Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
"Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia...
inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!"

Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kampeni Pana ya Kiulimwengu kwa Anwani:
Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia... inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!

Kwa muongozo wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amlinde, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni pana ya kiulimwengu kuadhimisha tukio Adhimu la Hijria la Ukombozi wa Konstantinopoli (mji wa Heraklias) ambao ulizungukwa kuanzia mnamo 26 Rabii’ al-Awwal mpaka 20 Jumada al-Awwal 857 H sawia na 5 Aprili mpaka 29 Mei 1453 M na hivyo bishara njema ya Hadith tukufu ya Nabii (saw) ikatimia «لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»“Mutaifungua Konstantinopoli, Amiri wake ni Amiri bora, na jeshi bora ni jeshi hilo.”

Sisi katika Hizb ut Tahrir tumezindua kampeni ya kiulimwengu kwa sababu tatu:

Ya kwanza, ni kukumbuka utukufu wake ili kila mwenye macho ataona utukufu wa Uislamu na Waislamu pale ambapo Uislamu wao unatekelezwa kivitendo. Ukafiri hautokuwepo, bali ukweli utakuwa juu na utanyanyuliwa kama Adhana (mwito wa kuswali) kwa Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa). Wafursi na Wabaizantino wakajisalimisha mbele yao, na hivi karibuni wataunganishwa, kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu, na dada wa Baizantino, Roma kwa kuamini sehemu ya bishara njema ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw), ukombozi wa Roma.

Ama ya pili, itulizeni mioyo yenu kwa kujihakikishia kutimia kwa bishara tatu nyingine za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw), kwa kuwa ya kwanza ishatimia. Mtume (saw) alitoa bishara njema za ukombozi wa Konstantinopoli, ukombozi wa Roma, kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume na kupigana na Mayahudi na kuwashinda kwa nguvu kubwa… Mtume (saw) anazungumza kutokamana na Wahyi, bishara njema tatu zilizobakia za Nabii zitatimizwa kwa idhini Yake, utukufu ni wake Yeye Subhannahu; lakini, hazitotimia kwa kushuka kwa malaiki kutoka mbinguni, na kutukukabishi sisi. Badala yake ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu kwamba tumnusuru Mwenyezi Mungu na Yeye atupe ushindi Wake ili tuweze kusimamisha sheria Yake na kuutukuza muundo wa Dola Yake na kuandaa tunachoweza katika nguvu na kisha kupambana katika njia Yake. Kisha dunia itang’ara kwa bishara njema tatu zilizobakia na dunia itanawiri kwa kuwepo Khilafah kwa mara nyingine tena.

Ama ya tatu, Kafiri Mmagharibi, pamoja na makhaini wa Kiarabu na Kituruki waliweza kuivunja Khilafah mnamo 1342 H - 1924 M na kuzingatia kuwa kuvunjwa huku ni sambamba na ukombozi wa Konstantinopoli, na hili likampa tena nguvu Kafiri Mmagharibi ambazo alikuwa amezipoteza. Wasiwasi wa Magharibi ukawa ni kuweka juhudi kubwa ili kuzuia kurudi tena kwa Khilafah ili isiweze kupoteza tena nguvu walizozirudisha hususan kwa kuwa wamekuwa wakoloni wa nchi za Waislamu. Wanafuatilia kwa makini harakati ndani ya nchi za Waislamu, kwa hiyo ilipotangazwa kusimama kwa Hizb ut Tahrir mnamo 1372 H - 1953 M na ikawa wazi kwa Magharibi kwamba nguzo ya kazi za chama na suala lake nyeti ni kurudisha Khilafah tena na kwamba kiko makini katika kazi yake, Magharibi ikaamrisha vibaraka na watawala wake kukipiga marufuku chama na kukifuatilia kwa kuwashika na kuwatesa mpaka kupata shahada ndani ya baadhi ya maeneo na kuwafunga vifungo virefu na katika maeneo mengine kufikia kuwafunga maisha… Kisha wakaongeza njia za kudanganya, kughushi na kubadilisha ukweli pasina aibu…

Hivyo basi, licha ya njia za kuupamba uongo waliouzua licha ya kukithirisha majaribio ya udanganyifu dhidi ya ukweli ambao wamejikita ndani yake, hawakupata sikio linalosikiza kutoka katika wanachama wa chama au kutoka katika kila Muislamu aliye timamu. Badala yake walikuwa

[كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاءً حَتَّى إِذَا جَاءَهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئاً] 

“Vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani, Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote.” [An-Nur: 39]

Na kwa njama, kashfa na uovu wote dhidi ya chama na uongozi wake, wakidhania kwamba watakishawishi chama lakini walifeli kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na wakakata tamaa na hawakupata lolote zuri licha ya kiwango cha uongo wao, njama zao na uhadaifu wao kilipofikia,

[وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ]

“…na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliye vifanya.” [Fatir: 43]

Wataona natija ya hilo kwa Mwenyezi Mungu, licha ya kuzidi kwa kashfa na hila zao,

[وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِنْدَ اللَّهِ مَكْرُهُمْ وَإِنْ كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ] 

"Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima.” [Ibrahim: 46].

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atuwezeshe kutimia kwa bishara njema za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) ili Khilafah ya Ummah huu iweze kurudi na baada ya hapo kuikomboa Al-Quds, na Roma itakombolewa kama ilivyotanguliwa na dadake… kutimia kwa hadith za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw)… Na pia tunamuomba Yeye, Utukufu uwe Kwake, atupe msaada kutoka Kwake ili tuweze kuboresha na kukita katika kazi ili tuwe tunaostahiki kupata ushindi wa Mwenyezi Mungu, Al-Aziz Al-Rahim.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi* Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

Ijumaa, 8 Jumada Al-Awwal 1441 H – 3 Januari 2020 M

                                               Fuatilia Kampeni kwa Lugha Nyingine

Hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Juu ya Tukio la Ukumbusho wa Ukombozi wa Konstantinopoli mnamo 857 H – 1453 M

Isome Hotuba kupitia Facebook

Isome Hotuba kupitia Ukurasa wa Afisi Kuu ya Habari

Video ya Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Mohammad)
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Akitangaza uzinduzi wa Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari
"Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia... inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!"

Video ya Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Akitangaza uzinduzi wa Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari
"Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia... inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!"

Video ya Eldar Khazmin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
kuhusiana na Kampeni ya Kiulimwengu
"Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia... inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!"

                Alama Ishara za Kampeni               

          

 #ConquestofIstanbul    tw  instagram
 #Constantinople   tw  instagram 
 فتح_القسطنطينية#    tw  instagram
 القسطنطينية#   tw  instagram 
 #İstanbulunFethi    tw instagram 
 #istanbul    tw  instagram

 

Banner Sw

Afisi Kuu ya Habari

Poster Sw

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 22 Januari 2020 09:44

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu