Ijumaa, 17 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 16/08/2023

Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, turegeshee ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahumma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 29 Muharram 1445 H sawia na 16 Agosti 2023 M

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa Unadumisha Ushuru Mkubwa ili Kuhakikisha Malipo ya Riba

Mnamo Agosti 6, mkutano ulifanyika katika makao makuu ya Bodi ya Mapato ya Shirikisho ili kusuluhisha maswala ya ushuru kuhusiana na miamala ya mali isiyohamishika. Hali mbaya inayozidi kuongezeka ya uchumi imewasukuma watu mbali na uwekezaji katika sekta hii. Mwenyekiti alikiri kwamba chini ya mpangilio na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, msamaha wowote mpya wa ushuru huenda usiwezekane. Mfumo wa kirasimali wa Kimagharibi unahakikisha kwamba ulimwengu wa Kiislamu unazama katika malipo ya riba. Wakoloni kisha wanadai kuongezwa kwa ushuru kulipa riba. Khilafah kwa Njia ya Utume itasitisha malipo yote ya riba kuanzia siku ya kwanza na kuzingatia kuimarisha uchumi wetu. Mwenyezi Mungu ﷻ amesema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبا إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ]

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini.” [Surah a-Baqarah 278-279]

23 Muharram 1445 H - 10 Agosti 2023 M

Marekani Haijali Kuhusu ni Nani Anayetawala Maadamu Demokrasia Inabaki

Mnamo tarehe 7 Agosti 2023, msemaji wa Idara ya Wizara ya Kigeni ya Marekani alijibu kukamatwa kwa Imran Khan, akisema, "Tunaamini hilo ni jambo la ndani kwa Pakistan, na tunaendelea kutoa wito wa heshima ya kanuni za demokrasia." Marekani inategemea demokrasia kuidhibiti Pakistan, bila kujali ni nani anatawala. Demokrasia inaruhusu vibaraka wa Marekani kutunga sheria kulingana na maslahi ya wakoloni. Khilafah kwa Njia ya Utume itamaliza utumwa kwa wakoloni. Kila kifungu cha Katiba na kila sheria imevuliwa kutoka kwa Quran Tukufu na Sunnah ya Mtume ﷺ. Idara ya mahakama ya Khilafah inaweza kumuondoa Khalifa ikiwa atakiuka Uislamu. Baraza la Ummah huwahisabu watawala kuhusiana na utabikishaji wao wa Uislamu.

24 Muharram 1445 H - 11 Agosti 2023 M

Mithili tu ya Awamu ya Kwanza, Awamu ya Pili ya Ukanda wa Uchumi wa China-Pakistan Haitabadilisha Utajiri wa Kiuchumi

Waziri Mkuu alisema mnamo 7 Agosti 2023 kwamba uwekezaji wa China chini ya Ukanda wa Uchumi wa China-Pakistan (CPEC) uliongeza dolari bilioni 30. Alidai awamu ya pili ya mradi huo mkubwa itaunda fursa zaidi. Lakini, awamu ya kwanza haikubadilisha utajiri wa kiuchumi wa Pakistan. Kwa hivyo awamu ya pili itasababishaje ufanisi? Chini ya mfumo wa kiuchumi wa kibepari, kila mradi utanufaisha tu kipote cha tawala, wandani wao na wawekezaji wa kigeni. Tunahitaji Khilafah kwa Njia ya Utume itakayotabikisha mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu. Masuluhisho ya mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu yana uwezo wa kubadilisha utajiri wa Pakistan. Kwa karne nyingi, Khilafah ilitawala uchumi wa ulimwengu kwa sababu ya utabikishaji wa hukmu za Sharia ya Kiislamu.

