Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Ripoti ya Mkao wa Kadhia za Ummah Julai 2022:

Dalili za Kuanguka kwa Dola ya Sudan… Kutoepukika Kusimamisha Khilafah

(Imetafsiriwa)

Licha ya kufungwa kwa barabara na madaraja, na kupelekwa kwa askari wengi katika mji mkuu, Khartoum, na maelezo ya kina, muamala thabiti, na mtazamo wenye taarifa ya matukio, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan ilifanya Mkao wa Kadhia za Ummah wa kila mwezi mnamo Jumamosi, 2/7/2022, wenye kichwa: " Dalili za Kuanguka kwa Dola ya Sudan… Kutoepukika Kusimamisha Khilafah."

Wazungumzaji ni pamoja na wakili na mshauri wa sheria, Ustadh Hatem Jaafar Abu Awab - mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na Ustadh Ahmed Al-Khatib - mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Afisa wa mkao alikuwa Ustadh Ibrahim Musharraf - mwanachama wa Afisi Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan.

Mzungumzaji wa kwanza, Bw. Hatem Jaafar (Abu Awab), aliwasilisha waraka wenye kichwa: “Sababu za Kuporomoka kwa Dola ya Sudan,” ambapo alieleza kwamba miongoni mwa ABC za fikra ya hali ya juu ya kisiasa ni kwamba dola zinaundwa kwa fikra, na mamlaka ndani yake hubadilishwa kwa mabadiliko ya fikra hizi, na akatoa mfano wa idadi ya dola zilizoegemezwa juu ya fikra ambapo Dola ya Kiislamu iliibuka mjini Madina juu ya itikadi ya Uislamu, na nchi za Ulaya zikaibuka juu ya itikadi ya kutenganisha dini na dola katika mfumo wa kisekula wa kirasilimali wa kidemokrasia.

Ustadh Hatem alionyesha kuwa sababu za udhaifu zinazotishia kuporomoka kwa dola ya Sudan ni kumi, ambazo aliziainisha katika sehemu mbili:

Ama sehemu ya kwanza, ni mambo ambayo mkoloni Kafiri mwenyewe aliyapanda, kuyasimamia na kuyadumisha, kabla ya kuyaacha majeshi yake katika kile kinachojulikana kuwa ni fahari ya uhuru, nayo ni:

1- Kuasisiwa kwa Sudan kwa msingi wa kanuni ya mkoloni... juu ya msingi wa kutenganisha dini na maisha, na kutokana nao kutenganisha dini na dola, hivyo hili lilifanywa katika sheria, kanuni, mitaala wa elimu, vyombo vya habari, na hata mijadala ya baadhi ya misikiti inayolenga hadhara ya nchi za kikoloni za Magharibi.

2- Kuweka idara za wanati na viongozi wa makabila na koo kama sehemu ya vyombo vya dola vilivyopewa dhamana ya kusimamia mambo.

3- Kugawanya ardhi, ikiwemo misitu na malisho, kwa msingi wa kabila, kwa kile kinachojulikana kama Al-Hawakeer.

4- Kuunda vyama vya kitaifa vinavyo tabanni miradi ya Kafiri mkoloni.

5- Harakati za kisilaha zinazoasi dhidi ya chombo cha dola.

Katika sehemu ya pili, Ustadh Hatem alieleza kuwa sababu za sehemu ya pili ambazo zilitokana na mvutano wa kimataifa kwa ajili ya ushawishi nchini Sudan. Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Amerika iliibuka kama nchi inayoshindana na Ulaya katika mapambano ya kimataifa juu ya makoloni. Walisaidiwa na uajiri na usaliti wa wanasiasa na watawala. Wakoloni walitengeneza zana kwa hili. Mavutano ya vyama, nguvu za kisiasa na viongozi wa kijeshi, yote haya yaliongeza mambo matano katika kuporomoka kwa dola hii:

1- Kupitishwa kwa majimbo na serikali ya kujitawala wenyewe kwa maeneo tofauti tofauti ya nchi, na jambo hilo lilifikia uamuzi wa kujitegemea uliosababisha kujitenga kwa kusini.

2- Laana ya utajiri; ambapo utajiri uligeuka kuwa laana, kwa sababu hakuna chombo chenye nguvu kuzuia mikono ya kuchezea utajiri wa nchi. Vijiji vilitelekezwa na watu kuuawa kwa sababu ardhi zao zilikuwa na utajiri wa mali.

3- Mazungumzo ya chuki ya ubaguzi wa rangi ya kisiasa yanayoeneza uhasama baina ya watu wa nchi hii, ambayo yanawasilishwa na wanasiasa na viongozi wenye tashwishi, wanaozuru balozi za kigeni na vibaraka wa wakoloni.

4- Kuchokoza maeneo, jamii na makabila, na kuyafanya kuwa ndio msingi wa hatua za kisiasa.

5- Kutengeneza njia kwa Magharibi kafiri kuwa dhidi ya Waislamu, na kuifanya msuluhishi kwa masuala yote ya nchi, kwani nchi za kikoloni na jumuiya zao ziliingilia mambo ya nchi, kama vile mabalozi na wajumbe wa Marekani na Uingereza, ujumbe wa Umoja wa Mataifa UNITAMS.

Ama mzungumzaji wa pili, Ustadh Ahmed Al-Khatib ambaye aliwasilisha waraka wa pili wenye kichwa: “Kutoepukika Kusimamisha Khilafah,” ambapo alifafanua nukta muhimu za kusimamishwa kwa dola yenye nguvu:

1- Uislamu ndio msingi pekee wenye uwezo wa kukabiliana na kuporomoka kwa dola, kwa sababu msingi ndani ya dola umeegemezwa juu ya kanuni, na Uislamu ni msingi mpana unaojumuisha maelezo yote ya maisha.

2- Kutoyapa makabila hisa katika utawala au idara, kwani hakuna mfumo wa utawala wa wanati katika Uislamu.

3- Kupiga marufuku mazungumzo ya ubaguzi wa rangi, kwani Uislamu unakataza na kuyaharamisha.

4- Vyama vya kisiasa ndani ya  Dola ya Khilafah vimejengwa juu ya imani ya Kiislamu, sio msingi wa kieneo au fikra yoyote inayopingana na Uislamu, kama vile demokrasia na nyenginezo.

5- Mfumo wa serikali katika Uislamu ni mfumo wa umoja, sio mfumo wa shirikisho.

6- Ni haramu kabisa kwa mgeni kuingilia mambo ya Waislamu.

Na akaashiria kuwa Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ina uwezo wa kushughulikia matatizo ya Sudan, ikiwemo sheria na vifungu vilivyo wazi, na kwamba Sudan ina utajiri mkubwa wa mali ikiwa itasimamiwa vyema na kurudishwa kwa watu wake kwa mujibu wa hukmu za Sharia.

Sehemu ya maingiliano:

Idadi kadhaa ya wanasiasa na wanahabari walishiriki katika maingiliano na majadiliano, na wazungumzaji hawa wawili wakajibu maswali na kupokea maingiliano na maswali kwa njia nzuri na maridhawa.

Mwishoni mwa mkao, mwendesha mkao, Ustadh Ibrahim Musharraf, aliwashukuru wahudhuriaji waheshimiwa kwa kushiriki kwao.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu