Jumamosi, 21 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Matembezi ya Halaiki ya Kuinusuru Gaza “Kuwahutubia wale Wanaohusika!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miezi 21, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa na kupotezwa kwa zaidi ya wanaume na wanawake 200,000 Waislamu hadi sasa. Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa matembezi makubwa ya halaiki kote nchini Uturuki licha ya serikali ya Uturuki kuyapiga marufuku.

Mkataba wa Biashara na Unyenyekeaji wa Indonesia kwa Maslahi ya Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza makubaliano ya kibiashara na Indonesia, kupunguza ushuru unaotishiwa wa 32% kwa bidhaa za Indonesia hadi 19%. Kwa upande wake, Indonesia ilijitolea kununua nishati ya Marekani kwa dolari bilioni 15, bidhaa za kilimo kwa dolari bilioni 4.5, na ndege 50 za Boeing, ikiwa ni pamoja na aina ya 777. Trump alidai Marekani itapata ufikiaji kamili wa soko la Indonesia bila kulipa ushuru. Makubaliano hayo yalifuatia vitisho vya ushuru wa juu na yalikamilishwa baada ya mazungumzo na Rais wa Indonesia Prabowo Subianto. Bado haijulikani ni lini upunguzaji wa ushuru na ununuzi utaanza kutekelezeka. Biashara ya Indonesia na Marekani ilifikia karibu dolari bilioni 40 mwaka 2024, na nakisi ya biashara ya bidhaa za Marekani ya takriban dolari bilioni 18.

Idhini ya Marekani sio Kipimo cha Uamuzi wa Kisiasa kwa Umma wa Kiislamu

Mnamo tarehe 17 Julai 2025, Dawn News ilinukuu kutoka Reuters, "Ikulu ya White House mnamo Alhamisi ilisema kwamba hakuna ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump iliyopangwa Pakistan "kwa wakati huu" baada ya kuenea kwa taarifa za safari hiyo. Mapema siku hiyo, baadhi ya vituo vya habari vya televisheni vya ndani viliripoti, vikinukuu vyanzo, kwamba Trump alitarajiwa kuzuru Pakistan mwezi Septemba. Chaneli za habari zilisema kwamba Trump pia angetembelea India baada ya kuwasili jijini Islamabad mwezi Septemba. Chaneli hizo baadaye ziliondoa ripoti zao.” [Dawn]

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu