kiislamu, kama moja ya sehemu muhimu zaidi za kuunda na kukuza kitambulisho cha Kiislamu ni kupitia malezi kulingana na maadili ya Kiislamu.
Wanachama wa tume hiyo wanarudisha nyuma misimamo yao na kujiondoa kwenye tume hiyo baada ya majibu ya Waislamu na mijadala mikali katika vyombo mbalimbali vya habari. Wanasiasa wa Denmark, miongoni mwao wakiwa chama tawala na vyama vingine vinavyoshindana, wanajitayarisha kwa uchaguzi ujao. Wagombea wote wa vyama vikuu wameelezea kuunga mkono marufuku hiyo ya hijab lakini bado hawajatoa matamshi madhubuti ambayo yanaweza kuwa kura katika bunge la Denmark. Vyovyote itakavyokuwa matokeo, ni wazi kama zamani, kwamba serikali ya Denmark ina mstari mmoja wa hatua dhidi ya Uislamu, Waislamu, matukufu yetu, na maadili. Wanashambulia, kuwatukana, na kuwapaka matope Waislamu, na wamefanya hivyo miongo mingi. Wanasoma mazingira kwa mujibu wa marufuku hiyo iliyopendekezwa. Endapo haitaonekani kuwa jambo la busara kulifuatilia kwa kipindi cha wakati huu, italetwa tena hivi karibuni, kama ilivyokuwa hapo awali. Hakuna mrengo wa kulia wala mrengo wa kushoto linapokuja suala la mitazamo na maoni dhidi ya Waislamu. Juhudi zao huungana dhidi ya Uislamu, na ndiyo maana juhudi zinazoendelea, za pamoja kutoka kwa Waislamu ni muhimu.
Ni muhimu kutoingia katika mitego ya kutumia uhuru wa kibinafsi na kile kinachoitwa haki za kiraia kama ufafanuzi wa kusisitiza juu ya hijab ya Kiislamu. Kubishana kupitia kutumia uhuru wa dini, au haki za kidemokrasia, za kiraia sio njia sahihi ya Kiislamu ya kupambana na pendekezo kama hilo, au jambo lolote hata kidogo.
Hizb ut Tahrir ilifanya maandamano mnamo tarehe 3 Septemba yenye alama ishara (hashtag) inayotafsiriwa kama "Tetea Hijab", ikiashiria kuitetea hijab ya Kiislamu, na itaendelea na kampeni inayoendelea ya kuchukua msimamo thabiti dhidi ya marufuku hii iliyopendekezwa. Tunatoa wito kwa Waislamu kusimama kidete juu ya maadili na kitambulisho cha Kiislamu, na kuungana katika kusimama kidete kwa ajili ya hijab kama jukumu la Kiislamu hasilowezi kujadiliwa.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Younes Piskorczyk