Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Matembezi ya Hizb ut Tahrir kupeleka Al-Burhan ni kitabu kilicho wazi

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa maandamano ya kishindo yaliyoanzia Msikiti Mkuu wa Khartoum hadi Ikulu ya Jamhuri, baada ya Swala ya Adhuhuri, Jumapili tarehe 15 Jumada al-Akhirah 1444 H sawia na 08/01/2023 M, ili kumkabidhi Al-Burhan barua ya wazi.

- Ripoti ya Picha juu ya Matembezi na Kukabidhi Barua ya Wazi -

Ripoti kwa Vyombo vya Habari kuhusu Matembezi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Kuanzia Msikiti Mkuu wa Khartoum hadi Ikulu ya Jamhuri ili kumkabidhi Al-Burhan Barua ya Wazi

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa matembezi ya kishindo yaliyoanzia Msikiti Mkuu wa Khartoum hadi Ikulu ya Jamhuri, baada ya Swala ya Adhuhuri, mnamo Jumapili tarehe 15 Jumada al-Akhirah 1444 H sawia na 08/01/2023 M, ili kumkabidhi Al-Burhan barua ya wazi.

Matembezi hayo yaliongozwa na mbebaji bendera ya al-liwaa Ustadh Ahmed Abkar, wakili na mjumbe wa Baraza la Hizb katika Wilayah ya Sudan, na nyuma yake walikuwepo viongozi wa hizb, mashababu wake na wananchi kwa jumla walioshiriki matembezi hayo kuanzia Msikiti Mkubwa, na wengine waliojiunga na matembezi hayo katika njia yake.

Wakati wa matembezi hayo, bendera za Al-Raya na Al-Liwaa zilipeperushwa, ambazo zinaashiria Al-Raya na Al-Liwaa za Mtume (saw).

Matembezi hayo yalianza katika jumuiya ambayo haikufunga barabara na wala haikutishia usalama wa mtu yeyote, hadi pale mtu alipotoa maoni yake kwamba matembezi haya yanathibitisha kwamba mashababu wa Hizb ut Tahrir wanapewa thaqafa na ni wenye nidhamu. Waandamanaji walipaza sauti zao kwa takbira, tahlil na miito, ikiwemo: (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Khilafah ni ahadi ya Mwenyezi Mungu), (Kiongozi wetu milele ni bwana wetu Muhammad), (Sio utawala wa kiraia wala wa kijeshi, bali Khilafah ya Kiislamu), (Dola zote zimefeli, na Khilafah ndio suluhisho).

Na matembezi hayo yalipofika kwenye lango la kusini la ikulu hiyo, baadhi ya viongozi wa kijeshi na wanajeshi walitoka nje na kujipanga mbele ya lango hilo, ujumbe wa hizb ulisonga mbele chini ya uongozi wa Mheshimiwa Nasir Ridha, mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb katika wilayah ya Sudan, akifuatana na Usradh Ibrahim Othman Abu Khalil, msemaji rasmi, na Ustadh Muhammad Al-Hassan, mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika wilayah ya Sudan.

Hizb iliwasilisha barua ya wazi yenye kichwa: (Barua ya wazi kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan kwa Al-Burhan na kwa Watu Wetu Nchini Sudan) kwa uongozi wa Ikulu ya Jamhuri ili kukabidhiwa kwa Al-Burhan. Mojawapo ya mambo muhimu yaliyomo ndani ya barua hiyo ya wazi ni: [Hakika Muundo wa Mkataba unabainisha kwamba: (Sudan ni nchi yenye tamaduni, makabila na kidini nyingi), na huo ni uwongo, kwa sababu karibu 98% ya watu wa Sudan ni Waislamu].

[Muundo wa Makubaliano hayo pia yanabainisha kwamba: (Sudan ni dola ya kiraia, ya kidemokrasia, ya kifederali, ya kibunge, ambayo ubwana ndani yake uko kwa watu na ndio chimbuko la mamlaka), na yote haya ni kinyume na Uislamu, dola ya kiraia ni dola ya kisekula inayotenganisha dini na maisha, na demokrasia inafanya haki ya kutunga sheria kuwa ni ya wanadamu, kwa kuwa haizingatii hukmu za kisheria, na kwa sababu ubwana ndani yake sio kwa Sharia; Kitabu na Sunnah na yaliyoongozwa kwazo. Na kwamba ufederali unaifanya dola kugawanyika kwa sababu ina humaanisha wingi wa watawala wanaopata mamlaka yao ya dhati kutoka katika majimbo yao, na pia inamaanisha wingi wa sheria, kwa maana kila jimbo lina katiba na sheria zake].

Na imekuja katika barua hiyo ya wazi: [Kwamba Uislamu mtukufu ni aqida na mifumo ya maisha, yaani ni dini na kutokana nayo ni dola, na kazi ya anayekaa kwenye kiti cha utawala ni kutabikisha Uislamu kikamilifu na usiopungua. Na kwamba Uislamu mtukufu pamoja na hukmu zake ndio unaoikomboa nchi kutoka kwenye joka la ukoloni unaotawala nchi kupitia balozi za nchi za Magharibi, ujumbe wa UNITAMS, na mashirika mengine yote ya Kimagharibi yanayoeneza ufisadi katika nchi zetu, na Uislamu ndio unaoweka mbali hali hii ya kisiasa, yenye kuwatumikia ukoloni].

Na ilisisitiza kwamba muundo wa makubaliano hayo hayatasuluhisha migogoro ya utawala na uchumi iliyokita mizizi nchini, na kwamba mzozo kati ya jeshi na viungo vya kisiasa, kwa kweli, ni mvutano kati ya vibaraka juu ya viti kwa niaba ya dola kubwa (Marekani na Uingereza), na kwa sababu ni makubaliano ambayo yaliegemezwa kwenye msingi wa batili; nao ni kutenganisha dini na maisha, dola na jamii, na kwa sababu ni suluhisho la maridhiano la muda kati ya nguvu zisizo na ikhlasi.

Na imekuja katika barua hiyo: [Sisi, katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan, tunaamsha azma ya watu wote wanyoofu wenye nguvu na ulinzi, ili kuipa nusra Hizb ut Tahrir ili kufikisha Uislamu safi na mtakatifu kwenye utawala, kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ili kung'oa ushawishi wa kafiri mkoloni kutoka katika nchi yetu... Ewe Al-Burhan, kuweni radhi kwa Mola wenu, na huenda mukamcha Mwenyezi Mungu, basi jua kwamba bado uko na nafasi katika umri, basi jinufaishe nayo kwa kutubia kwa Mwenyezi Mungu, ﴾تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَصُوحاً﴿ “Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli!” [At-Tahrim: 8] na kuacha kutabikisha hukmu za ukafiri na mifumo yake, na hiyo ni kwa kuipa nusra Hizb ut Tahrir inayoufahamu mfumo mtukufu wa Uislamu, na jinsi ya kuutabikisha, na inafahamu uhalisia wa mvutano wa kimataifa, na jinsi ya kupita ndani yake, ili muwe kama wale wa mwanzo: ﴾وَالسَّابِقُونَ الأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالأَنْصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُمْ بِإِحْسَانٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ﴿] “Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye” [At-Tawba: 100]

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah ya Sudan

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ukurasa wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Vyuo Vikuu vya Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu