- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ukiukaji wa Makubaliano; Tabia ya Kale ya Amerika!
(Imetafsiriwa)
Habari:
Ripoti ya hivi karibuni ya Kikundi cha Utafiti cha Afghanistan (ASG), iliyo idhinishwa na Bunge la Congress la Amerika, inapendekeza utawala mpya wa Amerika kuongeza makataa ya vikosi vya Amerika kujiondoa Afghanistan, na upunguzaji mwingine wowote wa wanajeshi unapaswa kutegemea maendeleo ya mazungumzo ya amani na kupunguzwa ghasia na Taliban. Amerika haipaswi 'kuwapa ushindi Taliban,' ripoti hiyo pia ilisisitiza. Ripoti hiyo ilitengenezwa na kikundi kisicho egemea upande wowote ambacho kinasimamiwa na Joseph Dunford, mwenyekiti wa zamani wa Wakuu Wote wa Jeshi wa Amerika na Kelly Ayotte, Seneta wa zamani wa Amerika (Republican). Ripoti hiyo pia iliangazia kwamba kuondolewa kikamilifu kwa vikosi vya Amerika wakati huu kunaweza kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe, kuyumba kwa eneo na kuzuka tena kwa al-Qaeda. (BBC Kifursi)
Maoni:
Chini ya Makubaliano ya Doha, yaliyotiwa saini baina ya Amerika na Taliban, Amerika imeahidi kupunguza polepole majeshi yake kutoka Afghanistan huku ikiondoa majeshi yake yote kufikia Mei 2021. Lakini katika siku za hivi karibuni, serikali ya Amerika imekuwa ikifanya kazi bila kuchoka kuongeza uwepo wake nchini Afghanistan. Kwa upande huo, Amerika, NATO na Muungano wa Ulaya wameituhumu Taliban kwa kushindwa kutimiza ahadi zao, pamoja na kupunguza ghasia, kukata mafungamano na al-Qaeda na kushindwa kuendeleza mazungumzo ya kindani ya Afghanistan. Kwa sababu hizi, wanadai kuwa kujitoa kikamilifu kunaweza kusababisha mashambulizi kamili nchini Afghanistan, huku Taliban ikichukua serikali na kuanzisha "vita vya wenyewe kwa wenyewe" nchini humo.
Wakati huo huo, Anthony Blinken, Waziri wa Kigeni wa Amerika, katika mazungumzo ya simu na Ashraf Ghani aliunga mkono mustakabali wa kidemokrasia na utulivu wa Afghanistan, jambo ambalo Taliban hawajaelezea hadharani kujitolea kwao kikamilifu.
Tumeirudia mara nyingi, na kuisisitiza kwa wakati huu, kwamba Amerika daima imekuwa ikikiuka makubaliano na miungano mingi pamoja na wengine katika historia yake yote kwa sababu sera yake inategemea mikakati ya kiutendaji. Huku, upande mwingine, Waislamu kihistoria walishikamana na makubaliano - kwani ukiukaji wowote wa mikataba unatafsiriwa kama 'khiyana' na/au kitendo kinyume na imani ya Kiislamu. Taliban, kama kikundi cha Kiisilamu, wamejitolea kwa makubaliano hayo kwa kutii Makubaliano mengi ya Doha hadi sasa. Kwa kuwa imekuwa ni takriban mwaka mmoja tangu majeshi ya Amerika yawe salama kabisa katika kambi zao na hayakukabiliwa na tishio kubwa wakati wa kujiondoa taratibu.
Kwa upande mwengine, udhuru wa Amerika juu ya Taliban kwa kutokata mahusiano yao na al-Qaeda na kuwasaidia kufufuka katika eneo hilo ni udhuru sawa na aliokuwa akitumia mbwa mwitu kwa kondoo. Mbwa mwitu alikuwa akimlaumu kondoo kwa kusema kwamba, "Kwa nini unayasababisha maji kuwa matope?" Wakati mbwa mwitu mwenyewe alikuwa akikaa juu na kunywa maji kutoka upande wa juu wa mto. Amerika daima imekuwa ikiwabandika Waislamu kuwa al-Qaeda na 'magaidi' wale ambao wamesimama kidete dhidi ya maslahi ya Amerika, Magharibi na mfumo uliopo wa ulimwengu. Lakini, Amerika na washirika wake lazima watambue kwamba Umma wa Kiislamu kamwe hautakuwa nje ya Mujahidina na wapiganaji kupambana dhidi ya uvamizi wala Amerika wala washirika wake hawataweza kuwazuia Mujahidina kusimama dhidi ya vitendo viovu vya uvamizi huo. Kwa hivyo, udhuru huu ni sawa na udanganyifu wa ujanja wa zamani na ushawishi uliofichuliwa wa adui huyo.