25 Muharram 1445 H - 12 Agosti 2023 M

Mfumo wa Kilimwenguni wa Marekani Unahakikisha Maamuzi dhidi ya Maslahi ya Waislamu

Mnamo tarehe 7 Agosti 2023, Pakistan ilitoa ilani ya ‘Nguvu Kubwa na Udhuru’ kwa Iran, kusimamisha majukumu yake ya kimkataba, kuhusiana na mradi wa bomba la gesi la Iran-Pakistan (IP). Pakistan imeelezea kutokuwa na uwezo wa kutekeleza mradi huo, maadamu vikwazo vya Marekani juu ya Iran vinabaki mahali pake. Mradi huu umekuwa katika hifadhi kwa karibu muongo mmoja, licha ya uhaba wa nishati nchini Pakistan. Mfumo wa sasa wa kisiasa na kiuchumi wa kilimwengu, unaoongozwa na Marekani, hauruhusu dola ndogo ndogo kuchukua maamuzi, kulingana na maslahi yao wenyewe. Lazima tukatae mfumo huu wa Marekani na kuchukua mfumo badali wa Kiislamu wa kilimwengu, kwa kusimamisha Khilafah nchini Pakistan, na kuunganisha ardhi za Waislamu. Khilafah itakuwa dola kuu yenye nguvu ili tuweze kupata uwezo wetu wa kweli wa kiuchumi.

26 Muharram 1445 H - 13 Agosti 2023 M

Simamisheni Khilafah kwa ajili ya Uhuru wa Kweli kutokana na Ukoloni

Mnamo tarehe 14 Agosti 1947, Pakistan ilianzishwa kwa jina la uhuru. Lakini, serikali mtawalia zimeunda hali mbaya kiasi kwamba watu wengi wanaondoka Pakistan. Demokrasia inaruhusu serikali za Magharibi kuamua kila sera kuu. Ni Khilafah kwa Njia ya Utume ndiyo itakayofunga milango ya utumwa kwa Magharibi. Khilafah inahakikisha kwamba Quran Tukufu na Sunnah ya Mtume huamua katiba, sheria na sera. Mwenyezi Mungu ﷻ amesema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surah al Anfaal 8:24]

27 Muharram 1445 H - 14 Agosti 2023 M

Khilafah Pekee ndiyo Inayoweza Kurejesha Muundo wa Usalama wa Makabila

Baada ya mashambulizi makali kwa vikosi vya jeshi la Pakistan katika maeneo ya kikabila, wajumbe wengi wa Serikali ya Pakistan wamerudi kutoka Kabul, bila mafanikio. Licha ya operesheni kuu ishirini, mamia ya operesheni za kijasusi na majaribio kadhaa ya "kuvunja mgongo" ya wapiganaji wa kikabila, hali hiyo imezidi kuwa mbaya. Kila siku askari wetu na watu wetu wa makabila wanauawa. Hakuna mtu yeyote katika ngazi ya serikali ana suluhisho la kudumu kwa tatizo hili. Sera ya sasa ya maeneo ya kikabila imejengwa juu ya maagizo ya Marekani, ambayo yanagongana na hali halisi iliyoko ardhini. Makabila haya yamewahi kujisalimisha kwa Uislamu na mamlaka yake, Khilafah. Ni kupitia Khilafah pekee kwamba maeneo ya kikabila hayatakuwa tu na amani, yatakuwa na nguvu kubwa kwa Uislamu!

28 Muharram 1445 H - 15 Agosti 2023 M

Huku Kipote cha Watawala Kikibishana Kuhusu Waziri Mkuu wa Muda, Waislamu Wanaikimbia Pakistan

Mnamo tarehe 11 Agosti 2023, kuteuliwa kwa Waziri Mkuu wa muda kulifanyika. Ama kwa Waislamu, wanapiga kura kwa miguu yao. Majadiliano makuu sasa ni jinsi ya kuondoka nchini kwa sababu ya ugumu mkubwa wa kiuchumi. Mnamo 2021, karibu watu 225,000 waliondoka nchini. Mnamo 2022, 765,000 waliondoka, pamoja na wataalamu 92,000 walioelimika sana kama madaktari, wahandisi, wataalamu wa teknolojia ya habari na wahasibu. Mnamo 2023, 200,000 waliondoka katika miezi mitatu ya kwanza pekee. Tunapoteza watu wenye uwezo zaidi ambao wanaweza kutuongoza kwa mabadiliko ya kweli. Wao hutumia kiasi kikubwa cha pesa kutoroka au kuhatarisha maisha yao baharini. Wanakabiliwa na hatari mpya kwa Dini ya watoto wao huko Magharibi. Bila ya utabikishaji wa Uislamu, tuko katika mateso. Ni lazima tufanye kazi kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume sasa.

29 Muharram 1445 H - 16 Agosti 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu