Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Kwa Mara ya Pili, Hotuba za Halaiki Zilitolewa dhidi ya Mfumo wa Makubaliano katika Msikiti Mkuu wa Khartoum

Katika muendelezo wa kampeni dhidi ya Mfumo wa Makubaliano, Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan ilitoa hotuba za halaiki kwa mara ya pili leo Jumatano tarehe 4/1/2023 M, baada ya swala ya Adhuhuri katika Msikiti Mkuu wa Khartoum, zikibainisha hatari ya fikra ya uhuru iliyodhaminiwa na Mfumo wa Makubaliano hayo.

Kwa mara hii hotuba hizi zilizungumzia juu ya kujitolea kwa wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu, na kujitahidi kusimamisha Sharia na kutabikisha hukmu za Mwenyezi Mungu (swt):

Hatari ya fikra ya uhuru, kama ilivyo katika nidhamu wa kidemokrasia ya kisekula ambayo ilijumuishwa katika mfumo wa makubaliano, na kwamba lengo la uhuru huu ni kusambaratisha jamii ya Kiislamu kwa kuishambulia familia kupitia kuwapa wanawake haki ya kuwa na mahusiano nje ndoa, na kusafiri bila ya Mahram, kwani inaruhusu uasi, upotovu, ushoga, na mambo mengine yenye kuangamiza. Wakathibitisha kwamba uhuru wote huu umejengwa juu ya mikataba ya kimataifa, ambayo inagongana na aqida ya Kiislamu, hivyo Muislamu, awe mwanamume au mwanamke, ni mja wa Mwenyezi Mungu (swt),  ambaye ni lazima ajifunge na amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu.

Na wakaonyesha hatari ya kuwa tegemezi kwa maelekezo ya balozi na mashirika ambayo yameegemezwa katika msingi usiyo wa Kiislamu, kama vile Umoja wa Mataifa, ambayo haijuzu kushiriki ndani yake, wala kufuata mikataba yake. Na wakavionya vikosi vya kisiasa vinavyohusiana nao, vikiwemo vya kijeshi na raia, juu ya hatari ya kutekeleza ajenda za dola hizi za kikoloni, balozi na mashirika yao. Na kwamba suluhisho msingi ni kukataa makubaliano hayo kwa kuwa kinyume kwake na Uislamu, na kufanya kazi ya kusimamisha dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume. Waumini walifanya maingiliano kwa kupiga takbira na tahlil, kushangilia na kutamka: (Dola zote zimefeli, Khilafah ndio suluhisho), (Hakuna njia kwetu isipokuwa kwa Uislamu) na (Sio utawala wa kijeshi wala wa kiraia, bali Khilafah ya Kiislamu).

Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa Walimwengu.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

- Ripoti ya Picha juu ya Ufanisi wa Amali ya Hotuba za Halaiki / Siku ya Pili -

Hotuba iliyotolewa na Ustadh Abdullah Hussein

Katika Lango la Kusini la Msikiti Mkuu jijini Khartoum

Hotuba iliyotolewa na Ustadh Ahmad Abbakar

Katika Lango la Kaskazini la Msikiti Mkuu jijini Khartoum

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu