- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ripoti ya Habari 25/10/2022
Muendelezo wa amali za umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan katika maeneo na mikoa tofauti tofauti ya nchi ili kujenga rai jumla yenye ufahamu juu ya hukmu za Uislamu na masuluhisho yake yanayohusiana na mifumo tofauti tofauti ya maisha, ambazo zilishughulikia rasimu ya katiba ya mpito na kodi na ushuru mbalimbali.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Omdurman Magharibi yenye kichwa: "Rasimu ya Katiba ya Mawakili Ilicho Nacho ni Kipi" mnamo Septemba 21, 2022 katika Soko la Libya, ambapo Ustadh Ishaq Muhammad Hussein alizungumza kwamba ikiwa sheria imeundwa kwa ajili ya wanadamu, huwaletea taabu, na tofauti kulingana na maumbile na mazingira yao. Rasimu ya katiba ya mpito ya Chama cha Mawakili ni rasimu ya kisekula inayotenganisha dini na maisha na miradi ya Kikafiri katika nchi yetu inaharakisha vita dhidi ya vifungu vya sheria vilivyosalia katika sheria na kanuni kupitia kutia saini CEDAW na kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi. Ni katiba yenye msingi wa kutenganisha dini na maisha na hivyo kutenganisha dini na siasa na dola na wanataka kuifanya imani hii kuwa ndio msingi wa katiba zote za ulimwengu, ukiwemo ulimwengu wa Kiislamu, na Sudan ni sehemu yake.
Chini ya mada: "Ushuru ulioharamishwa na athari zake kwa maisha ya watu", Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Khartoum mnamo Septemba 29, 2022, karibu na bandari ya ardhini jijini Khartoum ambapo Ustadh Fadhallah Ali alizungumzia hali ya uchumi nchini kwa jumla, na kuhusu maamuzi ya Waziri wa Fedha yaliyoyafanya maisha ya watu kuwa motoni, na yaliyosababisha wafanyibiashara kufunga masoko, na kupandisha bei za bidhaa na huduma. Mzungumzaji alieleza kuwa sababu kubwa ya hali hiyo mbaya ya kiuchumi ni kodi, forodha na ushuru, fedha hizi, ambazo ni rasilimali kuu ya serikali kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Fedha. Aliwaeleza wahudhuriaji jinsi ada hizi zinazotozwa na serikali kwa wafanyibiashara zinapunguza pensheni za watu, kuongeza bei, na kuweka mifano halisi ya mateso ya watu ili kujipatia riziki.
Pia, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ilifanya mkao wake wa kawaida katika mji wa El Obeid mnamo tarehe 8 Oktoba 2022 chini ya kichwa: "Kodi kubwa zinazotozwa wafanyibiashara, suluhisho ni nini?" Katika waraka wa kwanza, Ustadh Hassan Farah alizungumzia madhara ya kodi kwa jamii, akionyesha kuwa inapandisha bei na kusababisha watu kupandisha bei. Katika waraka wa pili, Ustadh Al-Nazir Muhammad Husayn alizungumza kuhusu utatuzi wa tatizo hilo, ambalo lipo katika kuondolewa kwa mifumo ya kibepari na kutekeleza mfumo wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ufaradhi ambao Mwenyezi Mungu (swt) aliuweka juu ya Waislamu. Maingiliano yalikuwa mazuri, ambapo Ustadh Muhammad Atron, ambaye anasoma katika ngazi ya sekondari, alishiriki, akiishukuru hizb kwa dori yake changamfu katika kuwaelimisha watu kuhusu Uislamu, akisisitiza kuwa suluhu iko katika Uislamu.
Chini ya kichwa: "Uundaji wa Mawaziri Unaotarajiwa na Ukosefu wa Maadili", Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa huko Omdurman Magharibi mnamo Oktoba 12, 2022, katika Soko la Libya, ambapo Ustadh Abd al-Rahim Abdullah alianza mazungumzo yake kuhusu kile kinachoendelea hapa na pale ndani ya korido za serikali ya kiutendaji (ya kitaifa) ambayo mbegu yake imemwagiliwa maji na kukuzwa na Kafiri Magharibi. Kila mihimili ya dola inapotikisika na mambo kuwa magumu katika kutatua matatizo yanayoikabili, mishale huelekezwa kwa mawaziri wa serikali, na huwabadilisha watumishi wa wizara ili kurefusha maisha ya mifumo hii iliyotungwa na binadamu. Kwa kumalizia, mzungumzaji aliwataka waliohudhuria kufanya kazi na Hizb ut Tahrir, ambayo imeandaa katiba ya kina ya utawala, idara, uchumi, jamii na mengineyo, na kwa watu wenye nguvu kuinusuru Hizb ut Tahrir, nusra ambayo utaregesha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Madani yenye kichwa: "Serikali, kwa kuchukua kodi na ushuru ulioharamishwa, imeyafanya maisha ya watu kuwa jahanamu isiyoweza kuvumilika," kwenye kituo cha basi katika Soko Kuu mnamo Oktoba 16. , 2022, ambapo Bw. Sowar alizungumza, akieleza kuwa serikali kupitia kuchukua kodi na ushuru ulioharamishwa imeyafanya maisha ya watu kuwa jahanamu isiyoweza kuvumilika, na kwamba serikali zote katika nchi za Kiislamu hazina rasilimali isipokuwa mifuko ya raia. Hivyo basi, hakuna suluhisho wala maisha yenye heshima isipokuwa chini ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Ujumbe wa Uislamu uenezwe kote duniani.
Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Madani yenye kichwa: "Katiba ya Waislamu lazima iwe chanzo cha msukumo na sio akili za wanadamu." Mnamo Oktoba 23, 2022, kwenye kituo cha basi katika Soko Kuu, Ustadh Sowar alieleza maana ya katiba na umuhimu wake katika nchi zinazoheshimika. Ama kuhusu vijidola vya kikatuni, katiba haina thamani kwao, na kwamba Hizb ut Tahrir imetayarisha katiba ambayo chanzo chake ni Wahyi; Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake (saw).
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
- Click to open image! Click to open image!
https://hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/sudan/2750.html#sigProIdcc8e6e966d