Alhamisi, 05 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Kongamano la kila Mwaka la Khilafah “Khilafah ya Kiislamu… Kuelekea Mfumo Mpya wa Kimataifa”

Mnamo Ijumaa, Oktoba 11, 2024, Hizb ut-Tahrir / Wilayah Tunisia ilifanya Kongamano la kila Mwaka la Khilafah chini ya kichwa:

“Khilafah ya Kiislamu… Kuelekea Mfumo Mpya wa Kimataifa”

Shukrani zote kwa Mwenyezi Mungu na fadhila yake, ukumbi ulijaa umati mkubwa wa watu wa Al-Khadra, Kongamano hilo lilifunguliwa kwa usomaji wa Aya za Qur'an Tukufu, na kufuatiwa na hotuba ya Dkt. Al-Asaad Al-Ajili yenye kichwa “Ilichopoteza Umma Baada ya Kuvunjwa Khilafah.” Kisha ikapeperushwa hotuba ya video kutoka Kitengo cha Wanawake katika Al-Khadra yenye kichwa “Ufisadi wa Ubepari, Demokrasia, na Hakuna Wokovu isipokuwa kupitia Uislamu na Khilafah” ya Ustadha Hanan Al-Khamiri, kisha baada yake Shab Omar Al-Arabi akatoa hotuba yenye kichwa “Uwezo wa Dola ya Khilafah Kuongoza Ulimwengu na Kusimamisha Mfumo Mpya wa Kimataifa.” Kisha hotuba ya video ikapeperushwa kutoka Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na kutoka mji wa Jenin Al-Qassam haswa na Ustadh Jandal Salah yenye kichwa “Kilio Kutoka Jenin, kikiomba Umma na Majeshi yake Kuinusuru Gaza.” Na kongamano likahitimishwa kwa hotuba ya Ustadh Muhammad Nasser Shuweikha ambamo alithibitisha kuwa Umma wa leo una uwezo wa kuregesha nafasi yake ya kuwa Umma bora zaidi kuwahi kutolewa kwa ajili ya watu ikiwa utatafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuchukua njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika kusimamisha dola kama dira na mwongozo wake, na kuichukua Hizb ut Tahrir kama kiongozi wake hasa kwa ajili yake, kwa kuwa umeelewa na kujifunza juu ya uaminifu wake, uthabiti, na uwezo wake wa kuuongoza.

Hotuba hizo zilijumuisha uingiliaji kati mara tatu wa mwendeshaji kongamano hilo, Ustadh Najm al-Din Shuaibin, ambapo alizungumza kuhusu mafunzo na hadithi kutoka kwa historia ya Kiislamu na kutoka kwa mashujaa wa mujahidina huko Gaza, ili kuwahamasisha wanazuoni na vijana wa Umma kuinua azma yao na kutekeleza kadiri mas’uliya katika hali hii nyeti katika historia ya Waislamu.

Hivyo basi, Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia inaendelea na kazi yake isiyochoka na yenye kuendelea, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, katika kukanusha fikra za Kimagharibi ambazo ni ngeni kwa Umma wa Kiislamu, kutoka kwenye mipaka ya Sykes-Picot, dola ya kiraia, na kutawaliwa na hukmu nyenginezo zisokuwa zile alizoziteremsha Mwenyezi Mungu, na kwa kurudisha fikra safi na asilia za Uislamu kuhusu umoja wa Waislamu na kuteuliwa kwa khalifa ambaye anatawala kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu na udharura wa kutekeleza hukmu za Uislamu mtukufu ulioteremshwa juu ya mbingu saba... mpaka Mwenyezi Mungu atangaze ushindi na ahadi yake... “Hakika Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake,” na dua yetu ya mwisho ni kwamba sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia

Ijumaa, 08 Rabi’ al-Akhir 1446 H sawia na 11 Oktoba 2024 M

- Sehemu ya Amali ya Kongamano -

Mwaliko wa Kuhudhuria Kongamano la kila Mwaka la Khilafah

Ustadh Khubayb Karbaka

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

- Ualishi wa Kongamano la kila Mwaka la Khilafah -

Alama Ishara za Kongamano

#أقيموا_الخلافة

#كيف_تقام_الخلافة

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

#TurudisheniKhilafah

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir

Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu