Ijumaa, 24 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Mkutano na Waandishi wa Habari: “Uchaguzi ni njia ya Kuendeleza Mfumo wa Kisekula ambao ni Wajib Ubadilishwe kwa Kusimamisha Khilafah”

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia ilifanya mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano huko Ariana katika mji mkuu, Tunis, saa 10:30 asubuhi kwa saa za eneo, wenye kichwa “Uchaguzi ni njia ya Kuendeleza Mfumo wa Kisekula ambao ni Wajib Ubadilishwe kwa Kusimamisha Khilafah” Ustadh Abdul Raouf Al Amiri, Mkuu wa Afisi ya Kisiasa ya Hizb ut Tahrir, alishiriki katika kuwasilisha kongamano hili la Wilaya ya Tunisia, Ustadh Muhammad al-Nasser Shuwaikha, Mjumbe wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Tunisia, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, na Ustadh Yassin bin Yahya, walishiriki katika kuwasilisha katika mkutano huu mbele ya kundi la wageni hotuba tatu za kongamano zilizotolewa na washiriki wa mkutano huu zilizogusa mada tatu. Mada ya kwanza, ya Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri, kichwa chake kilikuwa “Ukumbusho wa msimamo wa Hizb ut Tahrir kwenye njia ya kisiasa tangu mwanzo wa mapinduzi hadi leo.”

Na mada ya pili, Ustadh Muhammad Al-Nasser Shuwaikha alizungumza juu ya “Ulinganizi wa mradi wa Umma bila kuruhusu sisi kuainishwa au kuanguka katika mfumo wa jozi pamoja au dhidi ya kushiriki katika uchaguzi, kuangazia sifa ya kilimwengu ya Hizb na kwamba mradi wake ni mradi wa Umma na kutoa ulinganizi kwa Umma kufanya kazi nasi kwa sababu ndiyo pekee yenye mradi wa hadhara unaotokana na itikadi ya Umma na yenye uwezo wa kuukomboa kutoka kwa ushawishi wa kigeni na kuumsha.”

Mada ya tatu, ilitolewa na Ustadsh Yassin Bin Yahya ambapo alitoa taarifa ya hitimisho ya mkutano na waandishi wa habari, ambapo alizingatia nukta tano:

Ya kwanza: ni kwamba mabadiliko msingi na ya kina kwa utawala huu ambao watu walitaka kuuangusha mwanzoni mwa mapinduzi hayawezi kupatikana kupitia uchaguzi chini ya paa la usekula.

Pili: Mifumo ya utawala iliyopo katika nchi za Kiislamu, msingi wake na kuendelea kwake iko mikononi mwa nchi za Magharibi

Tatu: Vita vinavyoendelezwa na utawala katika kila kituo cha uchaguzi, ili kuwavuruga watu kutoka katika mradi huo mkubwa wa Uislamu, na kwa ajili ya hayo maisha ya watu yakapotea na vizazi vya Waislamu kuangamizwa, vinazunguka katika korido za balozi za Magharibi.

Nne: Haiwezekani kuupindua utawala na kuikomboa nchi kutoka katika utiifu wa kisiasa wa nchi za Magharibi isipokuwa kwa kuwaweka sawa watu wenye nguvu pamoja na jamaa zao, ili mgogoro huo utatuliwe kwa manufaa ya Umma.

Tano: Mwamko wa mataifa haupatikani kwa kubadili mtawala na kurekebisha katiba, bali ni kupindua utawala na makaazi yake yote ya kifikra, kithaqafa na kikanuni na kuubadilisha kwa utawala wa Kiislamu ulioteremshwa kutoka juu ya mbingu saba. Hivyo basi, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia inaendeleza mapambano yake ya kisiasa dhidi ya mfumo huu uliotungwa na makafiri wa Magharibi na miradi yake yote ambayo inawafanya watu wa Zaytouna kuwa wanyonge zaidi katika maisha yao hadi kufikia lengo lake, ambalo ni kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kwa kusimamisha dola ya Khilafah Radhida kwa njia ya Utume, yenye kuwaokoa wanadamu.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia

Alhamisi, 16 Rabi’ ul-Awwal 1446 H sawia na 19 Septemba 2024 M

- Sehemu ya Amali ya Mkutano na Waandishi wa Habari -

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir

Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu