Vipi Khilafah Itakavyo Wadhamini Wanawake Haki Zao za Kielimu
- Imepeperushwa katika Khilafah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Uislamu hutazama utafutaji elimu ya Kiislamu kuwa faradhi kwa wanawake na wanaume.
Uislamu hutazama utafutaji elimu ya Kiislamu kuwa faradhi kwa wanawake na wanaume.
Uislamu umeipa hadhi kuu heshima kwa wanawake. Dalili kadha wa kadha za Kiislamu zinawawajibisha wanaume na mujtama kuwatazama na kuamiliana na wanawake kwa heshima na daima kulinda hadhi yao.
Leo kuna zaidi ya dola hamsini za Waislamu, zote zikidai kuwa Uislamu ndio dini yao na chimbuko la utambulisho wao. Dola zote hizi daima ziko katika mchakato wa kujenga na kujenga upya matumaini ya kufaulu katika malengo ya maendeleo yaliyowekwa na Wamagharibi.