Tumesisitiza pia kwamba Amerika ni dhahiri imeshindwa kijeshi nchini Afghanistan na haiwezi tena kuendelea na vita nchini Afghanistan. Kwa hivyo, inataka kugeuza kushindwa kwake kuwa 'mafanikio' kupitia ule unaoitwa mchakato wa amani, na pia inakusudia kutoka nje ya mlango na kurudi tena kupitia madirishani kwa msingi wa makubaliano yaliyofanywa pamoja na Taliban. Huku Joe Biden akichukua afisi, Amerika kwa mara nyengine tena inatoa wito wa marekebisho ya Makubaliano ya Doha, ikitumia kama visingizio vya kutoviondoa vikosi vyake kutoka Afghanistan kwa kusema kwamba Amerika haipaswi "kukabidhi ushindi kwa Taliban."
Kwa hivyo Wataliban wanapaswa kutambua kuwa Chama cha Kidemokrasia kinazingatia zaidi diplomasia kuliko vita. Utawala wa Trump ulitumia Makubaliano ya Doha kwa manufaa ya Amerika, ikitumia fursa hiyo kupunguza gharama za jeshi la Amerika pamoja na kuongoza uondoaji salama wa idadi kubwa ya majeshi yake. Sasa, chini ya pazia la diplomasia, Wanademokrasia hawatamaliza tu vita virefu zaidi katika historia ya Amerika, lakini pia watajitahidi kuimarisha misingi dhaifu ya Amerika katika eneo hilo, haswa nchini Afghanistan. Kwa hivyo, sera ya sasa ya Biden pamoja na visingizio vya Ikulu ya White House kwa Taliban kutotii Makubaliano ya Doha ni sehemu ya matukio haya.
Taliban lazima pia itambue kwamba Amerika imejifunza kwa miaka 20 iliyopita kwamba kuwashinda Taliban kwa hatua za kijeshi haiwezekani kwa sababu wapiganaji wa Taliban wana imani ya Kiislamu na azma imara ya kutekeleza 'Jihad' dhidi ya uvamizi. Lakini Amerika na Magharibi, kupitia uzoefu wao wa vikundi vya wapiganaji, haswa katika nchi za Kiislamu, wamepanga kuingia katika uwanja wa kisiasa nanyi kwa namna ile ile ili kwanza kuiburuta sehemu kubwa ya uongozi wenu kutoka katika vita hadi katika uwanja wa kisiasa na hatimaye kupata njia wazi kwenu kupitia watawala vibaraka wao na mifumo yao ya kukuondoeni hatua kwa hatua kutoka kwa uwanja wa kisiasa kupitia kukusukumeni kuzama ndani ya mchakato wa kidemokrasia.
Kwa hivyo ni lazima mkubali kwamba mumekwama kwenye uzi wa udanganyifu wa Makubaliano ya Doha kwani idara mpya ya Amerika inajaribu kulazimisha kila walichopanga kupitia mbinu anuwai za kuwashinikiza. Wakati huo huo, mojawapo ya khiari ambazo zina uwezekano ambao ulihisika kihakika hata kabla ya kutiwa saini kwa Makubaliano ya Doha ni kuendelea kwa majeshi, ujasusi na kadhalika… uwepo wa Amerika nchini Afghanistan.
Kwa hivyo Taliban haipaswi kuhadaiwa kupitia kushikamana na makubaliano ambayo Amerika itayakiuka kila inapotaka au wakati wowote inaposhindwa kupata maslahi yake. Kwa sababu Amerika na Magharibi daima wamekuwa wakiwadanganya Waislamu mmoja baada ya mwengine, na watakabiliana nanyi na kusonga mbele kwa njia ile ile ya vikundi vyote vya Kiislamu. Beijing, wala Moscow, wala Tehran hawataweza kuwasaidia katika njia hii kwenda mbele, lakini njia pekee ya kujinasua ni kuondoka kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo, na kukoma kutembea kwenye vichochoro vya mji mkuu wa serikali zao vibaraka na maadui dhahiri wa Ummah. Suluhisho tu liko katika mwendelezo wa 'Jihad' katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) ili kuzishinda na kuziangamiza dola za kikoloni, pamoja na Amerika, NATO na washirika wao, ambao wamemwaga damu ya maelfu ya Waislamu kutoka Iraq hadi Syria na kutoka Libya hadi Yemen na Afghanistan katika miongo miwili iliyopita, na kuwawezesha Ummah kwa panga, subra na ikhlasi yenu.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Saifullah Mustanir
Mkurugenzi wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan