Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Misimamo ya Hizb ut Tahrir Yausumbua Usingizi wa Ukoloni na Kuwachanganya Vibaraka na Mawakala Wake!

Mnamo siku ya Ijumaa, Oktoba 15, 2021, Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia iliandaa visimamo baada ya swala ya Ijumaa jijini Tunis na katika miji ya Kairouan na Sfax ili kukabiliana na upuuzi wa kisekula na njia ya kisiasa inayoharibu nchi. Kauli mbiu kama "Hapana kwa Demokrasia Hapana kwa Udikteta, Bali Khilafah ya Kiislamu" ilipazwa katika visimamo hivyo. Kisha hotuba zilitolewa za kutoa wito wa ukombozi wa nchi kutokana na utawala wa Magharibi na zana zake za ndani, na kukataliwa kwa usekula, katika sehemu zote mbili, mfumo wa kidemokrasia wa bunge na mfumo wa urais wa kidikteta, na kuufanya Uislamu peke yake kuwa ndio msingi wa utawala na sheria kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Visimamo hivyo vilifanyika mbele ya Msikiti wa Al-Fath jijini Tunis, Msikiti wa Lakhmi huko Sfax, na misikiti ya Al-Ghufran na Al-Naqra huko Kairouan, baada ya mamlaka tawala kukataa ombi la kufanya visimamo hivyo katika viwanja na kugeuza ukumbi wa manispaa na Barabara ya Al-Thawra katika mji mkuu kuwa kambi ya usalama ili kuzuia utitiri wa washiriki, na kisha kutuma kikundi cha magari ya usalama kwa Msikiti wa Al-Fath kuzuia watu kukusanyika. Maafisa wa usalama walizunguka kisimamo hicho na kulitenga eneo lote la msikiti ili kusiwe na mtu yeyote atakayekaribia kisimamo hicho, hata hivyo, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia, Dkt. Al-Asaad Al-Ajili alitoa hotuba yake.

Ukamataji kadhaa pia ulifanywa miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika mji wa Sfax, dhidi ya nyuma ya hotuba kali iliyotolewa na Mwanachama Omar Al-Arabi mbele ya umati wa waumini.

Pia, kufuatilia ripoti za vyombo vya habari zilizoegemea upande mmoja kama vile ya Shirika la Habari la Anatolia, inaonyesha kwamba kile ambacho Mosaique FM imefanya, na vyombo kadhaa vya habari vya sauti na maandishi vimefuata nyayo, sio utaalam katika utoaji wake, bali ni fursa mpya kupoteza kile kilichobakia cha uaminifu wake.

Taarifa kutoka kwa mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia, Ustadh Khabib Karbaka, ilitolewa kwa habari hii ya uwongo. Vipande vyake ni pamoja na: katika kukabiliana na mkanganyiko huu wa wazi ambao ni kinyume na inavyotakiwa na uadilifu na uaminifu wa taaluma ya vyombo vya habari, ninasema yafuatayo:

1. Hizb ut Tahrir anatoa wito wa kuondolewa kwa mfumo fisadi wa kidemokrasia ambao ndio sababu ya machafuko ya kisiasa nchini Tunisia, na kutoa wito wa kuregesha tena maisha ya Kiislamu kwa kurudisha utawala wa Uislamu.

2. Khilafah ambayo Boubaker bin Okasha (mwandishi wa habari wa Tunisia) anaibeza sio ndoto, na sio muundo unaojulikana kwa historia ya Kiislamu kwa mamia ya miaka tu. Badala yake, ni mfumo wa sheria ulioasisiwa na mkusanyiko wa hukmu za kisheria zilizovuliwa kutoka kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kutoka kwa Sunnah ya Mtume (saw), na kutoka kwa Ijma ya Maswahaba, Mwenyezi Mungu awawie radhi.

3. Tunatoa wito kwa vyombo vya habari katika taifa letu (Ummah) kutenda kulingana na dini yao na kuwa kwao kwa Umma wao. Suala la Khilafah ni mada ya habari ya kiwango cha juu katika saizi yake kwa sababu ni suala la Umma mzima wa Kiislamu na lengo la umakini wake na matumaini ya wokovu, na ni suala la chama cha siasa ambacho Hizb ut Tahrir imejaza wigo wa ardhi. Kwa hivyo vitendo vya Hizb ut Tahrir kwa ajili yake, na kampeni zote za uchafuzi wa jina, tashwishi na uzibaji macho hazitafanya kazi kwa Hizb ut Tahrir. MWISHO.

Linki za ripoti za habari kuhusu visimamo vya Hizb ut Tahrir nchini Tunisia:

تونس.. "حزب التحرير" يدعو للتصدي للمسار السياسي "العابث" بالبلاد

من أمام مسجدي"الفتح" و"اللخمي": حزب التحرير يُجدّد استغلال المساجد لأغراض سياسية

أنصار حزب التحرير يقتحمون جامع الفتح ويدعون لإقامة دولة الخلافة محرضين على الرئيس سعيد

عاجل: أنصار حزب التحرير يحاصرون جامع الفتح وينادون بإقامة الخلافة

تونس.. أنصار حزب التحرير "الإسلامي" يقتحمون جامعا ويحرضون على سعيّد

"ذراع الإخوان" يقتحم أكبر مساجد تونس ويحرض ضد الرئيس

وزارة الشؤون الدينية: "لا صحة لما تم ترويجه حول اقتحام منبر جامع الفتح.. ولن نسمح بتوظيف المساجد"

وقفة حزب التحرير الإحتجاجية من جامع الفتح: وزارة الشؤون الدينية توضح

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah ya Tunisia

Sehemu ya Video za Visimamo

Kisimamo cha Mji wa Kairouan

Kisimamo cha Mji wa Sfax

Kisimamo cha Mji Mkuu wa Tunis

Hotuba Iliyotolewa Kuhusiana na Amali Zilizofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Na Dkt. Al-Asaad Al-Ajili

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukemeaji wa Vyombo vya Habari kwa Habari za Uongo kuhusu Visimamo Vilivyofanywa na Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu