Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

The Blessed Land – Palestine A Massive March in support of the Ummah's Armies to Save Gaza!

Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina):

Matembezi Makubwa ya Kuomba Nusra kwa Majeshi ya Umma Kuiokoa Gaza!

Maelfu walishiriki katika matembezi makubwa yaliyoitishwa na Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) na watu mashuhuri wa mji wa Hebron (Al-Khalil) kuinusuru Rafah na kuokoa kile kilichobaki cha Gaza. Matembezi hayo yalianza kutoka Makutano ya Msikiti wa Al-Abrar kuelekea Mzunguko wa Ibn Rushdi katikati mwa mji wa Hebron, na washiriki walinyanyua bendera na kauli mbiu za kuutaka Umma na majeshi yake kuchukua hatua za haraka ili kuokoa Rafah na watu wa Gaza.

Katika Mzunguko wa Ibn Rushdi, kalima ilitolewa kushambulia njama na mauaji ya halaiki ambayo umbile nyakuzi linayatekeleza dhidi ya Gaza na watu wake. Mzungumzaji huyo aliukashifu utawala wa Misri kwa msimamo wake dhaifu, kwani ulidai kuwa uvamizi wa Rafah ni mstari mwekundu, wakati uvamizi huo ulipotokea, utawala wa Misri uliwaondoa askari wake, isipokuwa kwa kikosi ambacho dhamira yake ilikuwa ni kumtesa kila aliyejaribu kuvuka mpaka kutoka Gaza! Msemaji huyo alisisitiza kuwa, tawala za Kiarabu zimeshiriki katika uadui huo dhidi ya Gaza kupitia vifaa walivyotoa kwa umbile hilo nyakuzi na kulinda mipaka na anga na kusisitiza kuwa, watawala hao ndio chimbuko la matatizo na ndio msingi wa masaibu. Kalima hiyo ilijumuisha msisitizo kwamba matukio ya Gaza yamehuisha katika Umma ari ya jihad na kujitolea mhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kusisitiza kuwa ukombozi wa Palestina unawezekana bali hata ni rahisi. Mzungumzaji huyo alichukulia vuguvugu la vyuo vikuu vya Marekani kuwa limefichua viongozi wa nchi za Magharibi na wafuasi wao na uwongo wa hadhara yao.

Msemaji wa hadhira hiyo alituma ujumbe kwa jeshi la Misri, jeshi lililo karibu zaidi kwa yale yanayojiri Rafah, akisema: “Enyi jeshi la Misri, Al-Sisi na kundi lake wamewashinda nyinyi, na wamekengeuka kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika vita vya wazi dhidi ya dini na ufadhili wa makafiri, jambo ambalo limedhihirisha bila shaka kwamba yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini, basi hatushangai kwa uvamizi wake na uadui wake pamoja na Mayahudi dhidi ya watu wa Gaza, bali sisi tunashangazwa na kimya chenu dhidi yake mpaka sasa, ingawa gharama ya kimya ni kuangamizwa kwa watu wenu huko Gaza kutokana na njaa, kiu, mauaji na kuzingirwa, na juu ya hayo ni tusi kwa watu wa Misri na askari wake, na kabla na baada yake ni vita dhidi ya dini yenu. Basi mutawezaje kukaa kimya wakati nyinyi ni Al-Kinana wa Uislamu na washindi na wakombozi waliosalia, na msaada wa Ash-Sham katika historia... Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, vipi mnakaa kimya?”

Msemaji wa hadhira hiyo alihutubia Umma wa Kiislamu kwa kusema, Hakika Gaza inawasihi muape kwa Mwenyezi Mungu kwamba nifikieni, na muda hautoshi, basi enyi Umma wa Muhammad, rehema na amani zimshukie, itikieni wito wake, na muwe usaidizi kwake na muanze kubadilisha historia kutoka kwake. Ushindi, ukombozi na ufunguzi, hivyo tutaijaza dunia nuru na uadilifu baada ya kujazwa dhulma na ujeuri.

Mwakilishi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Jumatatu, 05 Dhu al-Qa’adah 1445 H sawia na 13 Mei 2024 M

Video ya Amali ya Matembezi

(Al-Khalili (Hebron) Inayaita Majeshi ya Umma Kuiokoa Gaza na Kutuma Risala kwa Jeshi la Misri!)

Sehemu ya Shughuli za Amali

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa maelezo zaidi, tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina):

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Ukurasa wa X wa Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu